KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU MLIPUKO ULIOTOKEA KATIKA KANISA KATOLIKI LA MT. JOSEPH MFANYAKAZI, PAROKIA TEULE YA OLASITI, ARUSHA MJINI, MEI 5, 2013

HAPA NDIPO WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HUKUTANA

HAPA NDIPO WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HUKUTANA

Mheshimiwa Spika,
kwa mujibu wa Kanuni ya 49 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013, naomba kuwasilisha Taarifa yaawali kuhusu tukio la mlipuko uliotokea katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Jijini Arusha tarehe 5 Mei, 2013 saa4:30 asubuhi.

Mheshimiwa Spika,
mnamo tarehe 5 Mei, 2013 saa 4:30 asubuhi kulitokea mlipuko katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha. Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada ya kuanza kwa ibada ya uzinduzi wa Parokia. Mgeni Rasmi katika uzinduzi alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini na Mjumbe wa Baba Mtakatifu, Askofu Fransisco Mantecillo Padilla. Aidha, alikuwapo mwenyeji wake Askofu Josephati Lebulu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha. Katika uzinduzi huo inakadiriwa kuwa kulikuwa na zaidi ya watu 2000. Wakati Mgeni Rasmi akiwa ametoka nje ya Kanisa akijiandaa kukata utepe kama ishara ya uzinduzi mtu alirusha kitu chenye ukubwa wa ngumi kuelekea eneo kulipokuwa na mkusanyiko wa watu ambapo baada ya kutua kulitokea kishindo na mlipuko mkubwa. Mlipuko huo ulisababisha taharuki miongoni mwa waumini na kusababisha watu kukimbia ovyo.

Mheshimiwa Spika,
katika tukio hilo watu wawili wamefariki dunia ambapo REGINA LONGINO KURUSEI, Mwarusha, umri wa miaka 45, mkazi wa Olasiti alifariki dunia siku ya tukio wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mount Meru na majeruhi mwingine JAMES GABRIEL umri wamiaka 16 amefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 6 Mei, 2013. Aidha, watu 59 wamejeruhiwa na watatu kati yao ni mahututi. Majeruhi 38 walikimbizwa hospitali ya Mount Meru kupatiwa matibabu. Majeruhi 16 walikimbizwa hospitali ya St. Elizabeth kwa Father Babu, majeruhi mmoja alipelekwa hospitali ya Selian na majeruhi mwingine alipelekwa katika hospitali ya Dkt. Wanjara, Mianzini. Natumia fursa hii kutoa pole kwa wafiwa, uongozi wa kanisa Katoliki, wakazi wa Arusha na Watanzania wote kwa tukio hili la kinyama. Aidha, nawaombea majeruhi wote wa tukio hilo wapone haraka.

Mheshimiwa Spika,
Viongozi wa dini na Serikali waliohudhuria ibada hiyo hawakupata madhara yeyote kufuatia mlipuko huo. Baada ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupokea taarifa ya tukio hilo waliimarisha ulinzi kwa kuongeza idadi ya askari katika eneo hilo. Aidha, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Magesa Mulongo walifika eneo la tukio na kufanya tathimini ya hali ilivyo na kuelekeza hatua za kuchukuliwa.

Mheshimiwa Spika,
kutokana na uzito wa tukio hilo, kitaifa na kimataifa, Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Pereira A. Silima, na Inspekta Jenerali wa Polisi, Said A. Mwema walikwenda Arusha na walitembelea eneo la tukio, waliwatembelea majeruhi na kuelekeza hatua za ziada za kuchukuliwa.

Mheshimiwa Spika,
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mlipuko huo ni bomu. Uchunguzi wa kubaini aina ya bomu lililotumika unaendelea kufanywa na Jeshi la Polisi na Wataalamu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Hadi sasa watuhumiwa sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi. Miongoni mwao ni Victor Calisti Ambrose mwenye umri wa miaka 20, dereva wa bodaboda, mkazi wa KwaMrombo, Arusha ambaye anatuhumiwa kwa kurusha bomu hilo. Watuhumiwa wengine watano waliokamatwa ni raia wanne wa kigeni na Mtanzania mmoja ambao wanashikiliwa kwa mahojiano.

Mheshimiwa Spika,
siku za karibuni kumekuwepo jitihada kubwa sana za watu wachache wasiyoitakia mema nchi yetu kutaka kupandikiza chuki za kidini miongoni mwa watanzania na kuleta mapigano na mauaji miongoni mwa watanzania, sina shaka kuwa shambulio la Arusha ni sehemu ya mikakati hiyo miovu. Nataka niwahakikishie Watanzania kuwa Serikali haitavumilia hata kidogo mbegu za chuki za kidini miongoni mwawatanzania na tutachukua hatua kali bila huruma kuzigandamiza njama hizi mbaya dhidi ya taifa letu. Tutachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujalihadhi na nafasi yake katika jamii. Amani yetu kwanza na taifa letu kwanza.

