KWA WALE WENYE VISIMBUSI TAMTHIRIA YA BUNGE YAREJEA TENA

  • BAADHI YA VIVUTIO KAMA REPOTI YA CAG VIMEONDOLEWA BAADA YA WAIGIZAJI KUANZA KUIGIZA UKWELI NA KUSABABISHA MADHARA KWA SERIKALI (KADHIA YA UKUSANYAJI WA KULA 70).

  • TAARIFA ZINASEMA UWASILISHAJI WA RIPOTI YA CAG BILA KUJADILIWA NI HATUA KUBWA AMBAYO AIWEZI KUBEZWA KUTOKANA NA KUWAEPUSHA WAIGIZAJI KUIGIZA KWA NJIA SALAMA BILA KUUMIZANA AU KULETA MADHARA KWA SERIKALI HILIYO MADARAKANI.

Episode ya 11 ya tamthiria ya watunga sheria za nchi hii unaanza leo mjini Dodoma, huku watayarishaji wake wakijigamba kufanya mabadiliko kadhaa ya taratibu za uendeshaji ambazo sitawezesha hata watoto kuangalia bila kuondoa radha na msisimko wake.

Taarifa iliyotolewa jana na Mratibu Msaidizi wa tamthiria kurugenzi ya (Habari), ilijinasibu kuwa bado wanapambana na  tishio la kutokuonyeshwa live kama baadhi ya wazandiki wa filamu hii walivyopendekeza. hata hivyo wazandiki hao wamefanikiwa kupunguza watazamaji kutokana na kuanzishwa kwa visimbusi (Vingamuzi) hali inayowapelekea watanzania wengi wasio kuwa na uwezo kujionea yanayojiri. Tamthiria hii itananza kurushwa tena leo live kupitia vituo pendwa vya TV na kukamilika Juni 28, mwaka huu huku ikilenga namna ya kuwakamua zaidi wananchi wake kwa kuwa neemesha wachache.

Kutokana na mabadiliko hayo, leo asubuhi wakati wa ufunguzi rasimi washiriki watapokea Azimio la Marekebisho ya Kanuni zake ambazo zinatarajiwa kuwasilishwa na Naibu Spika, Ndugu kazi.

Aliyataja mabadiliko hayo kuwa ni utaratibu mzima jinsi ya uwasilishaji bajeti za wizara, kwa mwaka huu itaanza Ofisi ya Waziri Mkubwa ambayo itajadiliwa kwa siku tano. “Siku zote tumezoea kuona Bajeti ya Sela-kali ndiyo inayotangulia kuanza kuwasilisha bajeti yake, utaratibu huo umeonekana siyo mzuri kutokana na mapendekezo ya wanazuoni wa kulinda maslahi yetu, hivyo tunaanza na wizara zingine ili Ngawila iwe ya mwisho,” ilisisitiza taharifa hiyo kutoka kurugenzi ya (Habari) ya filamu hiyo.

Hata hivyo, taarifa za zilizopatika kutoka ndani zinadai kanuni nyingi zinatarajia kubadilishwa na kwamba, iwapo zitapitishwa zitapunguza watazamaji wake kuichukia Sela-kali yao.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, kesho itakuwa siku maalumu kwa Ofisi ya Waziri Mkubwa kuwasilisha bajeti yake, ambayo itajumuisha wizara zote zilizo chini yake na inatarajia kujadiliwa kwa muda wa siku tano.

Mabadiliko mengine ni kuwasilishwa mezani kwa taarifa ya CAG kwa mwaka 2011/12 bila kujadiliwa hili kuondoa madhingila ya kuumizana waingizaji na kuakikisha atuta lifumuo tena baraza letu.

 

Advertisements