AFRIKA KUSINI HAIJAWA MTELEMKO KWA BARACK OBAMA

Baadhi ya wachambuzi kisiasa nchini Afrika Kusini na wamemtuhumu Barack Obama kuto toa mchango wa kutosha kwa ajili ya bara la Afrika, ingawa baba yake ni mkenya.

Baadhi ya wachambuzi wa kisiasa nchini Afrika Kusini wamemtuhumu Barack Obama kwa kuto toa mchango wa kutosha kwa ajili ya bara la Afrika, ingawa baba yake ni mkenya.

Ziara ya rais mweusi wa kwanza wa Marekani kwenye mji mdogo wa Soweto Afrika Kusini, mji ambao ulikuwa chachu ya mapambano dhidi ya utawala wa wazungu wachache, imepokewa kwa hisia tofauti huku ikitarajiwa kuwa swala na tukio la kihistoria lenye kuvutia umati mkubwa wa watu.

Badala yake Barack Obama alilakiwa na kundi dogo la watu huku wakosoaji wake wakijikusanya kwa maadamano ya kupinga sera za kigeni za Marekani.

Obama aliepushwa na kadhia hiyo, huku yeye mwenyewe asijuwe kile kilichojili kutokana na kazi kubwa iliyo

Polisi wakipika risasi na mabomu ya tahadhari wakati wa maandamano nje ya Chuo Kikuu cha Soweto jijini Johannesburg chuo ambacho Rais Obama alikuwa anakitembelea

Polisi wakipiga risasi na mabomu ya tahadhari wakati wa kutawanya maandamano nje ya Chuo Kikuu cha Soweto jijini Johannesburg chuo ambacho Rais Obama alikuwa anakitembelea

fanywa na polisi wa Afrika Kusini walio lazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji muda mchache kabla ya msafara wake kupita kuelekea katika Chuo Kikuu cha Johannesburg, ambapo uliofanyika mkutano pamoja na maswali na majibu kutoka kwa watazamaji wa bara zima la Afrika.

Moja ya sababu ya kuchukulia ugeni huu kuwa wa kawaida, imeelezwa ni kukosa msisimko baada ya kutopata manufaha kutoka kwa  huyo kiongozi mweusi wa White House.

Kijana mmoja wa Afrika Kusini aliniambia alifanya sherehe wakati Obama alipochaguliwa kwa mara ya kwanza lakini, “sasa tumeona kwamba hakuna tofauti kati yake na marais walio mtangulia wa Marekani“.

Miongoni mwa watu wachache ambao walijitokeza kumlaki Obama lakini hawakuridhika ni pamoja na mfanyabiashara Alex Motloung, 40.

Motloung alisubiri kwa zaidi ya lisaa limoja ili kumuona rais wa Marekani akipita mitaa ya Pimmville Soweto kama ilivyokuwa imepangwaya bila kukata tamaa, ingawa, kama ilivyo pangwa msafara wa rais ulipita ila magari yalikuwa kwenye mwendo kasi wa zaidi ya km 140 kwa saa hivyo kumfanya ashindwe kumuona habiria yoyote ndani ya magari hayo.

Awali katika mkutano wa pamoja na wanahabari viongozi hao wawili Obama wa Marekani na mwenyeji wake Rais Zuma ambaye alimliganisha Obama na Nelson Mandela, ambaye kwa sasa ni mgonjwa huku swala la afya yake ikigonga  mawazo ya wananchi wote wa Afrika Kusini bila jawabu.

Zuma alibainisha kuwa wote walikuwa ni marais wa kwanza weusi wa nchi zao, na hivyo kuchochea “ndoto ya mamilioni ya watu wenye asili ya Afrika na Waafrika wanaoishi nje, ambao hapo awali walidhulumiwa“.

Motloung kwa kufuata ulinganifu huu yeye alisema ni yamkini Obama alikuwa na mafanikio ya kuvutia zaidi kuliko Madiba (Mandela).

“Obama amefanya kile ambacho kina onyesha kwamba hakuna lisilowezekana” – hata nchi yenye  idadi kubwa ya watu weupe wanaweza kupiga kura kwa ajili ya mtu mweusi.

“Hii ndiyo tunataka Afrika Kusini, pale watu wanavyo weza kumuukumu mtu juu ya uwezo wake na si rangi ya ngozi, na hii ndiyo ndoto ya Madiba.”

Msisimko wa ziara ya rais Obama ulikuwa mdogo mahali pengine katika vitogoji vya Pimmville, kwa mfano maeneo kama ya Small  Kopie  (hill) karibu kabisa na  chuo kikuu ambacho ilifanya mkutano, wananchi waliendelea na shuguli zao kama kawaida.

Wanandoa walionekana wakiwa wamejilaza kwenye jua nyakati za alasiri ikiwa ni njia ya kupambana na baridi kali nyakati za usiku ambayo ni kawaida ya maeneo haya ususan nyakati hizi za majira ya baridi, makundi ya vijana walionekana kwenye migahawa wakinywa wengine kwenye vijiwe vya vinyozi.

Baadhi ya vijana wa Kiafrika walioalikwa kushiriki katika Mr Obama mkutano "ukumbi wa mji" walikuwa msisimko kuwa kuna

Baadhi ya vijana wa Kiafrika walioalikwa kushiriki kwenye mkutano na Obama “ukumbi wa Town Hall”.

Ntuthuko NzimandeDlamini, (24), mwanafunzi wa sheria alisema kwa hali yoyote ile uwezi kumliganisha Obama na  Mandela, ambaye alitumia miaka 27 jela kwa kupinga utawala wa wazungu wachache.

Lerato Mahasha kwa upande wake alisema yeye alifurahia ujio wa ziara ya rais wa Marekani lakini amekelwa na hatua za usalama, ambazo zimepelekea barabara na chuo kikuu karibu chote kufungwa.

Wakati Rais Zuma alianza kutoa maoni yake kwa kumsifu Obama, yeye pia akumungunya maneno pale  alipo weka hadharani ubabe wa sera za kigeni za nchi hiyo kubwa duniani.

Alibainisha kwamba ongezeko la wanamgambo wa Kiislam katika nchi jirani ya Mali na nchi za Afrika Magharibi ilikuwa ni matokeo ya kuanguka Kanali Gaddafi kutoka madarakani.

Advertisements

RAIS OBAMA AVUNJA UKIMYA NA KUSEMA SABABU ZA KUTOTEMBELEA KENYA

Barack na Michelle Obama walipo wasili katika jiji la Pretoria, South Africa jana

Barack na Michelle Obama walipo wasili katika jiji la Pretoria, South Africa jana

Barack Obama avunja ukimya na kusema kwanini alisisitiza kwa nini aliamua katika ziara yake ya pili ya Afrika kama Rais wa Marekani kutotembelea KENYA .

Alikuwa akijibu swali kutoka Kenya kwa njia ya tekhama ya mawasiliano, juu ya ahadi yake aliyoitoa kutembelea nchi ya baba yake wakati wa urais wake. Kauli hiyo alizungumza wakati akiwautubia vijana zahidi ya mia moja walio kuwa wamekusanyika katika kitongoji cha Soweto katika Chuo Kikuu cha Johannesburg Juni 29 2013.