Mheshimiwa Spika,
Pamoja na kukamatwa kwa watuhumiwa hao, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wametoa maelekezo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo tayari Inspekta Jenerali wa Polisi kwa kushirikiana na Wakuu wa Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama wameunda Kikosi Kazi maalumu ili kuchunguza tukio hilo.

Mheshimiwa Spika,
kokote duniani, tukio la kushtukiza, linalosikitisha nakuhuzunisha kama hili linapotokea, wananchi wote huungana na kuwa wamoja kama taifa na kulaani wahusika na kuwafariji waathirika wa tukio hilo. Nchini Marekani, Mgombea mmoja wa Urais wakati wa uchaguzi mkuuwa Mwaka 2012 aliishutumu Serikali kutokana na tukio la kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani nchini Libya. Ni wazi kuwa mgombea huyu alichukua tatizo lile kama ajenda ya kisiasa. Hata hivyo, alishutumiwa vikali na Wamarekani wenzake kwa kuelezwa kuwa ni mtu mwenye kukosa kabisa misingi ya uaminifu na uzalendo kwa taifa lake (Fundamental dishonest).

Serikali inasikitishwa sana wanasiasa wa aina hii ambao wanajitokeza nchini na kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa gharama za maisha ya Watanzania. Wanasiasa na viongozi wote wajiepushe na kauli zinazochochea ubaguzi wa kidini, mifarakano ya kijamii na chuki miongoni mwa Watanzania. Serikali isilaumiwe kwa hatua kali za kisheri aitakazochukua dhidi ya viongozi wa aina hii ambao maslahi yao ni muhimu kuliko maisha ya Watanzania, maslahi yao ni muhimu kuliko utulivu waWatanzania na maslahi yao ni muhimu kuliko umoja wa Watanzania.

Mheshimiwa Spika,
kwa niaba ya Serikali naungana na Watanzania wenzangu kulaani wahusika wote wa tukio hilo walioshiriki kwa njia yoyote.

Aidha, Serikali kwa nguvu zake zote itahakikisha kuwa watuhumiwa wote waliohusika na kushiriki kwa namna yoyote katika tukio hili wanasakwa popote walipo na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Tunawataka viongozi wa kisiasa, kidini na wananchi wote kwa ujumla kila mmoja kwanafasi yake kuwajibika ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwakisiwa cha amani na utulivu.

Mheshimiwa Spika,
mwisho nawasihi Watanzania wawe watulivu wakati vyombo vya dola vikiwasaka waliohusika na shambulio hilo, kila mwenye taarifa za kuwezesha kukamatwa wahalifu hao atoe taarifa hizo kwa Jeshi la Polisi. Aidha, ninawaomba Watanzania tuendelee kukataa vitendo vyauvunjifu wa amani katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

Advertisements

VIDEO:- TUSIPOTOSHE AU KUPOTOSHWA… HAYA NDIYO LEMA ALIYO SEMA BAADA YA SHAMBULIO LA BOMU KANISANI ARUSHA

  • NASHANGA KWANINI VYOMBO VYA HABARI AWAKUONYESHA VIDEO HII.
  • BAADA YA HAPO ALIWAONDOA WANANCHI SEHEMU YA TUKIO KWA AMANI KAMA VYOMBO VILIVYO SHAULI.
  • ALIWAAMASISHA WATU WA ARUSHA WAENDE KUCHANGIA DAMU.
  • WATANZANIA WA SASA WANAJUWA NANI ANAYE WAGOMBANISHA NA KUWACHONGANISHA.
  • UKWELI WAKE NDIYO SABABU YA KUPENDWA ARUSHA.
  • ANGALIA ALAFU TOA USHAURI WAKO JINSI UONAVYO…..

UNYAMA MKUBWA ULIOFANYIKA ARUSHA, SIYO DINI WALA SIASA, HAYA NI MAUAJI YA KUANGAMIZA WATOTO NA KINAMAMA

  • SIKUBALI KAMA KWELI TANZANIA TUNAVITA VYA KIDINI, WALIO FANYA HIVYO NI WAUNI WACHACHE AMBAO LAZIMA WACHUKULIWE HATUA STAHIKI.
  • UGAIDI NI UDHAIFU (cowards) UWEZI KWENDA KUWASHAMBULIA WANAWAKE NA WATOTO ILI UTEKELEZEWE MATAKWA YAKO…… KWANINI USIMFUATE MUHUSIKA?
  • ARUSHA TUKO IMALA NA HATUOGOPI KUSEMA UKWELI HATA KAMA UTAWAUDHI BAADHI YA WATU, HASA WAKATI HUU WA MACHUNGU.

