SABABU ZA KISAYANSI KWA WANAWAKE KUVAA NGUO ZA KUONYESHA MAUMBO YAO.

40

14476-1

african women romantic wear

Wakati mwingne wanaume au watu tofauti hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nguo za kuonyesha maubile yao kwa kiasi kikubwa huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume.

Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba wanamapungufu kwa mfano sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo.

Wakati mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao. Hawa nao ni lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani waliyo nayo.

Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.

Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri.

Kuyatangaza huko humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani, kwani ataangaliwa sana na wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa.
Hebu angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa. Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya.

Huvaa nguo hizi ili kuonyesha kwamba, pamoja na ubaya wa sura zao, bado wao ni wazuri sana katika maeneo mengine ya mwili ambayo wanaume na hata wanawake wengi huyapenda au kutamani kuwa nayo.

Wengi hawavai tu nguo hizi za kubana kwa sababu ni fasheni, la hasha, wengi hili ni kimbilio la udhaifu wao

……NATOA HOJA KWA WALE WAKOSOAJI NAFASI NI YENU….

Advertisements

6 thoughts on “SABABU ZA KISAYANSI KWA WANAWAKE KUVAA NGUO ZA KUONYESHA MAUMBO YAO.

  1. Mkuu ngoja wenyewe waje, cjui kama utaweza makombora yao! Mi huyooo napita hiviii…………………… ……….

  2. Sasa ndugu yangu wewe unadhani kwanini wanaamua kuficha udhaifu huwo kama kweli sio kutafuta soko??? Maana kwa uhalisia kichu chochote kinapo kuwa na madhaifu, mapungufu au kasoro nyingine hata wewe huto kipenda kama kisicho na kasoro na kama unakiuza nidhahiri kuwa soko lake linapungua. So ili soko lisipungue inabidi utafute nyongeza au uangalie jinsi yakuziba hayo mapungufu ndungu. Na kwajinsi hiyo sisi wanaume huwa tunawanunua wanawake na kwa mila na desturi zetu mwanaume hutoa mari kwa mwanamke na wazazi wetu ndiyo hupanga kulingana na uzuri wake, elimu yake N.K na zaidi dada zetu wanajua kabisa kwa njia hizi nitamnasa mwanaume tu, na kwakuwa kila mtu ana mapungufu na kasoro zake basi anatafuta njia za kuziba mapungufu ili apate soko kwa wanaume dhaifu. Na hayo madhaifu unayo ongelea yako kwa wanaume sio wanawake. So wanawake hufanya hivyo kutafuta soko ila kwa wale wasio tafuta soko utakuta wametulia kabisa na wanavaa kiheshima na kwa wanaume pia walio tulia hufuata tabia na sio uzuri wa macho kwani hakuna mbaya duniani.

  3. Kunamabo mengine hayasemwi kama yalivyo ndugu yangu. kunadada zetu wengi siyo wanakosa wanaume au wanaitaji wanaume bali ni kuitaji mtazamo wa jamii juu yao pamoja na kujijengea security kuwa na yeye yumo na jamii inatambuwa uwepo wake likiwemo la muonekano.

Comments are closed.