CCM VIPANDE VIPANDE SAKATA LA LOLIONDO

BALOZI KAGASHEKIWaziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki

  • NCHEMBA AWATAKA WANANCHI, WAZEE WA MILA NA MADIWANI KUTOOGOPA MATAMSHI YA KAGASHEKI.

  • KAGASHEKI AKEJELI MATAMSHI YA NCHEMBA NA KUBAINISHA HUO HAUWEZI KUWA MSIMAMBO WA CHAMA BALI NI MAWAZO YAKE BINANFSI.

  • WAMASAI WACHUKIZWA NA DHIAKA YA CHAMA HICHO JUU YA MASLAI YAO.

  • BAADHI YA WANASHERIA WASHANGAZWA SERIKALI KUENDELEA KUTUMIA SHERIA YA ZAMANI KWANI MWAKA 2009 BUNGE LILIPITISHA SHERIA NAMBA 5 YA UHIFADHI, KATIKA SHERIA HIYO BUNGE LILIFUTA MAENEO YA UHIFADHI NA UWINDAJI WA KURATIBIWA.

Serikali kupitia kwa waziri mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki imetangaza kuchukua kilomita za mraba 1,500 za ardhi ya Tarafa ya Sale na Loliondo kwa ajili ya eneo maalumu la uhifadhi na uwindaji unaoratibiwa, huku ardhi hiyo ikitajwa kuwa ni mali ya vijiji.

Hatua hiyo ilifwatiwa na kuibuka kwa mgogoro kati ya Serikali, madiwani, wananchi na wazee wa mila wa maeneo hayo mahalia na kukilazimu cha tawala (Chama cha Mapinduzi) kuunda tume iliyoongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba kuzungumza na kusikiliza maoni ya wananchi.

Tume hiyo ilifanya mkutano na wananchi katika Kijiji cha Olorien Magaiduru, Tarafa ya Loliondo mwishoni mwa wiki, ikiwahusisha pia Mbunge wa Simanjiro Christopher ole Sendeka na Mbunge wa Longido, Michael Laizer.

Katika mikutano hiyo Mwigulu Nchemba alitoa kauli za kuonyesha kuwa serikali iko tayari kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu mgogolo huu ambao unazaidi ya muongo mmoja sasa.

“CCM inatambua wazi maslahi ya wananchi ndiyo maslahi ya taifa na kamwe hakuna maslahi ya taifa ambayo si maslahi ya wananchi.” Alinukuliwa Nchemba katika moja ya mikutano yake.

Nchemba aliwataka wananchi, wazee wa mila na madiwani kutoogopa matamshi ya Waziri Kagasheki badala yake Chama kinaangalia uzito wa tatizo.

Akizungumza kwa simu jana, Kagasheki ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Mjini (CCM), alisema kauli zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wakiwamo wabunge wa CCM, haziwezi kubadilisha msimamo wa Serikali.

Waziri huyo alisema kuwa Nchemba, ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi, anapaswa kuelewa kuwa Serikali haikukurupuka kuchukua uamuzi.

“Hayo maneno kama kweli yamesemwa na Nchemba, basi hayo ni mawazo yake na wala siyo msimamo wa chama. Mimi najua chama chetu kina taratibu za kujadili mambo na siyo kuanza kuzungumza nje ya vikao,” alisema na kuongeza:  

Hatua hiyo imepokelewa kwa mshangao na baadhi ya wakazi wa eneo la Loliondo na kuhoji dhamira ya Serikali kupitia chama hicho, wengi wakijiuliza kama Chama kupitia serikali kiliisha fanya maamuzi kwanini kiliunda tume.

M2S walipo wasiliana na baadhi ya wanasheria walishangazwa na serikali ya Jamuhuri ya Muungano kuendelea kutumia sheria ambazo ziliisha futwa tayari.

“Mwaka 2009 Bunge lilipitisha Sheria namba 5 ya Uhifadhi, katika sheria hiyo Bunge lilifuta maeneo ya uhifadhi na uwindaji unaotaratibiwa kote nchini.” Alisema mwanasheria mmoja ambaye akutaka jina lake liwekwe bayana.

Advertisements