“Mimi bado naendelea kuwa rais kwa miaka mitatu na nusu zaidi,” alisema alipoulizwa kupitia kiungo video kutoka Nairobi kwa nini hakupanga kutembelea nchi hiyo “. Nimeweza kujifunza kama rais kwamba watu si tu wanataka wewe kutimiza ahadi yako, lakini wanataka kutimiza ahadi yako jana. “

Lakini Obama alikiri kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ambayo bado inasikiliza kesi dhidi ya rais wa Kenya na makamu wake ni moja ya ushawishi wa uamuzi wake. “Mimi nafikiri si wakati muafaka wa kutembelea Kenya,” alisema lakini aliahidi bado anaweza kufanya safari ya kutembelea Kenya kabla ya wakati wake akiwa rais.

Mapema katika mkutano wake na wanahabari mjini Pretoria, Obama alisema akutembelea Kenya katika ziara yake kwa sababu ya migogoro ya kimataifa, ambao ni Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari kwa kumshtaki Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji, mateso na matendo ya kinyama yanayo daiwa kufanywa na wafuasi wake katika ghasia baada ya uchaguzi wa Kenya 2007.

Muda huu siyo muafaka kwangu kama rais wa Marekani kutembelea Kenya wakati masuala hayo bado hayaja patiwa ufumbuzi“.

Lakini alibainisha yeye alitembelea Kenya mara kadhaa hapo awali na anatarajia pia kutembelea katika siku zijazo.

BREAKING NEWS: YA MTWARA SASA YAHAMIA MGODI WA DHAHABU BULYANHULU – KAKOLA NI MWENDO WA MAWE NA RISASI TU…

 • WASUKUMA WAACHANA NA MSEMO WAO WA NDUHU TABU YANI HAKUNA SHIDA WANAPAMBANA NA POLISI.

 • MADAI YAO NI KUPEWA ARDHI YA KUCHIMBA; INADAIWA JANA POLISI WALITEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA KUWAPIGA WAKOLOFI NA KUSABABISHA KIFO CHA MCHIMBAJI MMOJA MDOGO.

 • POLISI WA KITUO CHA BUGARAMA WAZIDIWA SASA WAOMBA MSAADA KUTOKA KAHAMA NA KAKOLA.

Hali ni ya wasiwasi mpaka dakika hii mgodini wa dhahabu wa Bulyanhulu na maeneo ya jirani huku barabara kuu ya kuingia mgodini ikiwa imefungwa na wananchi  kwa kutumia mawe na magogo wakidai na wao wapewe sehemu ya kuchimba kandokando ya mgodi wa Bulyanhulu ili nao waweze kujikimu kimaisha.

Hakuna kuingia wala kutoka, Hakuna gari wala bodaboda. Ni mwendo wa mabomu ya machozi tu ndiyo yanayoendelea kulindima mpaka sasa katika kijiji cha Kakola.

Hali hii imeanza kuanzia saa kumi jioni kabla ya shift ya mchana. Kwa ujumla wafanyakazi wa shift ya usiku hawakuingia na waliokuwa kazini wanajaribu kutafuta mbadala wa kufika makwao.

Habari za sasa hivi zinasema jeshi la polisi kituo cha Bugarama limeomba nguvu kutoka Kahama na Shinyanga kwani vurugu ni kubwa sana kiasi cha kulazimu polisi kutumia risasi za moto.

Hakuna maongezi zaidi ya mawe na risasi. Ila inavyoonekana polisi ni wachache na raia ni wengi isitoshe giza nalo limeingia hivyo hali inazidi kuwa si salama tena.

Inadaiwa jana polisi waliuwa mchimbaji mdogo mmoja aliyekuwa anachimba pamoja na wenzake nje ya fensi ya mgodi, jambo ambalo limepelekea asira miongoni mwa wananchi hasa wale wa asili ya Wasukuma na sasa wamejitutumua! Ule msemo wao wa ‘nduhu taabu’ yaani hakuna shida umekwisha. Uvumilivu wa kuona zao zinaondoka bila kimegewa umefikia mwisho. Wanaambulia vumbi tu.

Ikumbukwe kuwa eneo hilo linalodaiwa na wananchi waliwahi kulichimba yapata miezi kama 5 iliyopita kabla mamlaka ya mgodi wa Barrick kuwafukuza. Mamia kama si maelfu ya polisi nao wako njiani kutoka wilayani na makao makuu ya mkoa usiku huu kuja kurejesha utulivu.

kwa taarifa kamili endelea kutembelea blog yako.

MKETO WA CHAMA CHA CUF NI MZIMA, YUKO GEREZANI AKIWA AMEJERUHIWA KWA KIPIGO.

m2s breaking news

Habari ambazo zimethibitishwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya CUF kupitia kwa Juma Mtatiro zimethibitisha kuwa Mkurugenzi wa CUF wa uchaguzi taifa ni mzima na hajapata ajali yoyote.

Mtatiro amesema kuwa kwa sasa uko Mtwara na ametoka magereza mida hii na kufanikiwa kumuona Mketo akiwa mzima isipokuwa yeye na wenzake wamepigwa sana. akufafanua kuwa wamepigwa na nani au nini kilicho wapata.

M2S wanaomba radhi kama kunausumbufu wowote ulio tokana na Taarifa za awali kuhusu ajali waliyopata wakiwa mikononi mwa wanajeshi wa JWTZ.

BREAKING NEWS: MKETO WA CHAMA CHA CUF WAOFIWA KUFARIKI DUNIA WAKIWA MIKONONI MWAJESHI

m2s breaking news

Habari tulizopokea hivi punde ambazo bado kusibitishwa zinadai kuwa Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni Uchaguzi na Bunge wa Chama Cha Wananchi CUF – Shaweji Mketo amefariki dunia baada ya gari waliokuwemo kukamatwa na wanajeshi wa JWTZ, inadaiwa kuwa wakati wakipelekwa Naliendele gari ilipata ajali na ndipo mauti yakawakuta, Idadi ya waliopoteza maisha bado haijajulikana.

Mwenyekiti wa CUF Lipumba inadaiwa kunukuliwa kuwa alipokuwa anajaribu kufwatilia swala hilo alijaribu kupika simu ya Mketo kwa mshangao alipokelewa na mtu asiemjua huku akitoa matusi mazito.

juhudi za wanahabari wa M2S bado zinaendelea kujaribu kupata ukweli. Pindi tukipata lolote tutawajuza.

VILIO, MATESO, DHULUMA NA UKATILI UNAFANYIKA MTWARA. SAUTI ZAO MBONA HAZISIKIKI? WANAHABARI WAKO WAPI?

NI MATESO, DHULUMA NA UKATILI MTWARA.

Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni Uchaguzi na Bunge wa Chama Cha Wananchi CUF – Shaweji Mketo ajulikani alipo. ifuatayo ni taarifa kuhusu yanayojiri mtwara hususan wanausalama na wanajeshi waliopiga kambi Mtwara MJINI.

Mketo alienda Mtwara MJINI jana na Leo asubuhi alihudhuria mahakamani ambapo kesi ya Mwenyekiti wa vijana CUF taifa (JUVICUF) Katani Ahmed Katani iliahirishwa.

Baada ya ahirisho hilo, Mketo alikutana na wanachama wa CUF walioko Mtwara MJINI na kufanya nao kikao cha ndani. Katika kikao hicho alielezwa namna wananchi wanavyoteswa kikatili na askari jeshi. Moja ya jambo aliloelezwa ilikuwa ni juu ya mama mmoja aliyebakwa na askari na kisha mamlaka zote zimekataa kumsaidia kuujulisha umma unyama aliofanyiwa.

