VIDEO:- TUSIPOTOSHE AU KUPOTOSHWA… HAYA NDIYO LEMA ALIYO SEMA BAADA YA SHAMBULIO LA BOMU KANISANI ARUSHA

 • NASHANGA KWANINI VYOMBO VYA HABARI AWAKUONYESHA VIDEO HII.
 • BAADA YA HAPO ALIWAONDOA WANANCHI SEHEMU YA TUKIO KWA AMANI KAMA VYOMBO VILIVYO SHAULI.
 • ALIWAAMASISHA WATU WA ARUSHA WAENDE KUCHANGIA DAMU.
 • WATANZANIA WA SASA WANAJUWA NANI ANAYE WAGOMBANISHA NA KUWACHONGANISHA.
 • UKWELI WAKE NDIYO SABABU YA KUPENDWA ARUSHA.
 • ANGALIA ALAFU TOA USHAURI WAKO JINSI UONAVYO…..
Advertisements

12 thoughts on “VIDEO:- TUSIPOTOSHE AU KUPOTOSHWA… HAYA NDIYO LEMA ALIYO SEMA BAADA YA SHAMBULIO LA BOMU KANISANI ARUSHA

 1. Wametugawa ili watutawale, nitashangaa kama wakishangaa haya yanayotokea sasa, au labda hawakujua athari zake ni nini mbele ya safari? sitaki kuamini hivyo, kidogo kidogo mpaka Nchi haitatawalika………..MUNGU TUEPUSHE NA JANGA HILI.

 2. Sijui kama ninakosea ila ninafikiri siasa za bongo ni upuuzi mtupu na usipokuwa na uwezo wa kutafakari mwenyewe ni hayari sana kwa kuharibika fikra na mutazamo yako,,,,ninafikiri Lema yupo sawa! La msingi ni waakina nchemba,nape,lusinde wakanushe kwa kuongea ukweli sio kushindana!

 3. Nilikuwa mmoja kati ya watu waliokerwa na maelezo kuhusu Lema lakini kama kweli haya ndo aliyoongea sioni ubaya ulipo,badala yake nadhani amesimamia ukweli, ccm wanaiharibu nchi yetu

 4. Lema anajua nani kalipua bomu hapo Arusha, akamatwe aunganishwe kwenye hiyo kesi.
  Hawa ni Magaidi wasionewe huruma.

 5. Maneno ya Lema kwa yenyewe siyo mabaya. Wasiwasi wangu ni kuwa tusije kuhusisha kila jambo na siasa. tena niseme hivi: isije ikawa kikundi fulani kinachoamini kuwa CCM ni muasisi wa udini, na kikafanikiwa kuwaaminisha watu wengi hivyo, sasa kinasababisha haya kwa kujua kuwa CCM na serikali yake ndo wadini na hata hili la olasiti wamelisababisha wao. God forbid!

  Tufike mahali wanasiasa tusiwe wepesi wa kufanya conclusion kwa maslahi ya kisiasa. Tuwaache polisi wafanye kazi yao japo nao ni wachakachuaji na wepesi wa kutumikia CCM (utadhani wanalipwa na CCM) na serikali yake dhaifu badala ya wananchi.

  Wapendwa; myaonapo haya yanatokea kwa frequency ya juu zaidi kila uchao tambueni kuwa ule mwisho u karibu; na ukombozi u karibu zaidi kuliko jana!

  Pole nyingi kwa wafiwa na majeruhi!

 6. watupo salama hata kidogo,,,ni majibu rahisi tu yatatungwa na kuaminishwa wahanga,kua ni alshaababu,alqaida,au M23 au chama Fulani,lakini huu ni mwendelezo wa yaliyowahi kutokea,yanayotokea wakati huu,makanisa yamechomwa na wa humuhumu,watu na viongozi wa dini wameuawa na wahumuhumu,vitisho na cd/dvd zimetengenezwa na zinauzwa na watu wa humuhumu,hivyo haya nayo ni ya humu humu,na haya yamechangiwa na siasa na hasa yamelelewa na kukua na viongozi wa humu humu,tuendelee upande wa waathirika uendelee kusali na kuvumilia,lakini siku wakichoka…

 7. Lema ajichunguze xana na kauli zake,anaposema tukio hilo sio la kijambazi bali ni la kiimani anamaanisha nn ikiwa tanzania inajumuisha dini kuu mbili (Muslims&Christian) kwa maana amewalenga dini fulani ndio waliofanya hivyo?

 8. katika dunia hii kweli kunawat hawa hata akili hivi ccm imehusika vipi katka mripuko

Comments are closed.