NDEGE YA MAREHEMU MAWALA YAANGUKA ARUSHA NA KUUWA RUBANI WAKE

m2s breaking news

Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba ndege iliyokuwa inamilikiwa na Wakili maarufu Marehemu Nyaga Mawala aliyefariki wiki 3 zilizopita na kuzikwa huko Nairobi imeanguka ikiwa katika hatua za mwisho za kutua (final approach) katika kiwanja cha ndege cha Arusha.

Taarifa zinasema kuwa ndege hiyo ilikuwa na rubani peke yake anayejulikana kwa jina la Jamal B S, au maarufu kama Bob Sambeke aliyekuwa anatokea West Kilimanjaro.

Maelezo zaidi kuhusu ajali hiyo ni kwamba ndege hiyo ilijaribu kutua baada ya masaa ya kawaida ya kufunga kiwanja(saa 12.30jioni) kupita.

UPDATE:

BOB SAMBEKE ALIYEKUWA RUBANI WA MAREHEMU WAKILI MAWALA. NYAGA NAYE KAFARIKI DUNIA MUDA MFUPI ULIOPITA.

Huu ndiyo mti unao sadikiwa kugongwa na ndege kabla ya kupata ajari

Huu ndiyo mti unao sadikiwa kugongwa na ndege kabla ya kupata ajari

NDEGE ARUSHA 02

NDEGE ARUSHA 03

NDEGE ARUSHA

Advertisements

WIZI MWINGINE KAMA WA EPA WAGUNDULIWA KWENYE RIPOTI YA CAG

Waziri kivuli wa Fedha, Mweshimiwa Zito Zuberi Kabwe

Waziri kivuli wa Fedha, Mweshimiwa Zitto Zuberi Kabwe

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Shilingi bilioni 620 za Deni la Taifa hazina maelezo

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ametoa taarifa yake ya mwaka 2011/2012 na kuonyesha kuwa kuna skandali kubwa sana katika akaunti ya Deni la Taifa. Nanukuu

‘Uhakiki wa mchanganuo wa madeni ya Taifa kama ulivyokuwa tarehe 30 Juni, 2012 ulibaini kuwepo kwa marekebisho ya deni ya shilingi 619,803,554,183.91 ambayo uongozi haukuweza kutoa maelezo ya kuridhisha.’ (Taarifa ya CAG, Ripoti ya Serikali Kuu 2011/2012 uk 158). Mwisho wa Kunukuu

Katika Taarifa yake hiyo CAG anaendelea kuonyesha kuwa Deni la Taifa linazidi kukua na mwaka unaoishia mwezi Juni 2012 deni lilikuwa kwa asilimia 17 kutoka mwaka unaoishia mwezi Juni 2011.

Kukosekana kwa maelezo ya kuridhisha kuhusu zaidi ya nusu trilioni za Deni la Taifa ni jambo linalopaswa kutiliwa mashaka makubwa, kuchunguzwa na kupata majawabu stahiki. Tafiti mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa kuna mahusiano makubwa sana kati ya Deni la Taifa la utoroshaji wa fedha kwenda kwenye mabenki ya ‘offshore’. Katika kitabu cha ‘Africa’s Odious Debts: How Foreign Loans and Capital flight bled a continent’ kilichoandikwa mabwana Leonce Ndikumana na James Boyce imeonekana kwamba Deni la Taifa huchochea utoroshwaji wa Fedha kwenda kuficha nje ya Tanzania.

Mabilioni haya kwenye akaunti ya Deni la Taifa yanashtusha sana. Kambi ya Upinzani Bungeni kwa miaka miwili mfululizo imekuwa ikitaka ukaguzi maalumu kwenye akaunti za Deni la Taifa lakini Serikali imeshindwa kufanya hivyo. Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya PAC pia nimemtaka CAG afanye ukaguzi huu maalumu.