Mkurugenzi wetu Mketo alipojulishwa jambo hilo aliomba akutane na mama huyo. Baada ya kikao, Mketo na viongozi waandamizi wa wilaya akiwamo mhe. Kulaga ambaye ni katibu wetu wa wilaya walianza safari ya kuelekea Msimbati ambako mama huyo amejisitiri baada ya kubakwa na kunyimwa msaada na vyombo vilivyopaswa kumsaidia.

Mketo alifika Msimbati na kukutana na mama huyo na akachukua ushahidi mbalimbali. Wakati wanarudi Mtwara MJINI ndipo walipotekwa na Askari jeshi. Hivi sasa ukipiga simu za Mketo 0782 095 434 na ile ya Kulaga 0789 604968 zote zinapokelewa na askari jeshi na wanajibu kwa matusi ya nguoni na kebehi za Hali ya juu.

Tumefanya juhudi za kuwasiliana na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa polisi na serikali bila mafanikio. Nimempata hewani RPC wa Mtwara ambaye anakiri kuwa hajawashikilia viongozi wetu. Nimemjulisha kama wako mikononi mwa wanajeshi na wanausalama anasema hana mamlaka yoyote juu yao. HII ina maana kuwa mkuu wa Jeshi la polisi wa mkoa Leo hana dhamana ya raia wanaokamatwa na kuteswa katija eneo lake la kazi. Kama Leo Mtwara iko chini ya Jeshi la wananchi na wanatesa watakavyo, Mbona rais hajatangaza Hali ya hatari Mtwara??

Kwa taarifa zenye ushahidi, hadi sasa askari jeshi hao wameshawakamata na kuwapeleka makambini zaidi ya wananchi 100 ambapo wote hao wameteswa kinyama kwa kuvuliwa nguo zote, kumwagiwa maji mwili mzima, kupakwa chumvi mwilini na kuanza kutandikwa viboko vya miti maalum na kisha wakimaliza kuteswa huachiwa na kurudishwa uraiani kuuguza vidonda vinavyotokana na vipigo. Hakuna utawala wa sheria Mtwara, ni ubabe, ukatili na dhuluma. Hakuna mahakama wala JAJI, kila anayedhaniwa kuwa anapaswa kukamatwa lazima atakamatwa na kamwe hapelekwi mahakamani, anateswa kikatili na kuachiwa.

Kwa namna askari waliowashikilia wanavyojibu kikatili, unaweza kupata picha Mketo, Kulaga, dereva Kashinde na yeyote mwingine walivyo chini ya mateso makali ya wanyama hawa.

Tunaposema kuwa nchi hii kuna siku kila mtu atachoka tusilaumiwe. Siku hiyo itakapofika hatutasita kuamuru raia wapambane na askari kila watakapowaona, tutakapofika hapo nchi itabakia vipandevipande. Haiwezekani Leo kusini mwa Tanzania kumegeuka sehemu ya mateso, ukatili na unyama.

Tunaendelea kupambana kwa nguvu kuhakikisha kuwa serikali inawajibika, jeshi linawajibika. Hatutakubali kuona uhuru na utu wa wananchi wa nchi hii unapotezwa kwa faida za watu wachache.

Vyombo vya HABARI hivi sasa haviripoti chochote kuhusu mateso ya wananchi Mtwara. Ripoti za mateso ni Arusha, DSM na Mwanza. Nani atasimamisha ukatili huu wa watu wasio na hatia kama siyo mimi na wewe?

Mawakili wetu pamoja na mimi binafsi tunaelekea Mtwara kesho, lazima haki itendeke na tutaitafuta haki kokote na kwa njia yoyote.

J. Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
Chama Cha Wananchi CUF,
Tanzania Bara.
+255717536759

BREAKING NEWS:- SUGU AMEKAMATWA

m2s breaking news

Habari zilizotufikia hivi punde zinadai  Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi amekamatwa kwa kile kinachoitwa uchochezi na kumkashifu Waziri Mkuu Mzengo Pinda.

habari kamili kuwajia hivi punde.

update:- ametolewa nje kwa dhamana

Quote By Godbless Lema
Ninasikitika na Jeshi la Polisi kumkamata Sugu na kumhoji juu ya kauli yake kuwa Waziri Mkuu ni Mpumbavu kwa maana ya maneno aliyosema Waziri Mkuu Bungeni juu ya kuruhusu Polisi kushambulia raia.Napenda kusisitiza kuwa alichosema Sugu sio matusi bali ni sifa kwa Waziri Mkuu juu ya kauli yake ya kinyama aliyotoa Bungeni.

Sugu, uko sawa na Mungu anatambua hilo.

Lema

BREAKING NEWS: SASA UCHAGUZI WA MADIWANI ARUSHA MPAKA 14/07/2013

m2s breaking news

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi muda huu ametangaza kuahirishwa kwa uchaguzi wa Udiwani katika kata za Elerai, Themi, Kaloleni na kimandolu Manispaa ya Arusha hadi tarehe 14/7/2013. Amesema sababu kuu ni hali ya amani bado sio nzuri ya kuruhusu uchaguzi kufanyika kwa sasa. Itakumbukwa kuwa Uchaguzi wa Kata Hizi ambao ulikuwa ufanyike tarehe 16/6 uliahirishwa hadi tarehe 30/6 kutokana na mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kufunga kampeni wa CHADEMA. Kampeni hazitakuwepo kwa kipindi hiki hadi tarehe ya Uchaguzi.

Habari kamili kufuata baada ya muda mfupi.

KAMA UKUBALIANI NA KAULI YA PINDA KUHUSU KUPIGA RAIA SAINI HAPA

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA

Wito ni kuwataka wananchi wa Tanzania waandike na kuweka saini kumtaka mheshimiwa waziri mkuu kufuta kauli yake inayoruhusu polisi kupiga raia katika hotuba yake ya kufunga Bunge la bajeti tarehe 27 Juni 2013.

Naomba tufuate hii link hapa chini na ku-saini

Wito kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

HIVI NDIVYO UCHAGUZI WA ARUSHA PRESS CLUB ULIVYOFANYIKA JANA JIJINI ARUSHA

Mwenyekiti wa Arusha Press Club(APC)akitangaza kujiuzuru kwa kamati yake baada ya kumaliza muda wa miaka mitatu,wengine ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa APC,Eliya Mbonea(kushoto) na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti,Charles Ngereza
Wajumbe wakifatilia kwa makini mkutano wa uchaguzi huo
Umakini na kuweka kumbukumbu kwa waandishi wa habari ni jambo lililopewa umuhimu wakati wa uchaguzi,kutoka kushoto ni Abraham Gwandu,Kiko,Bertha Ismail,Asraji Mvungi,Veronica Mheta na Mustafa Leu wa Radio Uhuru
Kutoka kushoto ni Cynthia Mwilolezi(Nipashe)Janeth Mushi(Jambo Leo)na Jane Edward (Majira)
Mkongwe wa Habari Leo jijini Arusha,John Mhala na  Mwandishi hodari wa  gazeti la Uhuru,Lilian Joel wakifatilia mkutano
Claud Gwandu akiomba wanachama wenzake wamchague tena kuongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitatu katika nafasi ua Mwenyekiti ambayo aliibuka mshindi 
Mwandishi wa Nipashe na Radio One,Charles Ole Ngereza akiomba kura katika nafasi ya Makamu mwenyekiti 
Mgombea nafasi ya Mwekahazina,Pamela Mollel(mmiliki wa http://www.jamiiblog.co.tz na mwandishi wa gazeti la Majira)akiomba kura kwa mbwembwe nyingi
Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi ambaye ni mjumbe wa Bodi ya UTPC na Mwenyekiti wa Mwanza Press Club,Deus Bugaywa akikusanya kura
Baada ya uchaguzi kutoka kushoto ni Mwekahazina,Pamela Mollel,Janet Mushi(mjumbe)na Katibu Mkuu,Semmy Kiondo.Picha zote na http://www.rweyemamuinfo.blogspot.com

