HOJA ZA MSIGWA ZAKOSA MAJIBU, ZAENDELEA KUWANYIMA USINGIZI WATAWALA.

MCHUNGAJI PETER MSIGWA

  • ASHANGAZWA NA NCHIMBI KUENDELA KUTETEA UJANGILI KWA NGONJELA BADALA YA KUOMBA USHAIDI.
  • ABAINISHA UDHAIFU WA TAASISI YA URAIS KWA SWALA LA LOLIONDO KUSABABISHWA NA MTEULE WA RAIS NA KUCHUNGUZWA VILEVILE NA WATEULE WA RAIS.
  • NIYAMKINI KUWA CCM AWAWEZI KUTATUTA MGONGOLO HUU KWA VILE WENYEWE NDIYO SABABU YA MGOGORO.
  • NYARANDU AKITOA MAJIBU YA UJUMLA ASEMA SERIKALI IKO KWENYE MCHAKATO WA KUPAMBANA NA MAJANGILI

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), ambaye pia ni waziri kivuri wa maliasilia na utali Mchungaji Peter Msigwa katika  katika kikao cha Bunge  asubuhi ya Mei 2 2013, alijangia hoja ya wizara ya maliasili kwa uchungu ususan  jinsi rasilimali za nchi hii zinavyoteketezwa kwa manufaa ya watu wachache. Ameshangazwa sana na Kitendo cha waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Nchimbi kwa kuendelea kutetea ujangili kwa ngonjera baadala ya kumtaka  alete ushahidi ili yeye kama waziri aliyepewa zamana kuchukua hatua stahiki kwa watuumiwa.

Kuhusu Mgogoro wa Loliondo anasema inashangaza Waziri anateuliwa na Rais, Katibu Mkuu wa CCM anateuliwa na Rais iweje jambo ambalo limetolewa uhamuzi na waziri likachunguzwe na hao wateule wengine wao Rais? Hili linaonyesha udhaifu katika taasisi ya Raisi. Hivyo wananchi wa Loliondo wanapaswa kuamka na kujua kuwa viongozi na serikali ya CCM haina nia ya dhati ya kuwasaidia.

Uwezo wa CCM kutataua mgogoro huu ni mdogo sana coz wao ndiyo waliutengeneza to enzi za mwinyi.Baada ya yeye kusoma hotuba yake amekuwa akipokea simu(Private Number) zikimtisha kwa kushikia bango issue ya Tembo.

CCM watambue kuwa maliasili niza watanzania wote na si mali ya watu wachache, hakuna watu au kikundi cha watu chenye mamlaka ya kupora au kujimilikisha raslimali hizo halafu watanzania wenye nia njema waendelee kukaa kimya. Hapa amemshangaa Nchimbi na kusema ndio maana hashangai alipata PHD kabla hata ya kuhitimu.

Amesema mgogoro wa Loliondo umesababishwa na serikali ya CCM. Akaitaja ikulu, na kusema Mwiny ndio aliuzalisha mgogoro huo na ukarithiwa na awamu zote. Hapa akarejea ile principal “Problems cannot be solved by the same level of thinking that created them” CCM ndio chanzo cha mgogoro hamuwezi kuundoa.

Kwa majozi aliweka wazi kuwa tangu aisome bajeti ya upande wa upinzania amekuwa akipokea ujumbe wa vitisho kwa simu zenye private numbers! Anasema ataogopa kusimamia na kuisema kweli.

Kwa upande wao  serikali kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Samuel Nyalandu akitumia Mwndelezo ule ule wa lugha za Kiserikali kuwa tupo kwenye Mchakato (Process) na Kutaka kusifiwa hata kwa kazi ambazo ni wajibu wao. Ametoa majibu ya jumla kuwa serikali imejizatiti kukabiliana na ujangili(Story) na wamepanga kuajiri vijana wengi tu kutoka Pasiansi (mwanza kwenye chuo chao) na JKT ili waweze kukabiliana na Ujangili….

Tofauti na Vikao vingine vya bunge leo hii kuanzia wachangiaji mpaka mawaziri wamekuwa wapole sana na hii ni hishara kuwa siku ya leo upande wa serikali na chama tawala walikuwa wamezidiwa japo kama kawaida vijembe vya hapa na pale avikukosa.

Advertisements