Kambi ya upinzani Bungeni ilisema hivi katika Bajeti yake kivuli 2012/13:

 

DENI LA TAIFA

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inasikitika kwa serikali kuendelea kutengeneza madeni kwa Taifa kwa kuendelea kukopa zaidi kwa matumizi ya kawaida ya serikali. Wakati Serikali inasisitiza kwamba Deni letu linastahmilika, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali anaonyesha mashaka makubwa sana kutokana na kasi ya kukua kwa Deni la Taifa. Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaonyesha  kuwa Deni la Taifa linazidi kuongezeka kwa asilimia 38% kutoka shilingi trillion 10.5 mwaka 2009/2010 hadi shilingi trillion 14.4 mwaka 2010/2011. Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha Deni la Taifa limefikia shilingi trillion 20.3 mpaka ilipofika mwezi Machi mwaka 2012. Ukisoma taarifa ya Mwezi wa Mei 2012 ya Benki Kuu ya Tanzania, Deni la Taifa sasa limefikia shilingi trillion 22.

Mheshimiwa Spika, Suala hapa sio ustahmilivu wa Deni kama inavyodai Serikali bali ni kwamba tunakopa kufanyia nini? Bajeti ya Mwaka 2012/13 inayopendekezwa inaonyesha kwamba Serikali itakusanya shilingi trilioni 8.7 kama makusanyo ya ndani na itatumia shilingi trilioni 10.6 kama matumizi ya kawaida. Ni dhahiri kwamba sehemu ya mikopo ambayo serikali inachukua sasa itakwenda kwenye matumizi ya kawaida. Hatutaki mikopo kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya posho, kusafiri, magari nk. Tuchukue mikopo kuwekeza kwenye miradi itakayokuza uchumi na kuzalisha kodi zaidi. Bajeti inaonyesha kwamba Serikali itakopa shilingi takribani trillion 5 mwaka 2012/13.  Serikali ikubalikutekeleza mapendekezoya Kambi ya Upinzani ya kuimarisha ukusanyaji  wa kodi na kupanua wigo wa kodi katika maeneo muhimu kama sekta ya madini na mawasiliano, kuzuia misamaha ya kodi, kutokomeza ukwepaji kodi, na kuepuka matumizi mabaya ili kuepuka madeni yasiyo ya lazima.

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inapenda kusisitiza kwamba Bunge lifanye ukaguzi maalumu kuhusu akaunti ya Deni la Taifa ili kuweza kubaini ukweli kuhusu ustahmilivu wa Deni na mikopo ambayo Serikali inachukua kama inakwenda kwenye Maendeleo na miradi ipi na kama miradi hiyo ina tija. Vilevile tumependekeza kwamba Mikopo yote ambayo Serikali inachukua iwe inapata idhini ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi au Bunge litunge sharia ili kiwango cha juu cha kukopa ambacho Serikali haipaswi kuvuka. Kuiacha Serikali inaendelea kukopa bila mpango ni kuliweka Taifa rehani na kupeleka mzigo wa kulipa madeni haya kwa kizazi kijacho. Hatuwezi kukubali Wazee wetu waishi maisha yao, waishi maisha yetu na pia wakope maisha ya watoto wetu. Mwisho wa kunukuu.

Kambi ya Upinzani inarejea kutaka ukaguzi maalumu kuhusu akaunti za Deni la Taifa na maelezo ya kina ya Serikali kuhusu shilingi 620 bilioni ambazo hazina maelezo kwenye Deni la Taifa. Hatuwezi kukaa kimya kuona Watanzania wanabebeshwa madeni ambayo kimsingi ni madeni bandia yanayotajirisha watu wachache wenye uwezo na ujasiri mkubwa wa kuiba, kupora nakufisidi hazina ya Taifa letu.

Kabwe Z. Zitto, MP- Kigoma North, Tanzania. Chairman Public Accounts Committee,
Deputy Secretary General CHADEMA and Deputy Leader of the Opposition,
Shadow Minister of Finance
Mobile: +255756809535
Blog: http://www.zittokabwe.com

UZINDUZI WA KANDA YA DAR ES SALAAM (CHADEMA) LIVE UPDATES

KONGAMANO LIVE

Baadhi ya watu ambao wemeisha fika  Wengine bado wako nje wanajiandikisha, bila shaka na wengine wako njiani wanakuja.

M2S kwa kushirikiana na Blog Pacha za Jamiiblog na Community pamoja na Jamiiforum tunawaleteeni Uzinduzi wa wa Kanda ya Dar es salaam unaofanyika Ubungo Plaza katika Hotel ya Blue Pearl Jijini Dar es Salaam. Tupo hapa kuwaletea live updates. Kwa wale wanaoweza kufika karibuni sana.