WAGOMBEA NA KURA ZAO KWENYE MABANO
MWENYEKITI;
Claud Gwandu(34)
Hapana (0)

MAKAMU MWENYEKITI
Charles Ole Ngereza (20)
Beatrice Gerard(16)

KATIBU MKUU
Semmy Kiondo(32)
Hapana (3)
Iliharibika (1)

KATIBU MSAIDIZI
Mustapha Leu(21)
Mosses Kilyinga(14)

MWAKAHAZINA
Pamela Mollel(26)
Veronica Mheta(9)

NAFASI ZA UJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJIJaneth Mushi(24)
David Frank(21)
Queen Lema(13)
John Nguge(9)
Daniel Sabuni(5)

community-herder-2.gif

BREAKING NEWS:- CHADEMA WAKUTANA NA WANAHABARI, WASEMA VIONGOZI WOTE WAMEFUNGULIWA KESI ZA JINAI.

CHADEMA

 • HENRY KAKAMATWA JUZI NA KUNYIMWA DHAMANA, INADAIWA AMESAFIRISHWA  KUPELEKWA IGUNGA AKIPITIA MWANZA, TABORA AKITUHUMIWA KUMWAGIA  MTU TINDI KALI.

 • MPAKA SASA WAMESHAKAMATA VIJANA ZAIDI YA 5 KUHUSIANA NA TUHUMA HIZO.

 • HINADAIWA MPAKA SASA POLISI WANAWASAKA M/KITI MBOWE, DR. SLAA, MYIKA NA TUNDU LISSU.

 • MNYIKA AMESEMA MAWAKILI WANAOTANGULIA KWENDA IGUNGA LEO NI PROF. ABDALLAH SAFARI, PETER KIMATARA NA HENRY MWANALIELA.

 • KESHO MAWAKILI WENGINE WATAONGEZEKA AMBAO NI MABERE MARANDO, NANYARO KICHEERE NA TINDU LISSU.

 • WANAOTAFUTWA NI KUTOKANA NA SHUTUMA YA KUMWAGIA MTU TINDIKALI KULE IGUNGA WAKATI WA UCHAGUZI MDOGO.

Habari kamili kupitia mitandao pacha ya http://www.community.co.tz na http://www.jamiiblog.co.tz kufuata hivi punde …

MAANDAMANO YA AMANI YA CHAMA CHA WANANCHI CUF, TAREHE 29 JUNI 2013 MPAKA IKULU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CUF

 • PROF.LIPUMBA KUONGOZA,MAANDAMANO KUPOKELEWA NA RAIS KIKWETE.


Waheshimiwa waandishi wa habari, kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya uongozi wote wa kitaifa wa Chama chetu, naomba kuchukua fursa hii kuwakaribisha Ofisi Kuu ya chama ili tupate fursa ya kuzungumza nanyi na kwa maana hiyo kuzungumza na watanzania kupia kwenu ili ujumbe uliokusudiwa na chama uweze kuwafikia wananchi popote pale walipo.

Tumewaita leo tarehe 22 Juni 2013 tukiwa na agenda moja kuu nayo ni kuwaeleza kwamba Chama cha Wananchi CUF kimeandaa Maandamano ya Amani siku ya tarehe 29 Juni 2013 maandamano ambayo yataanzia eneo la Buguruni kituo cha Mafuta saa nne kamili asubuhi, kupitia barabara ya Uhuru, Mnazimmoja, Bibi Titi, Posta mpya , Aridhi hadi Ikulu.

Maandamano hayo ambayo yataongozwa na Mwenyekiti wa Chama taifa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, yanatarajiwa kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au mwakilishi wake, na kwamba yanalengo la kufikisha malalamiko ya wananchi kutokana na vitendo vya ukatili vinavyofanywa na jeshi la polisi na jeshi la wananchi ambalo kimsingi taifa letu linaelekea mahali pabaya.

Waheshimiwa waandishi wabari, mtakumbuka tarehe 15 Juni 2013 wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakihitimisha mkutano wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata nne za Arusha, palitokea mlipuko wa bomu uliopoteza maisha ya wananchi wane kwa mujibu wa taarifa za polisi na wengine wengi kujeruiwa vibaya.

Kwa kuwa jambo hili lipo katika hatua za uchunguzi, Chama cha CUF hakikusudii kuingilia uchunguzi unaoendelea lakini tunataka kufikisha ujumbe kwa rais kwamba hii si mara ya kwanza kuundwa kwa tume mbalimbali za uchunguzi hapa nchini. Kinachotusikitisha ni kuwa hata mara baada ya uchunguzi huo, hakuna ripoti inayotolewa hadharani kuonyesha chanzo cha tukio, wahusika na hatua zilizo au zinazotarajiwa kuchukuiliwa.

Tutamtaka Mheshimiwa rais kuhakikisha ripoti ya uchunguzi itokanayo na maafa yaliyotokea Arusha iwekwe wazi na serikali iwachukulie hatua stahiki wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo ili iwe funzo kwa wengine au wale wenye kuwa na malengo yanayofanana na hayo kwa kuwa Tanzania ni yetu sote na haitowezekana watu wachache wayachezee maisha ya watu kwa sababu ya kukidhi matakwa binafsi ambayo hayana tija kwa jamii.

Maandamano pia yanalenga kuishinikiza serikali kukomesha vitendo vya kinyama, vitendo vya kijangili vinavyofanywa na Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kuwakamata, kuwatesa, na kubaka wananchi wasio na hatia wa Mkoa wa Mtwara na hasa wanaoishi katika wilaya za Mtwara Mjini, MtwaraVijijini, na Newala huku baadhi yao wakichomewa nyumba zao moto na wengine wakiporwa mali zao.

Waheshimiwa waandishi wa habari, mtakumbuka hivi karibuni pamekuwa na fukuto la suala la gesi katika Mkoa wa Mtwara ambapo baadhi ya maafisa wa Serikali wamekuwa wakipotosha madai ya wananchi ikidaiwa kwamba wananchi wa mkoa huo wamesema hawako tayari kuona gesi yao inatumiwa na wananchi wengine kinyume na wale wa mikoa ya Lindi na Mtwara jambo ambalo si kweli lakini wanayafanya haya ili kuwajengea chuki dhidi ya watanzania wengine ionekane kwamba wananchi wa Mtwara na Lindi ni wabinafsi na wasioitakia mema nchi yetu.

Madai ya wananchi wa Mtwara yanatokana na uzoefu waliokuwa nao katika maeneo yote ambapo pana miradi ya kimaenedeleo itokanayo na maliasili ya nchi, maeneo hayo yamekuwa masikini na watu wachache wamekuwa wanatajirika, walichotaka kufahamu wananchi watanufaikaje na uwepo wa gesi katika maeneo yao kabla ya kuinufaisha nchi mzima kwa kuwa wao ndiyo watakuwa wa kwanza kuathirika ikiwa patatokea hitilafu yoyote itokanayo na uchimbwaji wa gesi hiyo.

