ZITTO ALONGA KUHUSU SAKATA LA LWAKATARE NA BARUA YAKE ILIYOONEKANA JF.

Mbunge wa kigoma kaskazini, Naibu katibu Mkuu (CHADEMA) Zitto Kabwe

Mbunge wa kigoma kaskazini, Naibu katibu Mkuu (CHADEMA) Zitto Kabwe

Kutokana na sakata la Lwakatare na Barua ambayo ilidaiwa kuandikwa na zitto Mwenyewe kuzaga mtandaoni hasa kwa mara ya Kwanza kupitia kwenye mitandao ya kijamii Zitto amejitokeza na kutoa taharifa hifutayo…..

1. Niliandika barua kwa Katibu Mkuu wa chama mnamo tarehe 15 Machi 2013 kutaka chama kifanye uchunguzi wake wa ndani kuhusiana na ukweli wa video iliyowekwa kwenye mitandao inayoonyesha kuwa Kiongozi wetu mwandamizi anapanga mipango ya kumdhuru Mhariri wa moja ya magazeti hapa nchini. Sikuamini kabisa mambo yale na hivyo kutoa ushauri kwa chama kwamba tufanye uchunguzi wetu wa ndani ili kujiridhisha. Uchunguzi wa ndani ungetufanya kuweka mikakati wa namna bora zaidi ya kulinda chama dhidi ya njama zozote, za ndani au za nje ya chama.

2. Mapendekezo yangu ndani ya chama kamwe hayakulenga kumtosa ndugu Lwakatare wakati huu anakabiliwa na changamoto hii bali yalilenga kuhakikisha kuwa wakati tunamlinda na kumtetea ili haki itendeke, lazima tuhakikishe kuwa chama hakitaathirika na sakata hili kwa namna yeyote ile. Ni jukumu letu kuhakikisha sura (image) ya chama inabakia salama maana hatujui mikakati (game plan) ya maadui zetu kisiasa hasa baada ya kauli zao kwamba chama kitakufa kabla ya 2015 ambayo imerudiwa rudiwa sana. Ni lazima kutilia shaka (doubt) kila linalotokea sasa kwa kulipima kwa jicho la mbele zaidi. Ikumbukwe maneno ya Mwenyekiti wetu “Mwenyekiti Freeman Mbowe anataka ikithibitika kuwa Lwakatare alishiriki kurekodi mkanda huo iwe kwa kurubuniwa, ‘kushikishwa’ au kuingizwa mkenge, itamlazimu kuwajibika kwa kosa la kukosa umakini” (Gazeti la Jamhuri).

3. Barua ile ya tarehe 15 Machi 2013 ilikuwa ni ya ndani ya chama, haikuwa ya kiofisi bali ya Zitto Kabwe kwa chama, ilisainiwa na haikukusudiwa kuwa ‘public’. Nimeshangazwa sana kusikia na baadaye kuona barua yenye maudhui kama yale yale ya barua yangu kwa Katibu Mkuu imewekwa mtandaoni. Barua imewekwa masaa machache baada ya kikao cha Kamati Kuu kwisha ambapo tuliweka msimamo wa pamoja wa chama juu ya namna bora ya kushughulikia suala la Lwakatare kama chama. Wakati mweka barua anadai kuwa kulikuwa na mgawanyiko katika kikao, ukweli ni kwamba ajenda hiyo haikuwa na mjadala wenye mgawanyiko kabisa na msimamo wa chama ulipatikana kwa mwafaka bila mgawanyiko. Ni dhahiri kuwa maadui zetu walitaraji mgawanyiko na baada ya kushindwa sasa wanatengeneza mgawanyiko huo kwa kusambaza uwongo wenye uzandiki.


