VIDEO CLIP YA SAKATA LA MWIGULU, LISSU KUHUSU UGAIDI LEO BUNGENI

KWA WALE WALIOKOSA KUANGALIA SAKATA LA MWIGULU, LISSU KUHUSU UGAIDI WANAWEZA KUBOFYA HAPO NA KUJIONEA HILIVYOKUWA.

Advertisements

SABABU ZA KISAYANSI KWA WANAWAKE KUVAA NGUO ZA KUONYESHA MAUMBO YAO.

40

14476-1

african women romantic wear

Wakati mwingne wanaume au watu tofauti hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nguo za kuonyesha maubile yao kwa kiasi kikubwa huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume.

Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba wanamapungufu kwa mfano sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo.

Wakati mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao. Hawa nao ni lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani waliyo nayo.

Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.

Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri.

Kuyatangaza huko humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani, kwani ataangaliwa sana na wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa.
Hebu angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa. Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya.

Huvaa nguo hizi ili kuonyesha kwamba, pamoja na ubaya wa sura zao, bado wao ni wazuri sana katika maeneo mengine ya mwili ambayo wanaume na hata wanawake wengi huyapenda au kutamani kuwa nayo.

Wengi hawavai tu nguo hizi za kubana kwa sababu ni fasheni, la hasha, wengi hili ni kimbilio la udhaifu wao

……NATOA HOJA KWA WALE WAKOSOAJI NAFASI NI YENU….

HABARI MPASUKO… BUNGENI MWIGULU ACHAFUA HALI YA HEWA KWA KUWAITA CHADEMA MAGAIDI

mwigulu nchemba bungeni

  • MWIGULU NCHEMBA:- Dr. SLAA NA MBOWE WAKAMATWE KWA UGAIDI!

  • SPIKA ASHANGILIA NA KUSEMA MKUKI KWA NGURUWE  WABUNGE WAMSHANGA.

  • TUNDU LISSU AMSHUSHUA SPIKA KWA KUSEMA SUALA LA MAWASILIANO KUHUSIANA NA KESI YA UGAIDI NA MARAFIKI ZAO HALIPO MAHAKAMANI.

Mwigulu Nchemba ameibuka na kile kilichotarajiwa kwa kuongelea suala la Mkanda wa Lwakatare huku akiwaomba Polisi kuwakamata viongozi wa CHADEMA kwa ugaidi

Akichangia bungeni muda huu Mwigulu Nchemba amesema yupo tayari kutoa ushahidi popote pale hata mbinguni kuthibitisha video ya Lwakatare jinsi alivyoipata, kiongozi wa CHADEMA aliyempa pia yupo tayari.

Amelitaka jeshi la polisi limkamate Mbowe kwa sababu ndiye anayewasiliana sana na LWAKATARE.

Comedy ni pale spika alipofunika kombe mwanaharamu apite kwa kuzima miongozo yote juu aliyokuwa anayasema Mheshimiwa huyo. Kasoro Utaratibu kutoka kwa Mheshimiwa Akunay na huku aki rule very politically.
Awali Mwigulu alisimama na kushambulia CHADEMA na viongozi wake hasa Mbowe kwa kumtaja jina na akisema hawa wote ni magaidi hali iliyopelekea Joseph Selasini aombe utaratibu kumtaka Mwigulu kufuta kauli yake ya kumshambulia Mbowe kibinafsi na kumtaka aache kuongele swala lililo mahakamani. Spika akuchukuwa hatua yoyote lakini pale aliposimama Tundu Lissu na kujibu hoja ya Mwigulu ndipo Spika alipo ibuka na kusema inatakiwa Mahakama ilindwe na kuheshimiwa bila kuingiliwa.
Akijibu hoja ya Spika kwamba masuala yaliyopo mahakamani yaheshimiwe:


“Mheshimiwa Spika, suala la mawasiliano kuhusiana na kesi ya ugaidi na marafiki zao humu ndani halipo mahakamani.”

Source: TBC1 Live coverage