Watu wa Dar es salaam wameweka utaratibu wa kila mshiriki kuchangia Tsh 5000 na 10,000 kwa kila mshiriki kama gharama za kutunisha mfuko wao wa Kanda.

Mgeni rasmi ni Mwenyekiti Taifa Mh. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr. Wilbrod Slaa.

Wageni wengine maalum ni Wabunge wa Dar es salaam na Wajumbe wa Kamati Kuu waliopo Dar es salaam. Mpaka sasa namuona Mh. Mabere Marando.

=============
UPDATES
=============

QuoteView Post

Mh. John Mnyika ndio amemaliza kutoa salamu zake. Sasa anazungumza Henry Kileo katibu wa muda wa Kanda. anatoa mrejesho wa tokea Baraza Kuu nini kimefanyika hadi leo katika mchakato wa uundaji wa Kanda hii

QuoteView Post

Hery Kileo ndio amemaliza nae kutoa taarifa nzima ya mchakato wa uundwaji wa Kanda hii. Sasa ni Halima Mdee ambae alikuwa M/kiti wa Kamati ya uteuzi wa viongozi wa Kanda. Anatangaza  uteuzi ulivyokwenda.

Sasa anaongea M/kiti wa Chama Mkoa wa Pwani Mh. Said Ukwezi yeye anatoa taarifa ya Maandalizi ya Mkutano wa hadhara wa kesho utakaofanyika Kibaha Mjini. Anasema maandalizi ni mazuri na watarusha njiwa wawili weupe kuashiria kazi ya M4C imeanza rasmi. anawakaribisha wadau wote Kibaha kesho. Anapigiwa makofi mengi na wajumbe

QuoteView Post

Sasa anaongea Mtafiti na Mwanamikakati wa Chama juu ya nini hasa kinatarajiwa katika Kanda hii ya DSM pamoja na wajibu walionao wanaKanda baada ya utafiti kufanyika. Amepewa dakika 15 mpaka 20. Anasema operesheni katika kanda hii itafanyika kwa njia ya mitandao, aridhini na hata angani. ambapo watapita mtaa kwa mtaa, mtu kwa mtu. Anasema changamoto kubwa ni fedha na rasilimali watu. anasema kutafanyika M4C fundraising ambayo itamhusisha kila mtu. Anasema suala la katiba ndio itakuwa agenda kuu katika mwaka huu na mwakani.

QuoteView Post

Dr. Slaa anawasalimu wananchi hapa ili amkaribishe M/kiti. Slaa anasema Magaidi jana wameonekana Bungeni. Anasema CHADEMA wako Makini kuliko serikali ya CCM, kuliko Usalama wa Taifa, Kuliko CCM wenyewe na umakini huo ndio utakaoiingiza CHADEMA madarakani. Anasema Serikali ndio inafadhili ugaidi na ndio magaidi wenyewe na kama si hivyo wasingempeleka Ofisa wake chumba namba 334 kumhonga ili atengeneze ushahidi wa kesi ya Lwakatare. Anasema wanazo taarifa zote muhimu kuhusu mambo serikali inayopanga dhidi ya CHADEMA. Amemkaribisha M/kiti Taifa nae ndio anatoa hotuba yake!

Quote View Post

Mbowe anaanza kwa kutoa salam toka Bungeni. Anasema CHADEMA sio mpango wa Mbowe, wala wa Slaa bali ni mpango wa Mungu. Anasema Serikali inateka Mchakato wa Katiba lakini wakumbuke CHADEMA haina bunduki lakini ina watu. Anasema mpaka April 30 kama serikali haitaleta taarifa muhimu Bungeni juu ya mchakato wa Katiba CHADEMA itajitoa katika mchakato huo na itamwambia Prof. Baregu arudishe gari, nyumba na ajitoe.

Anasema walianza na Propaganda za Chama cha Mbowe, mara cha Wachaga, mara cha Kaskazini, mara cha Wakristo sasa wanadai cha Magaidi. Mbowe anasema hawezi kupoteza muda wake kumzungumzia mtu kama Mwigulu Nchemba atampandisha sana chati. Anaomba asimzungumzie mtu kama Mwigulu

Mbowe anasema udini katika nchi hii umeanzishwa na Kikwete wala hakuna haja ya kumumunya maneno. Anasema wana majina ya vikundi vilivyofadhiliwa na Ikulu kuzunguka nchi nzima kueneza sumu hii ya udini. Anasema muda si mrefu watawataja kwa majina kama watalazimishwa kufika hapo.

