LEMA KUSOTA KOROKORONI MPAKA JUMATATU; MAKOSA YALIYOMNYIMA DHAMANA NDIYO HAYA

godbless lema

Kamanda Mpambanaji G. Lema Mbunge wa Arusha Mjini kulia akiwa na vyombo vya sheria

Hakika sikutaka kukurupuka kuposti kitu chochote leo kuhusu kadhia hii… kwanza sikuamini kama Jeshi letu pamoja na Mkuu wangu wa mkoa wa Arusha alikuwa na kesi ya kumfikisha Mbunge Kipenzi cha wanaArusha maakamani.

Lakini kubwa zaidi nilijuwa busara za Mkuu wetu huyo ambaye ni mtoto wa aliyekuwa msaidizi wa Katibu mkuu wizara ya utumishi (mama yake) japo angalikuwa na busara kama mama yake, nakili wazi uwezo wake niliubeba zaidi ya uwasilia wake ulivyo.

Naomba niwasilishe kwanza mashtaka ya Kamanda mpambanaji G. Lema nikirudi nitajadili na kuwaletea maojiano ya mkuu wetu wa mkoa alivyo zungumza na Redio 5 leo pamoja na Video ambazo polisi walilazimika kufanya upekuzi wa  masaa kadha kuzitafuta nyumbani kwa Lema.

Kwa mujbu wa wakili wa mbuge wa Arusha Mwanasheria Humphrey Mtui makosa aliyoshitakiwa nayo Lema ni haya:-

 1. Kosa la kwanza ni kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa (Worth fighting for). {HAPO KOSA NI UCHOCHEZI}

 2. Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa ‘’Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye send-off. Hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawajali matatizo ya wananchi’’ {HAPO KOSA NI UCHOCHEZI}

 3. Kosa la Tatu ni pale alipotamka kuwaambia wanafunzi kuwa ‘’Mimi Mbunge wenu nipo sambamba nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa mkoa hatakuja hapa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake ili mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika utekelezaji wa utawala bora wa kidemokrasia ambao msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’  {HAPO KOSA NI UCHOCHEZI}

Hayo ndiyo makosa mabayo yamemyima Kijana wetu Kamnda Godbless Lema dhamana.  hayo ndiyo makosa yaliyosababisha polisi watumie fedha za walipa kodi kumvamia usiku kurusha fataki badala ya kutumia busara ya kumuita tu kituoni na kusababisha taharuki maeneo hayo na ndani ya nyumba yenye ndugu jamaa na hata mtoto mwenye miezi mitano huku polisi wakitumia nguvu na kukiuka sheria

Huo umeitwa uchochezi baada ya mkuu wa mkoa kumtumia ujumbe wa mkononi kupitia simu yake kupitia namba 0752960276 aliyotishia kumbambikizia kesi anayoitaka yeye.

WHAT NEXT…..

Advertisements

8 thoughts on “LEMA KUSOTA KOROKORONI MPAKA JUMATATU; MAKOSA YALIYOMNYIMA DHAMANA NDIYO HAYA

 1. Enyi wenye mioyo migumu! kwamara nyingine tena tumeonyeshwa viongozi wa kitanzania wa kurithishana! Mkuu kweli, Mulongo ni chaguo la Mungu.

 2. Wasomi kama ndiyo wamekuwa wajinga kiasi hiki basi ndomaana watoto wanafeli mashuleni kwani wanafkiri wanazo akili kuliko hao wenye degree, diploma and phd.

 3. Chuki na unafiki unaoendekezwa na tofauti zetu za kiitikadi kulingana na vyama vyetu. Utu na maadili ya kiuongozi yako wapi? Tatizo limeachwa sasa siasa imeanza kazi. Ndivyo tulivyo watanzania!

  Mungu ailaze mahala pema ndugu yetu mwanachuo wa chuo cha uhasibu Arusha. Haki ya kuishi si kitu cha kufanyia mchezo.

  Lema sasa ndicho chanzo cha mauwaji ya huyo mwanachuo?

  Acheni masiara, mauti ni yetu sote.

 4. mimi binafs nashindwa kuelewa kuwa hawa watawala wetu wana upeo kiasi gani? La pili hata wanaotumwa kufanya hayo wanayofanya wanashindwa kutumia hakili za kuzaliwa?!! …..

 5. We! hay we… eliyangu sijasema kwamaana sikuhizi hata ukiona tukio ukisema au kuwaita wausika kesi inakugeukia…. NAPITA TARATIBU HATA KUSOMA SIJASOMA

 6. NATUMAI WEWE ULIEANDIKA MAKALA HII UJAONA KOSA. NA HUFAHAM MADHARA YA KITENDO ALICHOFANYA UNAEMUITA KAMANDA. TAIFA HILI LINGAWALEA MUNAOWAITA VIONGOZI KAMA UNAVYOTAKA, LISINGEKUA LAITWA TAIFA PEKEE LA AMAN AFRICA. ACHENI USHABIKI NA UTAIFA MBELE. KAMA NA MAPENZI YA WANACHAMA KWA KIONGOZI WA CHAMA HAYAJI KWA KUPANDISHA JAZBA. ANGALIFUATA TARATIBU KAMA KINGOZI NATUMAI KUSINGETOKEA HAYO. KUPAYUKA NA KUONEKANA UNASHNGILIWA NA VIJANA SI KUA UMEKUBALIKA BALI WENYE BUSARA WATAJUA /NA WATAKUONA HUFAI KTK JAMII. TANZANIA SI YA KIKWETE PEKEE. YEYE YUPO KAMA KIONGOZI TU. LKN WAPO WENYE KUFUATA MISINGI YA UTAIFA NA KUHAKIKISHA TUNASONGA MBELE KWA AMAN NA BUSARA. UCHEZEENI AMAN MUTAIJUTIA NA KUITAFUTA KUSIKI JULIKANA. *! AMAANII LAZIMA IZINGATIWE..IZINGATIWE NA WATU WOTE.!” NAMKUMBUKA JUSTIN KALIKAWE.

 7. Ntalaluka Rashid (agandi wo muka?) ukiliangalia swala hili kwa kauri hizo tu unaweza kufikili au kuona ni kosa. ila kama ulikuwa unafwatilia sakata hili toka mwanzo na ukajionea mwenyewe video ambazo zinaonyesha mambo yalivyokuwa unaweza kuelewa na kwanini nasema hakuna kosa. Ntalaluka unaweza kunielewa zaidi kama ukifuta mfano huu. Vitabu vyetu vyote vya dini ukisoma mstali mmoja mmoja uwezi kuelewa maana yake mpaka upate kisa chote.

  kwafaida ya wote nilisema nitaweka video ila kwa bahati mbaya sikufanya hivyo ila naomba nikupe link hili uweze kuziona kwa muda wako.

Comments are closed.