Leo tunaweza kujifunza kutokana na uchimbaji wa Dhahabu Geita (GGM), uchimbaji wa Almasi Mwadui Shinyanga, Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Nyamongo na maeneo mengine mengi, nini hali ya maisha ya wananchi wa maeneo hayo.

Pamoja na upotoshwaji wa makusudi uliofanywa na unaoendelea kufanywa na watendaji wa serikali juu ya suala la gesi ya Mtwara, inashangaza hata Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambalo lilionekana awali kutenda haki kwa wananchi wa Mtwara baada ya wananchi kukosa imani dhidi ya Polisi kutokana na wizi na uporaji wa mali za wananchi huku wakichoma moto baadhi ya maduka kwa lengo la kuhalalisha vitendo vya hujuma pamoja na kuchoma moto soko la Nkana Read, Jeshi lililojijengea heshima kwa jamii nalo limeanza kuingia mkumbo wa kuwatesa raia bila makosa.

Mwanzoni mwa wiki hii Mkurugenzi wetu wa siasa wa wilaya ya Mtwara Mjini Mhe. Saibogi ambaye pia ni mwenyekiti wetu wa serikali ya Mtaa alitekwa na wanajeshi na kumpeleka katika Kambi yao iliyopo barabara ya kwenda Nanyamba ambapo walimvua nguo na kumpiga mijeredi usiku kucha bila hatia na kumuachia asubuhi yake huku wakiahidi kuwakamata viongozi wengine wa CUF ili kutoa funzo kwa wale wanaopigania haki za wananchi.

Matukio ya namna hii si ya kuyafumbia macho na yanatengeneza serikali yenye kiburi isiyotokana na maamuzi ya raia. Maisha ya namna hii hayawezi kuendeshwa katika nchi inayojiita huru kama yakwetu na badala yake mambo haya yanatukumbusha enzi za utawala wa kikoloni ambpo CUF kamwe hatupo tayari kuruhusu vitendo vya kishenzi kuona vinafanyika nchini petu.

Tulikianzisha Chama hiki kwa madhumuni ya kuwaunganisha watanzania wote popote walipo, bila kujali itikadi zao, waweze kukataa aina yoyote ya uonevu, ukandamizaji, unyanyasaji, ubaguzi na udhalilishaji wa kisiasa au kiuchumi.

Aidha tuna dhamira ya kulinda, kutekeleza na kuzienzi haki za Binadamu pamoja na kuinua uchumi wa nchi kwa siasa zitumikie uchumi badala ya uchumi kutumikia siasa kama inavyofanyika hivi sasa. CUF tunaamini katika siasa za ustaharabu ambazo zitatuwezesha kuwa na jamii salama yenye mshikamano na ushirikiano katika kuijenga nchi yetu, lakini wenzetu wanatumia upole wetu na ustaharabu wetu kutufanyia vitendo vinavyokiuka utu wa mtu na hatimaye kila aliyepewa mamlaka ya kuongoza sehemu ya nchi yetu anageuka kuwa mfalme na kuamrisha kamata Yule, mpe kesi Yule na mwache Yule. Uvumilivu wetu usiwe mtaji kwa CCM na serikali yake kutufanya watakalo, nasi ni binadamu.

Waheshimiwa waandishi wa habari, maandamano yetu yanalenga pia kuitaka serikali kuwasikiliza wananchi wa Mtwara kwa kukaa nao chini, kujua hoja zao na kutoa ufafanuzi pale patakapobidi, sisi tunaamini wanazo hoja za msingi na wakisikilizwa serikali itaona namna ya kuzifanyia kazi hoja hizo badala ya kukurupuka na kutoa kauli za kibabe eti hawa wanachochewa na vyama vya siasa au pana watu wasioitakia mema nchi ndiyo wanachochea, kauli hizi zinajenga chuki na zanakosa uzalendo wa taifa. Haiwezekani hao wanaojiita ndiyo wazalendo halisi wawe wanaifidi nchi alafu tuendelee kukaa kimya kama vile wananchi wa kusini ni watu wasioweza kufikiri na kupambanua baya na zuri.

Wakati wananchi hawa walipopeleka maombi yao kupitia kwa Mhe. Mohamedi Habibu Mnyaa Mbunge wa Mkanyageni, ilikuwa nafasi nzuri kwa serikali kuweza kusikiliza maombi yao na kutoa maamuzi, badala yake siasa zikatumika, maombi yakakataliwa leo Bunge linaunda kamati ya uchunguzi iende mtwara wakachunguze nini ikiwa tayari hoja zao zilikataliwa?

Ieleweke kuwa nchi yetu itajengwa na watanzania wenyewe kwa kushirikiana na kusikilizana. Amani ya kweli itapatikana ikiwa haki itaonekana kutendeka kwa jamii yote. Waheshimiwa waandishi wa habari, haya ni sehemu tu ya mambo ambayo tunakusidia kumfikishia rais wetu ili aweze kuyafanyia kazi.

Mungu Ibariki CUF, Mungu ibarika Tanzania.


Imetolewa na Shaweji Mketo,
Naibu Mkurugenzi wa Mipango, Uchaguzi na Siasa,
tarehe 22 Juni 2013

CCM UK WATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA SHAMBULIA LA BOMU NA RISASI KWENYE MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA.

Chama Cha Mapinduzi Logo 86318

Chama cha mapinduzi Tawi la Uingereza kwa masikitiko makubwa tunapinga vikali tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa hadhara wa chadema uliofanyika jijini Arusha hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu watatu na zaidi ya watu 40 kujeruhiwa.

Tunatoa pole zetu za dhati kwa familia za wafiwa na kwa wale wote waliojeruhiwa katika janga hili la kikatili na kuwatakia uponaji wa haraka.

Tukio hili limefuata badala ya lile la awali lililotokea katika kanisa katoliki la mtakatifu Joseph mnamo tarehe 5 mei mwaka huu jijini Arusha, ambapo pia lilisababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi zaidi ya watu 60.

Ni imani yetu kwamba uchunguzi kamili wa mashambulio haya utakamilika haraka na wahusika watakamatwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria.

Tanzania ni nchi yenye hazina ya amani ya muda mrefu. Vitendo vya kigaidi vya aina hii na ambavyo vina mlengo wa kutugawanya kamwe havitavumiliwa na vikomeshwe ili kuondoa wimbi la vurugu zinazoweza kusababisha uvunjikaji wa amani.

Tunawasihi Watanzania wote tuwe pamoja na wenye busara na kuondokana na itikadi zozote za kisiasa au ushabiki wa vikundi , aidha na maneno ya kujibizana pasipo sababu. Ili kuondoa ama kutoamsha hisia za chuki zisizo na manufaa kwa yeyote yule na Taifa kwa ujumla , ni vyema wakati wa majanga kama haya kuachia vyombo vya usalama kufanya kazi yake ya uchunguzi bila kuingiliwa na vyama au kundi lolote kwa maslahi binafsi au umaarufu wa kisiasa .

Tunawasihi WaTanzania tuienzi amani yetu iliyolelewa kwa kipindi kirefu na Waasisi wa Taifa letu wakiongozwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Amani ambayo ni mfano na hadaa kwa wapenda amani kote ulimwenguni.

Imetolewa na idara ya Itikadi Siasa na Uenezi

CCM UINGEREZA – UK.

PINDA! HAKI YA KUJITETEA NI HAKI YA MSINGI YA MWANADAMU

??????????????????????

DSCF9336

18. Subject to the provisions of section 18a, a person is not criminally liable to an act done in the exercise of the right to self-defence or the defence of another or the defence of property in accordance with the provisions of this Code.