Anasema Pinda hafai kuendelea kuwa Waziri Mkuu kwa sababu anaunda tume kuchunguza tatizo la kufeli wakati tayari ana ripoti ya tume kama hiyo iliyoundwa mwaka jana na hajaifanyia kazi. Anasema CHADEMA imejenga historia leo kwa watu kuingia kwenye mkutano wa Chama cha siasa kwa kulipia kiingilio cha Tsh 5000 na 10,000 na kujigharamia chakula. Anasema Viongozi wasizue wanachama wapya na anawapongeza Marando na Safari kwa kukubali kuiongoza Kanda ya Dar es salaam. Anasema Kanda zimeundwa kuwapa wanachama wengi zaidi fursa ya kuongoza na kwamba uongozi wa Chama sio Mbowe na Slaa tu bali kila Mwanachama anaweza kupewa fursa na akaiongoza vizuri

QuoteView Post
PICHA MBALIMBALIA KUONYESHA MATUKIO KATIKA PICHA KAMA YALIVYOTOKEA PICHA ZOTE KWA MSAADA WA BLOG PACHA ZA community blog na jamiiblog KWA HISANI YA jamiiforum.
Mijadala ya hapa na pale kabla ya kuanza mapema asubuhi
chadema 1
chadema 2
chadema 3
chadema 4
chadema 5
chadema 6

Kwaniaba ya blog za Community.co.tz, jamiiblog.co.tz pamoja na hisani kubwa ya Jamiifolum tunawashukuru wote walituwezesha kuwaletea mkutano huu live. … usiku mwema…..

{VIDEO} KUFWATIA YALIYOTOKEA BUNGENI DR. SLAA AJIBU KWA KUSEMA CHADEMA WAKO MAKINI

Dr. Slaa alipokuwa akiwasalimia wananchi kwenye kongamano la uzinduzi wa kanda ya Dar es Salaam  kabla ya kumkaribisha M/kiti. Slaa anasema Magaidi jana wameonekana Bungeni. Anasema CHADEMA wako Makini kuliko serikali ya CCM, kuliko Usalama wa Taifa, Kuliko CCM wenyewe na umakini huo ndio utakaoiingiza CHADEMA madarakani. Anasema Serikali ndio inafadhili ugaidi na ndio magaidi wenyewe na kama si hivyo wasingempeleka Ofisa wake chumba namba 334 kumhonga ili atengeneze ushahidi wa kesi ya Lwakatare. Anasema wanazo taarifa zote muhimu kuhusu mambo serikali inayopanga dhidi ya CHADEMA!

MISS UNIVERSE YAPONGEZWA NA BASATA

Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai (wanne kutoka kushoto) akisisitiza jambo wakati wa kuwakilisha tathmini ya mashindano Miss Universe Tanzania mbele ya maofisa wa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) makao makuu ya baraza hilo Ilala jijini

Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai (wanne kutoka kushoto) akisisitiza jambo wakati wa kuwakilisha tathmini ya mashindano Miss Universe Tanzania mbele ya maofisa wa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) makao makuu ya baraza hilo Ilala jijini

Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai (kulia) akiwakilisha tathmini ya mashindano ya Miss Universe Tanzania mbele ya maofisa wa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) ambao hawapo pichani makao makuu ya baraza hilo Ilala jijini. Kushoto ni Mratibu Msaidizi wa mashindano hayo, Mwanakombo Salim

Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai (kulia) akiwakilisha tathmini ya mashindano ya Miss Universe Tanzania mbele ya maofisa wa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) ambao hawapo pichani makao makuu ya baraza hilo Ilala jijini. Kushoto ni Mratibu Msaidizi wa mashindano hayo, Mwanakombo Salim

Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai (kulia) akisisitiza jambo wakati wa kuwakilisha tathmini ya mashindano Miss Universe Tanzania mbele ya maofisa wa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) ambao hawapo pichani makao makuu ya baraza hilo Ilala jijini. Kushoto ni Miss Universe 2011, Nelly Kamwelu

Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai (kulia) akisisitiza jambo wakati wa kuwakilisha tathmini ya mashindano Miss Universe Tanzania mbele ya maofisa wa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) ambao hawapo pichani makao makuu ya baraza hilo Ilala jijini. Kushoto ni Miss Universe 2011, Nelly Kamwelu

Baraza la Sanaa nchini (BASATA) limeipongeza kampuni ya Compass Communications kwa mafanikio makubwa waliyopata pamoja na kuandaa mashindano ya urembo nchini kwa muda mfupi.

