PAMOJA NA KESI ZA KILA MARA ARUSHA MJINI KUPATA HOSPITALI; LEMA

Godbless-Lema-akipokewa-Arusha-dec-22-2012-9

  • HATAKI KUWA MTU WA KUTOA SABABU TUU ZA KUTOTIMIZA AHADI.

  • UOGA NI UJINGA, SIYO BUSARA… UMASKINI WETU  NI WA FIKRA.

  • WANA ARUSHA WASEMA PAMOJA NA PROPAGANDA ZA WATAWALA JUU YA ELIMU YAKE HAKIKA YEYE NDIYO CHAGUO LAO NA NIBORA KULIKO HAO WENYE ELIMU KUBWA.

Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema, Mpambanaji Kamanda Godbless Jonathan Lema Jumatatu 22 April 2013 aliendelea kuzipangua kesi pamoja na vifungo vya ndani na nje, vinanvyo mkabili kwa kuinurisha jumatatu ambapo ilishuudia ombi la kwanza la waleta rufani la kutaka review ya uamuzi uliotolewa na mahakama ya rufaa juu ya kesi yake isikilizwe na jopo la majaji 7 kutupiliwa mbali huku ikiamuru tena wakata rufaa walipe gharama zote za kesi.

Mara baada ya kuakikishiwa ubunge wake Mpambanaji Kamanda Lema huku Sura yake ikiwa imepambwa na bashasha na kuonyesha ukakamavu aliwaambia watanzania kupitia TV ya ITV kuwa “nitaondoka katika kiti cha ubunge wa arusha endapo mimi na mungu tutaamua lakini sio vinginevyo”.

Kauli ambayo ilionyesha kuwakera wengi hasa wale ambao hawajuhii heshima ya kiongozi huyu hasa jimboni mwake Arusha mjini sifa ambayo inatokana na uwezo wake wa kuongea bila kupindisha maneno hasa pale anpoamini kuwa kuna uonevu.

Kupitia channel 10 kipindi kinacho julikana kama Mimi na Tanzania kinachoongazwa na Mtangazaj Hoyce Temu Mpambanaji Kamanda Lema alitabanaisha kwa kusema Tanzania tuna Pamba, Korosho, Kahawa, gas , mafuta, uraniam, Tanzanite, mlima wa pili kwa urefu duniani, mbuga za wanyama kubwa kabisa duniani, hali ya hewa nzuri, nk, hivyo tukisema Tanzania ni maskini ni kumkufuru Mungu.

Aliongeza kwa kusema tatizo ni hatuna viongozi wenye upendo na nchi yao ndiyo maana tuko hivi tulivyo!

Alipoulizwa kuhusu ahadi yake ya kujenga Hospitali jimboni kwake kwamba atawezaje kuitimiza wakati amekaa nje ya ubunge kwa muda mrefu, amesema ni kweli amekuwa katika usumbufu kwa takribani miaka miwili LAKINI LAZIMA NDOTO YAKE HIYO ITIMIE KUFIKIA 2015. Hataki kuwa mtu wa kutoa sababu tuu za kutokimiza ahadi.

“Hata kama elimu yake ni ndogo kama tunavyoaminishwa ila jamaa yupo smart kuliko hata hao wenye elimu kubwa hapa tz…..” alisikika mwananchi mmoja wa Arusha aliyekuwa anafwatili kwa karibu kipindi cha channel 10 kipindi kinacho julikana kama Mimi na Tanzania kinachoongazwa na Mtangazaj Hoyce Temu.

Mpambanaji Kamanda Lema alimalizia kwa kusema kama kupigania haki ni fujo basi waendelee kumwita kinara wa fujo kwani hata nyerere wakati anapigania uhuru wazungu walisema anavunja sheria za nchi.

MY TAKE: – napenda kudi clear my interest namkubari sana huyu bwana mdogo. Am proud of him as my MP…. Ni bora kuliko selukamba.

Advertisements