LEMA MBELE YA WAPIGA KULA WAKE ASEMA YALIYOJIRI CHUO CHA UHASIBU, CHADEMA YATAJA KIKOSI CHAKE CHA MAANGAMIZI KATA NNE ZA UDIWANI ARUSHA.

Maelfu kwa mamia ya wanachama wa CHADEMA pamoja na wananchi wa jiji hilo leo wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya Ngarenaro Primary & Secondary school jijini Arusha bila kujari mawingu na manyunyu yaliyokuwa yakidondoka wakati wote kwenye mkutano wa hadhara ulio hitishwa na chama cha   hicho ulio kuwa na lengo la kuwaeleza wananchi kilicho mpata Mbunge wao katika chuo cha Uhasibu mwishoni mwa wiki hiliyopita.

Katika mkutano huo ulifanyika leo uliudhuriwa na Polisi wengi pamoja na usalama wa taifa, lile lililokuwa siyo la kawaida ni polisi hao kuonekana wakiwa na vifaa vya kunasia sauti pamoja na camera za video kwenye mkutano huo.

Kikosi cha wanachama wa CHADEMA waliotangaza nia ya kugombea udiwani katika viti vinne kati ya vitano vilivyo wazi katika kata ya kimandolu watakao shikana mashati ni pamoja na Magoma A. Magoma aliyekuwa Mwenyekiti Vijana Mkoa na Mch. Rayson, huku katika kata ya Elerai watakao gombania nafasi kupitia chama hicho ni pamoja na  C. Mkapa  na Damuni Malemari, Emanuel Kessy na Jamal Milanzi watakuwa kata ya Kaloleni huku  Mwl. Alphonce  kata ya Themi, na Rogers mchezaji wa zamani wa Ndovu kata ya Unga Ltd.

KAULI NA NUKUU MBALI MBALI ZA VIONGOZI WA CHADEMA WALIZO SEMA KWENYE MKUTANO WA LEO.

James Millya:

• Niliondoka ccm sababu ya uhuni wa ccm.
• Mulongo alikua ni mjumbe mwenzangu mpuuzeni na msameheni amezawadiwa madaraka na yeye anawatumikia waliomzawadia.
• CCM ni wahuni watu wa arusha tusiumie sana, tuwe na umoja 2015 tunawamaliza.

Kamanda Kalisti:

• Tunamwambia Lema atakutana na wahuni wengi wa aina ya Mulongo, lakini mwisho wao umefika.
• Madiwani wa ccm wamekuwa wezi wakiongozwa na meya feki. Tunaomba wananchi watuunge mkono kwenye uchaguzi wa kata nne ili tuwaondoe hawa mchwa kwa idadi ya kura

Mwenyekiti wa Wilaya Efatha Nanyaro:

• Kwa kuwa TAMISEMI bado inamtambua Alphonce Mawazo kama diwani wa Sombetini, tutamuita aje aingie kwenye vikao vya halmashauri kama diwani wa CHADEMA!
• Tunaenda kuanza kampeni za uchaguzi ambao utakuwa ni uchaguzi wa ubadhirifu na uadilifu.
• Mkuu wa wilaya na mkoa wanaingilia shughuli za manispaa, nikamwendea mkuu wa wilaya nikamwambia kama anataka kazi za manispaa aende akagombee udiwani. Wamezuia uchaguzi wa sombetini kihuni. Leo tumeandika barua tamisemi, tumewaambia wasipotangaza uchaguzi wa sombetini tutamwita alfonce mawazo aendelee kuwa diwani wa kata ya sombetni. Mkuu wa wilaya anadiriki kuingilia ukataji ushuru wa soko la kilombero, anawateua akina Jumanne Mjusi mwizi anayejulikana hapa mjini ndiyo wanakusanya ushuru watu wahuni.

MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA:

• Nilitumia lugha na hekima ya hali ya juu kuwatuliza wanafunzi pale CHUO CHA UHASIBU, nikamuita mkuu wa mkoa kama mwenyekiti wa kamati ya usalama ya mkoa, akaja kwa madaha kama anaingia kwenye shindano la U-MISS, akazomewa na wanachuo akachukia
• Mulongo anadiriki kuniuliza unanijua mi nina? Nikamjibu nakujua we ni mkui wa mkoa na mimi ni mbunge, mimi nimechaguliwa na msururu wa watu wamepiga foleni kunichagua wewe umekuja kama kiota.
• Field Force na wamama wawili wa USALAMA WA TAIFA waliniokoa wakati mabomu yanapigwa chuoni.
• Polisi walikuja kwangu na mabomu na risasi kama mhalifu nikaficha ushahidi wangu wote kwenye Jamii Forums, Facebook, YouTube na Aljazeera. Kazi ikabaki kwy simu yenye ushahidi mke wangu akanipa maarifa pa kuificha kwa kumvisha mtoto pampers!!!
• Mulongo wakati nilipovuliwa ubunge alinipigia simu kuwapongeza majaji. Baada ya kushinda rufaa nikampigia simu kumwuliza vp amesahau namba yangu mbona haumipi pongezi?
• Mimi ni diplomat, Mulongo si diplomat, anwakilisha kikwete.
• Toka mmenichagua kuwa mbunge siyo mchovu tena. Makamanda hapa wamesema kesho kutwa tuna uchaguzi wa tkata nne. Mi nasema ni kata tano, na ushahidi wangu naupeleka bungeni. Uchaguzi wa sombetini ni lazima siyo ombi. Wakikataa uchaguzi wa sombetini tunakataa uchaguzi wa kata zingine, tunaweka court injuction mpaka watangaze uchaguzi wa kata ya sombetini
• Nilisikia askari wanatafuta simu yangu, mke wangu akanambia namwongezea mtoto pampas, halafu simu tunaificha kwenye pampas. Halafu wakiingia ndani nitamfinya mtoto akianza kulia naanza kumbembeleza wasijue la kufanya. Nikwambia mke wangu una akili sana.
• Unapoongea na wanachuo inaitaji saikoloji na sio mbwembwe.
• Kama kiongozi ukifika mahali watu wana jazba inahitaji ujishushe kama kiongozi na mimi nilijishusha nikawatuliza wanachuo.

Click image for larger version.

Name:	DSC05022.JPG

Views:	0

Size:	164.7 KB

ID:	92265

Click image for larger version.

Name:	DSC05023.JPG

Views:	0

Size:	165.3 KB

ID:	92266
Click image for larger version.

Name:	DSC05025.JPG

Views:	0

Size:	164.6 KB

ID:	92267

Advertisements