Akizungumza katika kikao cha tathimini ya mashindano ya Miss Universe yaliyofanyika juzi makao makuu ya Basata,  Afisa Sanaa baraza hilo Malimi Mashili  alisema kuwa pamoja na kampuni ya Compass kuanza kushiriki katika mashindano ya Miss Universe mwaka 2007, waliweza kufanya vyema na kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake.

Alisema kuwa mrembo wake, Flaviana Matata ambaye alimaliza katika hatua ya sita bora, mpaka sasa anafanya vyema nje ya nchi katika sekta ya maonyesho ya mavazi au wanaminitindo.

Mbali na mafanikio hayo, Mashili alisema kuwa usimamizi bora wa kampuni hiyo imewafanya warembo kuwa na tabia njema na kuepukana na skendo mbali mbali ambazo zinawatokea warembo waliopitia mashindano tofauti na mashindano mengine ya urembo nchini.

“Ni mashindano bora ambayo kwa kweli yametuvutia sana, tunaomba muongeze bidii ili kuyaboresha zaidi kwani mashindano haya kwa sasa ni makubwa na warembo wengi wanayaulizia jinsi ya kujiunga nayo,” alisema Mashili.

Pia aliwataka waandaaji wa mashindano hayo kutafuta udhamini wa televisheni ambayo itaonyesha moja kwa moja ‘live’ mashindano hayo ili kupanua wigo wa wafuatiiaji wake kama ilivyo kwa mashindano mengine ya urembo.

 Mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai aliishukuru Basata kwa usimamiaji bora wa mashindano katika sekta ya sanaa nchini na kusema kuwa watajiathidi kuongeza wigo wa washiriki kaika mashindano ya mwaka huu.

Maria alisema kuwa pamoja na changamoto zote wanazokabiliana nazo alisema kuwa wameongeza mikoa saba zaidi na kufanya jumla ya mikoa 14 ambayo warembo wake watawania mataji mbali mbali mwaka huu.

Mikoa hiyo ni Katavi, Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Dodoma, Arusha, Mtwara, Dar es salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Kagera na Manyara.

Kwa mujibu wa Maria, Miss Universe Tanzania imeweka mikakati ya kuwaendeleza warembo ambao hawakufanikiwa kushinda katika mashindano hayo. Alisema kuwa mpango wao mkuu ni kuwapa msaada wa kielimu kwa kushirikiana na asasi mbalimbali za hapa nchini hususani zinazoshughulika na masuala haya ya elimu.

TANZANIA LOSES 305.3bn/- AS PROF. MUHONGO FAILED TO KEEP IS PROMISE OVER THE EXCUSE OF NO LEGAL REQUIREMENTS TO ENFORCE THE PAYMENT

Minister for Energy and Minerals, Professor Sospeter Muhongo

Minister for Energy and Minerals, Professor Sospeter Muhongo

OVER 305.3bn/- in capital gain tax which the Australian-based Mantra Resources Limited owes the government will not be paid after all because there is no legal requirements to enforce such payment.

Minister for Energy and Minerals, Professor Sospeter Muhongo told ‘Daily News on Saturday’ that lack of the capital gains law has made it difficult to force Mantra pay the tax which emanates from its 980 million US dollars (1.58trn) earning made after selling a majority stake to Russian-based Atomredmetzoloto (ARMZ).

So Zitto wants us to stop the whole mining process until Mantra pays the capital gains tax? It’s not practical because we have no law to enforce it,” said Prof Muhongo over phone from Brussels, Belgium where he has been on official business.

Prof Muhongo said much as he would like to see Mantra pay Treasury the tax money required, it’s a pity that the country has no legislation to back up such payment hence losing out. “Many other companies have sold each other shares without paying capital gains tax because of absence of the law,” argued the Minister.