Mojawapo ya haki ambazo labda hatujazizungumza sana na hazieleweeki ni haki ya kujitetea (the right of self defence). Haki hii haijaleweka au haieleweki kwa wengi kwani inachanganywa na kuonekana ni uhalifu.

Mwanadamu anayo haki ya kulinda nafsi yake na mali yake kutoka kwenye dhulma yoyote ile.

Mara kwa mara haki hii tunaitumia kwa njia za sheria – kama kwenda mahakamani au kumkamata mwizi.

Lakini inakuwaje kama jambazi amevamia familia yako na kuitishia maisha na wewe una silaha? Je unaweza kutumia silaha kuitetea familia yako? Jibu ni ndiyo! Hiyo ni haki yako na ukifanya hivyo kwa kujitetea maisha yako na ya familia yako ni vigumu kwa mahakama kukuta una hatia isipokuwa kama inaonekana kwa mfano, umeweza kumweka jambazi chini ya ulinzi na kumnyang’anya silaha halafu kwa kisasi ukaamua kumuua! Hapo huwezi tena kujitetea ‘self-defense”.

Lakini inakuwaje kama wanaokushambulia ni maafisa wa vyombo vya usalama? Je maafisa wa vyombo vya usalama wakifuata agizo la Pinda wakakukufuza na kuanza kukupiga bila kujaribu kukukamata au kukuletea mashtaka au si kwa ajili ya kukuweka chini ya ulinzi unatakiwa kufanya nini?

Je, polisi au wana usalama wanaweza kuja nyumbani kwako na kukushambulia kwa vile wanakushuku wewe ni mkorofii kama walivyofanya Mtwara je wewe nyumbani kwako una haki ya kujitetea? Baadhi ya watu ambao nimewasoma toka jana wanaamini kuwa serikali inaweza kupiga wananchi wake na wananchi hawapaswi kujitetea! Kuna watu ambao ukiwasoma wanaamini kabisa kuwa polisi na vyombo vya usalama vina haki na uwezo wa kuja na kukuambia “wanachotaka” na wewe unatakiwa ufanye wanachotaka kwa sababu unatakiwa ‘kutii sheria bila shurti’!

Wapo kabisa ambao wanaamini kabisa kuwa Mkuu wa Polisi fulani anaweza kuja na nyota na mwenge wake na kukuambua “Chochote” na wewe unatakiwa ufanye tu kwa sababu yeye kasema!

Kwamba wanaamini wananchi hawatakiwi kuwabishia polisi, hawatakiwi kuwauliza na kwa hakika hawatakiwi kuwapinga! Je hili ni kweli? Je ni kweli polisi wana nguvu hiyo katika maisha ya watu wetu kiasi kwamba watu wetu wanatakiwa watii bila shurti!? Yaani, watii lolote, popote, kwa lolote na vyovyote kwa vile wameamriwa hivyo?

Mwanadamu siyo mnyama ambaye anaweza kusukumwa sukumwa au kunyanyaswa na watu wenye nguvu na madaraka. Mwanadamu ameumbwa na dhamira na utu wake. Wapo wanadamu kati yetu ambao hawajali kunyanyaswa alimradi wanaachwa na “amani”.

Wapo kati yetu ambao utu wao kwao ni chakula cha leo tu na ukiwapa chakula cha leo tu basi unaweza kuwafanyia lolote, popote, na kwa lolote! Naam, wapo kati yetu ambao hawawezi kuhoji serikali yao, hawawezi kuipinga, na kamwe hawatothubutu kulalamika kwa sababu wanaogopa au kuhofia kuonekana siyo watiifu. Hawa wakiambiwa ‘inama’ wanainama, ‘inuka’, ‘lala’ wanalala na wakiambiwa ‘lia’ wanalia kama wameona mzimu! Hawa hawana namna ya kuwasaidia kwani kila jamii inayo watu kama hao; watu ambao wanaabudu kwenye altare ya watawala wa zama zao!

Self Defence Section 18 of the Penal Code

18. Subject to the provisions of section 18a, a person is not criminally liable to an act done in the exercise of the right to self-defence or the defence of another or the defence of property in accordance with the provisions of this Code.

18A. (1) Subject to the provisions of this Code even person has the right—
(a) to defend himself or any other person against any unlawful act of assault or violence to the body; or

(b) to defend his own property or any property in this lawful possession, custody or under his care or the property of any other person against any unlawful act of seizure or destruction or violence.

(2) in this section, the expression “property of any other person” includes any property belonging to the Government or a public corporation or an employer or any property communally owned by members of the public as a co-operative society or a village, whether or not that village is registered under the Villages and Ujamaa Villages (Registration, Designation and Adminisration Act, 1975.

18B. —(1) In exercising the right of self -or in defence of another or defence of property, a person shall be entitled only to use such reasonable force as may be necessary for that defence.
(2) Every person shall be criminally liable for any offence resulting from excessive force used in self-defence or in defence of another or in defence of property.
(3) Any person who causes the death of another as the result of excessive force used in defence, shall be guilty of manslaughter.

18C. —(1) The right of self-defence or the defence of another or defence of property shall extend to a person who, in exercising that right, causes death or grievous harm to another and the person so acting, acts in good faith and With an honest belief based on reasonable grounds that his act is necessary for the preservation of his own life or limb or the life or limb of another or of property, in the circumstances where-

(a) the lawful act is of such a nature as may reasonably cause the apprehension that his own death or the death of another person could be the, consequence of that act; or

(b) the lawful act is of such a nature as may reasonably cause the apprehension that grievous harm to his own body or the body of another could be the consequence of that unlawful
act; or

(c) the unlawful act is with the intention of committing rape or defilement or an unnatural offence; or

(d) the unlawful act is with the intention of kidnapping or abducting; or

(e) the lawful act is burglary or robbery or arson or any offence which endangers life or property.

(2) If, in the exercise of a right of defence in accordance with this Code, the person exercising that right is in such a situation that he cannot effectively exercise that right without risk of harm to an innocent person or property, his right of defence extends to the running of that risk.

SEHEMU YA TAFSIRI NA MAELEZO YA SHERIA HII IMEFANYWA NA MWANAKIJIJI

TABLETS MPYA ZA SAMSUNG SASA KUTUMIA OS MBILI

samsung-ativ-q-android

Alhamisi 20.6.2013 samsung ilitoa laptop (tablet) ambayo inauwezo wa kutumia operating system (OS) mbili kwa wakati mmoja, android jelly bean na window 8, lengo kuu ni kuwapa wateja wao ladha tofauti baada ya kuwa na device mbili zinazorun OS  mbili tofauti.

kulingana na melezo ya cnet editors wanasema wakati wa matumizi kutoka OS moja kwenda Nyingine ni rahisi sana, haihitaji kurestart system na inachukua sekunde chache tu.

Uzuri wa hii kitu ni kwamba inashare files, folder lililohifadhiwa kwenye android na katika window 8,

 • Je tutarajie nini kampuni nyingine nyingi kuiga kitu kama hiki???,

 • Vipi samsung atafanikiwa katika mauzo ya hii device ama la ???,

Baadhi ya watu wamependezwa na ubunifu huu, huu ni mwendelezo wa samsung kujaribu kuliteka soko, awali waiingia mkataba na Mwanmziki Nguli  Jay z wa kuuza album yake katika simu sa samsung galaxy.

source:Android duels with Windows 8 on Samsung hybrid | Business Tech – CNET NewsAndroid duels with Windows 8 on Samsung hybrid | Business Tech – CNET News

MWANDISHI PAUL SARWAT AZUNGUMZIA KILICHOTOKEA SOWETO ARUSHA JUNE 15 2013

??????????????????????

