MAADHIMISHO YA MAUAJI YA KIMBARI YAFANYIKA DAR

 

Maandamano ya raia wa Rwanda wanaoishi nchini Tanzania pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakijipanga katika ukumbi wa New World Cinema tayari kuanza maandamano ya kuadhimisha miaka 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda kuelekea ukumbi wa mikutano wa Mlimani City. 

Picha juu na chini Umati wa maandamano yakielekea katika ukumbi huo.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Dr. Salim Ahmed Salim njiani kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano Mlimani City.

Mgeni rasmi Dr. Salim Ahmed Salim (wa tatu kulia) akiwa na balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Benjamin Ruganganzi (wa tatu kushoto) wakisubiri kupokea maandamo ya maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar.

Dr. Salim Ahmed Salim akipokea rasmi maandamano hayo.

Mgeni rasmi katika maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda Dr. Salim Ahmed Salim akizungumzia kumbukumbu ya mauaji hayo ambapo amesema historia ipo kwa ajili yetu sote kujikumbusha yaliyopita ili tuweze kupanga yajayo na kuwa mauaji ya Kimbari ni mzigo wetu sote na tunapaswa kujifunza kutambua alama za watu wa jamii moja kuanza kuhitilafiana na kutafuta namna ya kuzitatua kabla hazijaleta athari.

Na pia alichukua fursa hiyo na kunukuu maneno yaliyowahi kusemwa na Baba wa Taifa wa Tanzania Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere ” Ukweli ni kwamba kila sehemu ya Afrika ina ihitaji Afrika kwa pamoja na Afrika kama bara inahitaji kila sehemu ya bara la Afrika”.

MC katika maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari Usia Nkhoma akirekebisha kipaza sauti wakati mgeni rasmi akizungumza wakati wa maashimisho hayo.

Wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kumbukumbu ya maashimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari Rwanda.

Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Jama Gulaid ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF akizungumza wakati maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ambapo amesema dunia nzima itakuwa na siku maalum ya kukumbuka wahanga wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda kwa heshima ambayo ni alama ya kukumbuka athari za mauaji hayo na kuwa pamoja na walionusurika na kwa namna nyingine ni alama msingi ya kupongeza hatua zilizochukuliwa na jamii ya Wanarwanda kuungana pamoja.

Katika mazungumzo yake alinukuu maneno yaliyozungumzwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ” Katika maasdhimisho ya 19 ya mauaji ya Rwanda tunawakumbuka watu zaidi ya 800,000 wasio na hatia ambao walipoteza maisha yao na tutanendelea kuwaheshimu walionusurika na tutaendelea kuwa nao pamoja na kukemea wale wote waliohusika na tukio hilo, na kuwapongeza waliojitokeza kuzuia mauaji hayo yasiendelee”.

Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Benjamin Ruganganzi akitoa salamu zake kwa wageni waalikwa pamoja na watu waliohudhuria maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda na kuhakikisha kuwa wananchi wa Rwanda wataendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano pamoja na nchini zingine za Afrika Mashariki ili kuhakikisha tukio kama hilo halitajirudia tena.

Sehemu ya wageni waalikwa wakiwemo mabalozi mbalimbali wakimsikiliza Balozi wa Rwanda nchini (hayupo pichani).

Msemaji wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Mauaji ya Rwanda (ICTR) Bw. Roland Ammousouga akitoa kauli yake wakati wa maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda ambapo amesema kwa miaka 19 iliyopita watu wanaweza wakajisifu kazi iliyofanywa na mahakama ya ICTR kwamba imetimiza kilio cha maelefu ya waathirika na kuwa imesaidia katika kuleta upatanishi na kuijenga upya Rwanda sambamba na kuhamasisha amani na ulinzi katika ukanda wa Afrika wa maziwa makuu, wakati haikufanikiwa kuwakamata wale wote waliohusisha na mauaji hayo kwa kutoa itumia Rwanda kuwatafuta wahusika 6 waiojulikana walipo ili waweze kukabiliana na kesi zinazowakabili kinachojionyesha hapa ni kwamba ICTR inaashiria kwamba mapambano dhidi ya mazingira ya wahusika wengine 3 hawawezi kukamatwa.

Umati wa watu waliofurika (chini) katika maadhimisho hayo wakiwemo wanafunzi wa shule ya sekondari Jitegemee (juu).

Mmoja wa viongozi wa Dini akiomba dua ya kuwarehemu walipoteza maisha katika mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda.

Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Dr. Salim Ahmed Salim kuwasha mishumaa ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha wakati wa mauji ya Kimbari nchini Rwanda.

Advertisements