Prof Muhongo had promised parliament during last year’s budget session that a special mining licence will not be granted to Uranium One until all applicable taxes are paid. Kigoma North lawmaker, Zitto Kabwe who is also the deputy leader of the official opposition in Parliament has reignited debate over the controversy after accusing Prof Muhongo of deceiving parliament. Mr Kabwe who has since officially written to the Speaker, Ms Anna Makinda, said Mantra has over 300bn/- in government taxes.

“This sum of money is enough to have solved the problem of teachers’ housing countrywide and pay their arrears, it’s also enough to build a road from Manyoni to Itigi in Singida region to bitumen standards,” he noted. He argued that as per parliament standing orders, the Minister should update parliament on the matter and debate should follow to allow lawmakers air their frustration at this sort of playing Father Christmas with the country’s resources.

Minister Muhongo promised parliament last year that his ministry’s experts were meeting with Uranium One representatives and State Mining Corporation (Stamico) to discuss a number of issues, including the project’s shares that would also involve local communities in the mining area.

“I can assure you that the licence has not been issued and we are very careful with the current negotiations,” said Prof Muhongo. The minister pointed out that his team was shifting from the ‘business as usual’ practice to ensure that the nation and communities benefit from mining.

Tanzania Revenue Authority (TRA) was still pressing Mantra Resources to pay 20 per cent taxes after selling its majority stake to ARMZ in 2011.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSIANA NA TUKIO LA MAUAJI YA MFANYABIASHARA WA MADINI ARUSHA

TUKIO LA MAUAJI

MNAMO TAREHE 09/04/2013 MUDA WA SAA 2:30 USIKU HUKO LEMARA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA, MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA JUMA S/O RASHID (45) MFANYABIASHARA WA MADINI NA NI MKAZI WA SOMBETINI, ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GEORGE KARAU MARRIE (38) MFANYABIASHARA NA NI MKAZI WA LEMARA.

UCHUNGUZI WA AWALI ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA ULIBAINI KWAMBA, MAREHEMU JUMA S/O RASHID, FRANCIS S/O EDWARD (37) NA MTUHUMIWA GEORGE KARAU MARRIE WALIKUWA NI WASHIRIKI KATIKA BIASHARA YA MADINI YA TANZANITE.

INASEMEKANA KWAMBA BAADAE WALIINGIA MAKUBALIANO AMBAPO MTUHUMIWA ALIKABIDHIWA MADINI AMBAYE THAMANI YAKE BADO HAIJAJULIKANA NA FRANCIS S/O EDWARD PAMOJA NA MAREHEMU ILI AKAUZE.

JUZI TAREHE 08/04/2013 MTUHUMIWA GEORGE S/O KARAU MARRIE ALIWASILIANA NA MAREHEMU PAMOJA NA FRANCIS S/O EDWARD NA KUWAAHIDI KUWALIPA FEDHA ZAO SIKU YA TAREHE 09/04/2013.

TAREHE 09/04/2013 MUDA WA SAA 2:15 USIKU, MAREHEMU PAMOJA NA MWENZAKE FRANCIS S/O EDWARD MWASHUYA WAKIWA NA GARI AINA YA HONDA LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 230 CBE WALITOKA MAENEO YA MJINI NA KUELEKEA MAENEO YA LEMARA. WALIPOKUWA NJIANI WALIKUTANA  NA MTUHUMIWA AMBAYE ALIPANDA GARI HILO HILO NA KUKAA KITI CHA NYUMA NA MAREHEMU ALIKUWA ANAENDESHA GARI HUKU MWENZAKE AKIWA AMEKAA KITI CHA MBELE CHA UPANDE WA KUSHOTO. WOTE WALIKUWA WANAELEKEA LEMARA NYUMBANI KWA MTUHUMIWA ILI AKAWAPATIE FEDHA AMBAZO ALIKUWA ANADAIWA.

WALIPOFIKA ENEO LA TUKIO, MTUHUMIWA ALIAMURU GARI HILO LISIMAME NA KISHA AKATOA BASTOLA NA KUMPIGA MAREHEMU SEHEMU YA KIFUANI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO NA KISHA KUMJERUHI KWA RISASI FRANCIS S/O EDWARD MWASHUYA SEHEMU YA KICHWANI.