Hii ndiyo sehemu ya mkutano iliyoshambuliwa kwa bomu. Picha hii ilipigwa wakati mkutano unaendelea takriban dk. 20 kabla ya bomu kulipuka.??????????????????????

Bahadhi ya wahanga wa shambulia la bomu.??????????????????????

 Damu ilivyo tapaka eneo lilishambuliwa kwa bomu.??????????????????????

Taharuki ikiwa dhairi kwa baadhi ya watu, huku mwenyekiti wa Chadema akiongoza wananchi kusaidia waathirika wa mkasa huo.??????????????????????

Pamoja na Kazi Kubwa ya Viongozi pamoja na wanachi ya kutoa msaada walizawadiwa mabomu ya machozi na polisi.

NAANZA kuandika simulizi hii kwa kumshukuru Mungu kwanza, kwa kuninusuru na mlipuko wa bomu uliotokea Jumamosi ya Juni 15, mwaka huu, katika mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa kuhitimisha kampeni za udiwani wa katika kata nne za ndani ya Jiji la Arusha.

Kwa hakika kabisa, Jumamosi hiyo ya Juni 15, 2013, ‘imejenga mnara’ wa kumbukumbu mbaya ndani ya moyo wangu, na itanichukua muda mrefu kidogo kusahau tukio hilo la kutisha na kuhuzunisha sana.

Naikumbuka siku hiyo vizuri. Kwanza, tofauti na siku zote, siku hiyo niliamka saa nne asubuhi, badala ya muda wangu wa kawaida wa saa 12:30 au saa moja asubuhi. Hiyo ilitokana na kwamba jana yake, yaani Ijumaa ya Juni 14, nilikuwa katika safari ndefu ya kutoka Iringa hadi Arusha nikitumia usafiri wa umma.

Nilikuwa Iringa kwa siku tano kuhudhuria warsha ya Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi kutoka mikoa yote nchini kuhusu ujangili, iliyokuwa imeandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Kwa hiyo, kutokana na safari hiyo ndefu, mimi na waandishi wenzangu Musa Juma na Anthony Mayunga (Mwananchi), David Ruennyagira (Radio 5) na Eliya Mbonea (New Habari (2006) Ltd) tulifika Arusha mjini usiku wa manane, tukiwa na uchovu mwingi.

Baada ya kupumzika nyumbani na kupata chakula cha mchana, nilikwenda mjini Arusha nikiwa nimeambatana na wanangu wawili, Laureen (12) na Lantah-Sonia (4), na moja ya malengo yangu katika safari hiyo, ilikuwa ni kushuhudia uhitimishaji wa kampeni za uchaguzi kwa vyama vyote vilivyokuwa vinashiriki uchaguzi wa madiwani wa kata nne zilizokuwa zikigombewa.

Nilichagua kuanza na kata ya Kaloleni kutokana na kata hiyo, kwa sehemu kubwa, kuwa eneo la mji na pia vyama vya CHADEMA, CUF na CCM vyote vilikuwa vinahitimisha mikutano yao ya kampeni katika kata hiyo.

Kwanza nilianza na mkutano wa Chama cha Wananchi (CUF) uliokuwa unafanyika jirani na uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Hata hivyo, mkutano huo haukuwa na watu wengi wala shamrashamra zozote, na hata mgombea wa chama hicho, Abbas Darwesh, alikuwa bado hajaanza kuzungumza.

Hali hiyo ya msisimko mdogo katika mkutano huo wa CUF, ilinifanya niamue kwenda kwenye mkutano wa CCM uliokuwa ukifanyika Ilboru, mkabala na ofisi za Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), ambao mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye.

Mkutano ulikuwa na mahudhurio makubwa na shamrashamra nyingi. Nilisikiliza hotuba za viongozi na makada mbalimbali wa CCM hadi saa 10:45, nilipoamua kuondoka hapo na kwenda kwenye mkutano wa CHADEMA ambao walikuwa katika viwanja vya Soweto, umbali wa kama mita 500, kutoka eneo ambalo CCM walikuwa wakihitimisha kampeni zao.

Kabla ya kuingia ndani ya viwanja hivyo, nilitafuta sehemu salama ya kuegesha gari langu. Kutokana na umati wa watu nilioukuta katika viwanja hivyo, niliamua kuegesha gari hilo katika nyumba za AICC (Soweto Flats), umbali wa mita takriban 300 kutoka viwanja vya Soweto, nyumbani kwa mama mmoja ambaye ni rafiki wa familia yangu, na zaidi watoto wa mama huyo na wa kwangu wanasoma shule moja. Hapo ndipo lipowaacha pia watoto wangu wawili hao.

Nilifika eneo la mkutano, kwa kweli uwanja wa Soweto ulikuwa umejaa watu.

Nilijaribu kupenya ndani ya umati huo wa watu hadi eneo la jukwaa kuu ili nipate fursa nzuri ya kuwasikiliza viongozi na makada wa chama hicho wakinadi sera zao.

Hali ilikuwa ya utulivu mkubwa katika mkutano huo, huku mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, akiwa jukwaani akiwanadi wagombea, na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, pamoja na viongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa wakiwa jukwaa kuu.

Kutokana na wingi wa watu muda wote nilikuwa nyuma ya gari la matangazo ambalo pia hutumika kama jukwaa na viongozi walikuwa juu ya gari hilo.

Baada ya Lema kumaliza, alimkarabisha Mbowe na wakati anaanza kuhutubia, ilikuwa yapata saa 11:20 jioni. Nilimwomba mpiga picha wa mtaani anayefahamika kwa jina la ‘Photo me’ atumie kamera yangu ndogo kupiga picha za umati ule wa watu pamoja na Mbowe akiwa jukwaani.

Nilikaa kwa muda kidogo eneo hilo la nyuma ya gari la matangazo, baadaye nilipenya pembeni ya gari hilo la matangazo ili niweze kwenda mbele ya jukwaa, lakini nikakutana na kizingiti cha kuzuiwa na mmoja wa walinzi wa kike wa CHADEMA, maarufu kwa jina la Red Brigade.

Wakati mlinzi huyo ananizuia, baadhi ya viongozi wa CHADEMA, akiwamo Judith William, Katibu wa Baraza la Wanawake wa chama hicho (Bavicha), Kata ya Sokoni One, aliyepoteza maisha katika tukio hilo la bomu, waliingilia kati na kumtaka mlinzi wao huyo asinizuie kwa kuwa mimi ni Mwandishi wa habari.

Hatimaye mlinzi yule aliniruhusu nikaingia eneo la mbele ya jukwaa.

Nilisalimiana na baadhi ya viongozi na makada wa chama hicho tunaofahamiana nao, akiwamo kada maarufu wa CHADEMA katika siasa za Arusha, Kalist Lazaro.

Aidha, eneo hilo la mbele kulikuwa kumekaliwa na viongozi wa ngazi za kata kutoka wilaya ya Arusha mjini, pamoja na watoto wadogo waliokuwa wamekaa chini, wapiga picha wa vituo mbalimbali vya televisheni na wapiga picha wa kujitegemea.

Freeman Mbowe, baada ya kukaribishwa na Lema, alihutubia mkutano huo hadi saa 11:45, alipohitimisha kampeni hizo kwa kumtaka Lema kutangaza utaratibu wa kuondoka eneo lile kwa maandamano kuelekea kata ya Elerai.

