MKUU WA MKOA WA ARUSHA KUMTOA KAFARA MBUNGE LEMA! AAGIZA AKAMATWE KWA UCHOCHEZI…..

5 3d33a

Gari la Mbunge wa Arusha mjini,Godbless Lema likivutwa kupelekwa kituo cha Polisi baada ya kudaiwa kuchochea fujo za wanafunzi

6 0f854

7 d7068

  • CHUO CHA UHASIBU CHAFUNGWA KWA MUDA NI BAADA YA VURUGU KISA  MWANAFUZI KUCHOMWA KISU NA KUFARIKI.

  • MKUU WA MKOA AWADHIAKI WANAFUNZI, AGOMA KUONGEA NAO BILA KIPAZA SAUTI. APIGWA NA KUJERUHIWA.

  • MBUNGE LEMA AWATULIZA WANAFUNZI KWA ZAIDI YA MASAA MAWILI, MKUU WA MKOA ASEMA YEYE NDIYO MCHOCHEZI AAGIZA AKAMATWE.

Chuo cha Uhasibu cha Arusha, kimefungwa kwa muda usiojulikana kwa sababu za kiusalama kutokana na vurugu zilizo zuka jana na kusababisha mkuu wa mkoa wa Arusha kujeruhiwa ni baada ya kifo cha mwanachuo mmoja anayesadikiwa kuchomwa kisu usiku akitokea chuoni hapo kujisomea, hatua hiyo inawataka wanachuo kuondoka chuoni hapo hadi watakapotangaziwa tena.

Baada ya taarifa za kifo hicho, wanafunzi wa chuo hicho walikusanyika kwa lengo la kuandamana hadi Kituo Kikuu cha Polisi kulalamikia ulinzi duni.

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema alifika na kuwatuliza na kuwasii wasiandamane na kuanza kuzungumza nao, kwa zaidi ya masaa matatu wakati wakimsubiri Mkuu wa Mkoa.

Hata hivyo, baada ya kufika chuoni hapo, mkuu huyo wa mkoa alishindwa kuzungumza na wanachuo hao kutokana na kutokuwa na kipaza sauti, taharifa nyingine zinasema alinukuriwa kisema kuwa wanafunzi hawana adabu na awezi kusongamana nao kwasababu wanaleta jasho, hatua ambayo ilipelekea wanachuo kumzomea na kumrushia mawe na chupa. Pamoja na jitihada za  uongozi wa chuo kubadili eneo kwa lengo la kutuliza hali ya hewa, zomeazomea iliendelea na mkutano kuvunjika baada ya FFU kufika na kurusha mabomu ya machozi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama na uongozi wa chuo hicho, mkuu huyo wa mkoa alisema polisi wanafanya uchunguzi wa suala hilo.

Licha ya kuelezwa kwamba aliuawa kwa kisu, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alisema taarifa nyingine, zinaeleza kuwa aliuawa akitokea katika Ukumbi wa Disko wa Bugaloo jirani na chuo hicho.

“Baada ya kuletewa taarifa za tukio hili na Mbunge Lema, niliondoka na kwenda kuwasikiliza wanachuo lakini tayari nilijua mazingira yalikuwa yamebadilishwa na pale nikagundua Lema ndiyo amekuwa msemaji mkuu badala ya uongozi wa chuo au Serikali ya wanachuo. Ndiyo maana mkaona na zomeazomea ile,” alisema Mulongo.

Alimtuhumu mbunge huyo uchochezi na ameamuru kukamatwa kwake na wanafunzi waliohusika na vurugu zile.

Lema alieleza kusikitishwa na agizo la kutakiwa kukamatwa akisema alizuia maandamano kufika mjini… “Nyie waandishi wa habari mlikuwepo nimezungumza zaidi ya saa mbili na wale wanafunzi kuwasihi watulie wasiandamane na mimi ndiye nilimpigia simu Mkuu wa Mkoa aje kuwasikiliza wanafunzi iweje niwachochee kufanya fujo? Ninawasubiri waje wanikamate.”

Advertisements

2 thoughts on “MKUU WA MKOA WA ARUSHA KUMTOA KAFARA MBUNGE LEMA! AAGIZA AKAMATWE KWA UCHOCHEZI…..

  1. huo si utawala bora ni kutumia mabavu tu hiyo ni sababu ya serikali legelege ndiyo imefikia mwisho wao sasa.mungu uwasaidie hao wanyonge amina

  2. duh kweli serikali imepanick, “nmeamuru akamatwe kukamatwa kwake na wanafunzi waliofanya vurugu”, aliyezuia maandamano ndo amechochea fujo, je lema angewaacha wakafanyie hiyo fujo mjini, ndo shida ya akili ndogo kutawala akili kubwa

Comments are closed.