MARA BAADA YA MAUAJI HAYO, MTUHUMIWA ALIMPORA  FRANSCIS S/O EDWARD FEDHA TASLIMU TSH 400,000/=, MADINI YA TANZANITE AMBAYO THAMANI YAKE BADO HAIJAJULIKANA NA KISHA KUCHUKUA HATI YA NYUMBA NA KUTOKOMEA MAENEO YA LEMARA BWAWA LA MAJI MACHAFU.

KUFUATIA TAARIFA JUU YA TUKIO HILO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WALIOKUWA DORIA MAENEO JIRANI WALIKWENDA KATIKA ENEO HILO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA KUFANIKIWA KUPATA MAGANDA MAWILI YA RISASI. JESHI LA POLISI MKOANI HAPA LINAENDELEA KUFANYA UPELELEZI PAMOJA NA KUMTAFUTA MTUHUMIWA.

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI CHA HOSPITALI YA MOUNT MERU KWA AJILI YA UCHUNGUZI WA DAKTARI NA MAJERUHI AMELAZWA KATIKA HOSPITALI HIYO AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HUKU HALI YAKE IKIENDELEA VIZURI.

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI,
(SSP) ZUBERI MWOMBEJI
TAREHE 10/04/2013.

SIMU ZILIZO NUNULIWA SANA (ULIMWENGUNI) MWEZI MACHI

1. Sony Xperia Z:

Orodha ya simu kumi bora kwa mauzo katika mwezi wa Machi imeongozwa na Sony Xperia Z. Orodha hii huchukua mauzo ya simu kutoka nchi 70 za mabari sita Duniani na kuchapishwa kila mwezi. Ubora na vielelezo utatolewa kwa simu tano za mwanzo tu.

Sony Xperia Z: Imepanda kutoka nafasi ya pili ambayo simu hii ilishikilia katika mwezi wa Februari. Sifa kuu za simu hii ni:

 • Vielelezo vya hali ya juu
 • Haiathiriki na maji (water proof)
 • Nyembamba na kubwa
 • Kamera ya megapiksel 13 nayo ni kivutio
 • Timescape UI
 • Sony Mobile BRAVIA Engine 2

2. Samsung I9500 Galaxy S4Haikuwemo katika orodha ya mwezi ulioita. Sifa zinazofanya simu hii kupata mauzo mazuri ni:

 • Mafanikio ya Samsung Galaxy SII na SIII.

 • Ni simu yenye prosesa yenye core nane (baadhi yake tu)

 • Umbile lenye kuvutia

 • Imevuma sana kufuatia uzinduzi wa aina yake.

 • Koti la TouchWiz na sifa mbali mbali mpya hasa za kamera na hata simu yenyewe kiujumla.


3. Apple iPhone 5

Imeshuka kutoka namba moja mwezi uliopita, iPhone 5 iliongoza orodha hii kwa miezi 6 mfululizo. Hakuna simu iliyofanya hivyo ambayo si iPhone. Sifa zinazovutia mauzo:

 • Ina jina (brand name) kubwa, yaani Apple

 • Inatumia iOS, ni OS ya kipekee ambayo haipatikani kwenye simu yoyote isiyo iPhone.

 • Inaongozakwa ubora na idadi ya apps ambazo zinapatika kwenye AppStore.

 • Inaongoza kwa vifaa (accessories), na hasa vifaa vinavyotumia apps kama vile kipima msukumo wa damu (BP), vifaa vya mazoezi kama Jawbone wristbandna Nike Fuelband, Drone, Mizani na kadhalika.

4. HTC One SV

Imepanda kutoka nafasi ya tisa kwenye orodha ya mwezi Februari. Sifa zinazovutia mauzo katika simu hii ni:

 • Umbile linalovutia

 • Bei nafuu mno

 • Sauti safi na bora ikiwa na Beats By Dre

 • HTC Sense

5. Sony Xperia ZL

Imeingia kwenye orodha hii kwa mara ya kwanza mwezi huu.

 • Simu hii ina sifa zote za Xperia Z inayoshika namba moja, tofauti kubwa ni kwamba hii haihimili maji (not water proof), na ni fupi na pana kulinganisha na Xperia Z, ingawa zote zina skrini zenye ukubwa sawa, hivyo tofauti ipo kwenye fremu.