Kila kinachotokea kina chanzo chake. Tumeona kilichotokea sasa swali ni nini chanzo chake. Hakuna ubaya hata kidogo kwa watu kushuku lolote au yeyote kwani ndivyo akili ya mwanadamu ilivyoumbwa. Hata hivyo kushuku siyo ushahidi. Wapo wanaoshuku M23, wapo wanaoushuku mambo ya kisiasa na wapo wanaoushuku masuala ya kidini. Wote hawa wana sababu zao za kufanya hivyo.

NI kwa sababu hiyo umakini, weledi na uharaka wa vyombo vya uchunguzi kutafuta chanzo unahitajika. Ni katika kuuweka wazi ukweli – haijalishi ni upi – ndivyo watu wanavyoweza kuelewa chanzo cha tukio hili na hata kuwapa mwanga wa namna ya kujilinda huko mbeleni.

Nalaani vikali tukio hili kwani ni la kiwoga na lenye lengo la kupandikiza hofu miongoni mwa jamii. Hakuna sababu yoyote inayoweza kutolewa kulipa uhalali.

SERIKALI IMEVIGIZA VYOMBO VYAKE VYOTE VYA USALAMA KUSHUGULIKIA SWAHALA HILI PICHANI WANAONEKANA WANA USALAMA PAMOJA NA WANAJESHI WAKIWA ENEO LA TUKIO MARA BAADA YA SHAMBULIO HILO LA KUSTUKIZA.

SEHEMU YA UMATI WA WANANCHI WAKIWA AWAJUHI LA KUFANYA WENGINE WAKIWA BADO WAMEPIGWA NA BUMBUWAZI KAMA KWELI HAYA YAMETOKEA NDANI YA NCHI YAO.OLYMPUS DIGITAL CAMERA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

BAHADA YA VYOMBO VYA USALAMA KUWASAHAULI WANANCHI WAONDOKE MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA PAMOJA NA MWENZAKE NASSARI WALIONDOKA KWA MIGUU HUKU WAKIWAIMIZA WATU WAENDE KUCHANGIA DAMU HOSPITALI YA MT. MERU KWAHAJILI YA MAJERUHI WALIO SHAMBULIWA. 

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

BAHADA YA VYOMBO VYA USALAMA KUWASAHAULI WANANCHI WAONDOKE MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA PAMOJA NA MWENZAKE NASSARI WALIONDOKA KWA MIGUU HUKU WAKIWAIMIZA WATU WAENDE KUCHANGIA DAMU HOSPITALI YA MT. MERU KWAHAJILI YA MAJERUHI WALIO SHAMBULIWA. 

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

OLYMPUS DIGITAL CAMERA


Hali ya eneo mlipuko ulipotokea

Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea

Ulinzi umeimarishwa

Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi.

Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio

Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh gaundence Lyimo akielekea eneo la tukio kwa miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia.

Magesa Mulongo akiteta na RCO wa Mkoa wa Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na wananchi kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa. Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.

Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia. Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi.

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

KIKWETE ATOA SALAM ZA POLE KWA WATU WA ARUSHA

251px-Coat_of_arms_of_Tanzania.svg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya tukio la leo, Jumapili, Mei 5, 2013 la mlipuko kwenye Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti Jijini Arusha.  Tukio hilo la kigaidi limesababisha mtu mmoja kupoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa.  Rais Kikwete analaani vikali shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na watu wake.

Rais Kikwete ameagiza vyombo vya usalama nchini kumsaka mtu au watu waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.Vile vile Rais Kikwete amewataka wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikalina vyombo vyake inaendelea kufuatilia tukio hili.  Tutawasaka popote walipo na kupambana nao bila huruma.  Aidha, tutakabiliana na aina yoyote ya uhalifu nchini iwe ni ugaidi au aina yoyote ya uhalifu wa namna hiyo au wa namna nyingine, uwe na chimbuko lake ndani ya nchi ama nje ya nchi yetu. Kamwe hatutakubali kuwaacha wavuruge amani na usalama wa Tanzania na watu wake. Rais anaamini kuwa Serikali, kwa msaada na ushirikiano wa wananchi, watu hao watapatikana na kuadabishwa ipasavyo.

Aidha, Rais Kikwete anatoa rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wafiwa na wale wote ambao wamejeruhiwa katika tukio hilo. Anaungana nao katika machungu na msiba. Rais pia anawaombea wote walioumia katika tukio hili wapate nafuu ya haraka na waendelee na shughuli zao za ujenzi wa taifa.

Rais Kikwete vilevile anatoa pole nyingi kwa viongozi na waumini wa Kanisa Katoliki kwa tukio hili la kusikitisha na kuvurugika kwa ibada na shughuliyao muhimu ya uzinduzi wa Kanisa lao.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

IKULU,

DAR ES SALAAM

 5 Mei, 2013