4. Baada ya kufanya uchunguzi mdogo nimegundua kuwa ID iliyoweka video ya Lwakatare mtandaoni na ID iliyoweka barua hii mtandaoni ni IDs za mtu mmoja. ‘Coincidence’ ya namna hii inashangaza na kushtusha, lakini inatuambia jambo moja kubwa ‘kwamba kuna kirusi ndani ya chama kilicho karibu sana na viongozi wa chama chenye kazi moja tu, yani kuonyesha kuwa CHADEMA hapako shwari, kuna migogoro na hatimaye kusambaratisha chama’. Kirusi hiki lazima kina nafasi andamizi au kipo karibu sana na viongozi waandamizi. Inawezekana kabisa kirusi hiki kinahusika na suala zima la Lwakatare katika kupanga, kuendesha na kutekeleza mpango mzima. Maswali kama ‘kwanini Dennis Msacky na Zitto ndani ya Video ya ‘Lwakatare’ lazima sasa yaanze kutafutiwa majawabu.

5. Natoa wito tena kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA kwamba, huu ni wakati wa kuwa na umoja na mshikamano kuliko wakati wowote ule katika uhai wa chama chetu. Chama cha Mapinduzi kitatumia njia zote kutugawa, kutugombanisha na kupenyeza chuki miongoni mwetu katika juhudi za wao kubakia madarakani. Umakini wa Kiongozi huonekana wakati wa changamoto kama hizi!

6. Msimamo wa chama umetolewa na Kamati Kuu iliyomaliza vikao vyake jana siku ya ijumaa tarehe 5 Aprili 2013. Huo ndio msimamo wangu pia! Kesi ya Lwakatare ipo mahakamani, chama kimeonyesha dhahiri kumwamini Jaji aliyekabidhiwa kesi hii, sasa tuache mahakama ifanye kazi yake na tusubiri hukumu. Msemaji wa chama kuhusu suala hili ni ndugu Tundu Lissu na amekuwa akitoa ufafanuzi kila inapohitajika.

Asanteni


Kabwe Z. Zitto,MP- Kigoma North, Tanzania. Chairman Public Accounts Committee,
Deputy Secretary General CHADEMA and Deputy Leader of the Opposition,
Shadow Minister of Finance
Mobile: +255756809535
Blog: http://www.zittokabwe.com

Advertisements

6 thoughts on “ZITTO ALONGA KUHUSU SAKATA LA LWAKATARE NA BARUA YAKE ILIYOONEKANA JF.

 1. big up mr MP.
  Nafuu mmeanza kuona huko juu kuwa kuna wa2 kazi yao ni kutafuta weak point ili kuwagombanisha. Ni bora viongozi waandamizi mkakubali kuwa mnaishi na kiruc kama vruc navyo vtawasambaratisha msipokuwa makini.
  Tanx Zito

 2. big up mr MP.
  Nafuu mmeanza kuona huko juu kuwa kuna wa2 kazi yao ni kutafuta weak point ili kuwagombanisha. Ni bora viongozi waandamizi mkakubali kuwa mnaishi na kiruc kama si virusi navyo vtawasambaratisha msipokuwa makini.
  Tanx Zito

 3. Kado Ombay…. je uwani kama amechelewa kutoa tamko lake na kuwacha watu wafikili mangi juu ya ukimya wake?

 4. kuna watu wanalipwa pesa nyingi chadema tishio kimeziba njia nyingi sana za watu kula hivyo watajitahidi kwa njia yeyote ile kuhakikisha wanakiua kama alivyosema naibu katibu mkuu huu ni wakati wa kushikana kwa nguvu ZOTE Mungu yu pamaja nasi .Mungu bariki na kuwaongoza viongozi wote wa chadema wenye nia na dhamira ya kweli katika ukombozi. Wewe ndiye unayejua mioyo na dhamira za watu matumaini ambayo watu wameyajenga kwa viongozi zikawe nira za kuwasimamia katika kutekeleza majukumu yao.Hivyo hivyo wale wote wanaotumika huku wakijua hali ya nchi ni mbaya vijana hawana ajira,maisha yako juu,kuongezeka kwa tabaka Mungu unawajua,na kama uluvyozihirika katika mambo mengi nafikiri na hili litazihirika.

 5. You really make it appear so easy with your presentation but I find this matter to be actually one thing
  that I feel I’d by no means understand. It seems too complex and extremely broad for me. I’m having a look
  forward for your subsequent publish, I’ll attempt to get the grasp of it!

Comments are closed.