6. Samsung Galaxy i9300 SIII: imepanda kutoka nafasi ya saba.

7. Sony Xperia E / E Dual: Imeingia kwenye orodha kwa mara ya kwanza.

8. Apple iPhone 4/4S: imeporomoka kutoka nafasi ya 3.

9. Samsung I8190 Galaxy S III Mini: Imeporomoka kutoka nafasi ya nne.

10. Blackberry Z10: Ni ingizo jipya katika simu 10 bora.

iPhone 5, iPhone 4S na Samsung Galaxy SIII ndo simu zilizoporomoka sana mwezi huu, huku Galaxy SIII Mini imeporomoka hadi kutolewa kabisa katika kumi bora hizi. Hata hivyo iPhone 5 imemuda kubaki kwenye nafasi ya tatu nalo si jambo dogo tukizingatia kuwa ni simu yenye miezi sita sokoni kwa sasa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba simu mpya zilizozinduliwa kwenye maonyesho ya WMC Barcelona na maonyesho ya CES, Las Vegas baina ya mwezi Januari na Februari ndio zimeanza kufikia idadi kubwa ya mauzo.

Wakati Sony Xperia Z haishangazi kuongoza kwa vile ina sifa ya kipekee muhimu yaani kutoathiriwa na maji, simu unayoshangaza kwa kukosekana kwake kwenye kumi Bora hii ni HTC One, ambayo sio tu ilitarajiwa iwemo kwenye 10 bora bali ilitarajiwa kuchuana na Xperia Z katika kugombania namba moja. Hata hivyo inawezekana sana uzalishaji hafifu ndio sababu ya msingi ya kukosekana kwa simu hiyo.

Hoja nyingine ya muhimu ni kwamba katika orodha hii ya simu kumi bora kwa mauzo haina hata simu moja inayotumia OS ya Windows Phone 8. Kwa upande wa OS, orodha hii imetawaliwa na simu saba zinatumia Android, hii inadhihirisha jinsi OS hii inavyotawala mauzo ya simu Ulimwenguni.

Kwa mwaka huu simu mbili tu ambazo hazikutoka bado ndizo zinazotarajiwa kuleta mabadiliko ya kimauzo katika orodha hii, simu hizo ni iPhone 6, iwapo itatolewa na Samsung Galaxy Note 3. Kwa utaratibu wa kawaida Apple mwaka huu walitarajiwa kutoa iPhone 5S, baada ya kutoa iPhone 5 mwaka jana, na iPhone 5S katika ratiba ya kawaida hutoka mwezi wa Septemba.

Hata hivyo katika hali ambayo si ya kawaida mwaka jana Apple walitoa iPad tatu tofauti, yaani iPad 3, iPad Mini na iPad With Retina Display. Miaka ya nyuma yote tangu kuzinduliwa kwa iPad ya kwanza Apple hutoa iPad moja kila mwaka. Hivyo huenda mwaka huu Apple wakatoa simu zaidi ya moja, kinyume na kawaida yao. Ikiwa ni hivyo basi moja kati ya simu hizo huenda ikazinduliwa kwenye mkutano wa WWDC 2013 ambao utatangazwa wakati wowote kuanzia mwezi huu.

Makala inayohusiana: Xperia Yaongoza Kwenye Kumi Bora

Chanzo: http://www.gajetek.com/

KIKWETE KUFUNGUA BARABARA YA TANGA – HOROHORO (KM 65.14) JUMAMOSI 13 APRIL 2013

Wizara ya Ujenzi inapenda kutoa taarifa kwa umma kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14.  Aidha, sherehe hizo zitahudhuriwa na Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wa Marekani.

Barabara ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Tanzania na nchi jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga.  Mradi huu umepata msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation – MCC).

Kukamilika kwa barabara hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara.  Aidha, kukamilika kwa barabara hii kutapanua fursa za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya na hivyo kutumia vizuri zaidi fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Sherehe hizi zitafanyikia kijiji cha Kisera katika Wilaya ya Nkinga mkoani Tanga.

Taarifa hii imetolewa na;

Balozi Herbert E. Mrango

KATIBU MKUU