Nami nilichukua nafasi hiyo kuondoka mbele ya jukwaa kuu kwa nia ya kumfuata mpiga picha aliyekuwa na kamera yangu, kabla ya kuungana na diwani wa Levolosi, Ephata Nanyaro, aliyeshuka jukwaani na baada ya kusalimiana, tulianza kuondoka eneo hilo la mkutano.

Lakini wakati bado tunashangaa eneo hilo, ghafla kukatokea kishindo kikubwa kilichoambatana na sauti ya kuogofya. Watu walianza kukimbia ovyo kuelekea huku na kule, na katika purukushani hizo, nilijikuta nikipigwa kikumbo kilichonisukuma hadi mtaroni, na kupata maumivu makali ya goti.

Kulikuwa na taharuki kubwa. Nilipoinuka kutoka mtaroni, nilimuona diwani Nanyaro akiwazuia watu kwa kuwatuliza, akisema kuwa ni ‘tairi la gari limepasuka’, lakini wakati huo huo kupitia gari la matangazo la CHADEMA, nikasikia sauti kali ya mbunge Lema ikisema; tumeshambuliwa kwa bomu.

Nilijaribu kurudi mbele ya gari la matangazo. Nilipofika mahali pale, ilikuwa balaa tupu. Zaidi ya watu 15 walikuwa chini huku damu zikiwa zimewatapakaa na katika eneo zima hilo mithili ya wanyama waliochinjwa. Kulikuwa na watoto wadogo, wanawake na watu wazima.

Nilimtambua kwa haraka Mama Judith William aliyekuwa amelala chini, huku akiwa ametapakaa damu mwili mzima, hali ilikuwa inatisha. Kwa haraka, nilikumbuka muda mfupi tu uliopita tulikuwa tumesimama eneo moja, na eneo hilo hilo ndipo bomu limetupwa. Alikuwa ameuawa kinyama. Sikuamini macho yangu!

Kulikuwa na watoto wadogo wamelala chini wakiwa na maumivu makali, hii ilinitisha sana na kunitia huruma, na hasa nikikumbuka kuwa hata nami nilikuwa mzazi wa watoto wenye umri kama niliowaona pale chini.

Nilijaribu kutoa kamera nipate picha ya mahali pale, lakini muda huo huo Polisi walianza kurusha mabomu ya kutoa machozi, na nikaanza kusikia milio ya risasi. Ilikuwa ni tafrani ambayo sikuwahi kuishuhudia.

Bomu lilitua karibu yangu na kulipuka, nilikimbilia eneo la wazi na wakati huo viongozi na makada wa CHADEMA walikuwa wanajaribu kuwaokoa majeruhi kuwapakia katika magari na kuwakimbiza hospitali.

Wakati nakimbia kujiokoa na risasi za moto na mabomu ya machozi nilimwona Mwenyekiti Mbowe akiwa amembeba mmoja wa watoto waliojeruhiwa, akiwa ametapakaa damu na kumpakia kwenye gari. Nilikimbia bila kusimama hadi nilipoacha gari langu na muda wote mabomu machozi yaliendelea kurushwa.

Nilipofika kwenye gari niliona kwa mbali gari la polisi pia likiondoka kwa kasi eneo hilo, nami pia niliondoa gari hadi baa maarufu ya Arusha Night Park na kuliegesha hapo.

Muda huo nilijaribu kuwasilina na Mhariri Mkuu wa gazeti hili la Raia Mwema, Godfrey Dilunga, kumweleza hali iliyotokea, lakini simu zilikuwa haziendi, na hii ilikuja kubainika baadaye kuwa kwa muda ule wa tukio hilo, mitandao yote ya simu ilikuwa haifanyi kazi.

Nilitafakari sana juu ya hatua ya polisi kurusha mabomu wakati walipaswa kutoa msaada wa kuokoa watu na kuwawahisha hospitali, sikupata jibu hadi wakati naandika simulizi hii.

Baada ya kuegesha gari nilirudi kwa miguu hadi uwanja wa Soweto. Niliwakuta makada wachache wa CHADEMA waliokuwa wanajaribu kuzuia (kulinda) eneo la mlipuko, huku eneo hilo likiwa na mabaki ya nguo, viatu na damu iliyotapakaa.
Niliendelea na kazi zangu kama mwandishi wa habari, licha ya kuwa na kumbukumbu za kuuawa kwa watu niliosalimiana nao muda mfupi hapo uwanja wa mkutano. Muda mfupi baadaye, nilikwenda Hospitali ya Selian. Huko majeruhi walikuwa wamefurika, huku madakatari na wauguzi wakijitahidi kutoa huduma ya kwanza na nje ya viwanja vya hospitali kulikuwa na umati mkubwa wa watu.

Kila moja alikuwa na ushuhuda wake, wengine walidai kumwona aliyerusha bomu likiwa katika mfuko mweusi wa ‘plastiki’ (rambo), wengine walidai baada ya kutupa alikimbia na wananchi walipojaribu kumfukuza, polisi waliwarushia mabomu ya machozi, wengine walidai alikimbia na kuingia ndani gari jeupe aina ya Landrover TDI. Kila mmoja alikuwa na hadithi tofauti.

Hapo hospitali hakukuwa na kiongozi yeyote wa Serikali wala wa Jeshi la Polisi, isipokuwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA pekee na wanachama wao waliokuwa wakiratibu shughuli zote, ikiwa ni pamoja na kutafuta damu kwa ajili ya majeruhi.

Hadi saa 4:30 usiku, majeruhi wote walikuwa wamepata huduma ya kwanza katika hospitali za Mount Meru, Selian na St. Elizabeth, na shughuli zote zilifanyika bila kiongozi hata moja wa Serikali kutokea.

Niliondoka eneo hilo nikiwa najiuliza maswali ambayo hadi sasa sijapata majibu yake. Nani anahusika na shambulio hilo? Kwa malengo gani? Nani kawatuma? Je; walengwa walikuwa viongozi wa CHADEMA? Tukio hilo linaashiria kuwa Arusha ambalo ni Jiji mashuhuri kwa utalii, likitoa ushindani mkali kwa majiji ya nchi nyingine kama Nairobi (Kenya), si salama tena kwa maisha ya watu na mali zao?

Kwa hakika, nimalizie kwa kumshukuru tena Mungu. Tukio hilo ni la kutisha, na waliohusika wana haki ya kulaaniwa. Kama si mapenzi ya Mungu, kuninusuru basi pengine, ningeweza kujeruhiwa vibaya au nami ningeuawa.

Nisingeweza kuonana tena na wanangu, mke wangu, ndugu na wanataaluma wenzangu na kwa kweli, kalamu yangu ingekuwa imefikia tamati. Lakini kwa mapenzi ya Mungu niko pamoja na natoa salamu za rambirambi kwa wote.

EXCLUSIVE VIDEO; VIDEO NZIMA YA MKUTANO WA CHADEMA ULIOSHAMBULIWA KWA BOMU LA KUTUPA KWA MKONO, RISASI PAMOJA NA MABOMU YA MACHOZI. MUDA NI 01:31:11.

 • TUNAOMBA RADHI KWA PICHA ZA KUTISHA NA MATUKIO AMBAYO SI MAZURI YATAKAYO ONEKANA.
 • BAADA YA MLIPUKO {EVENT OCCUR IN REAL TIME} HESABU MILIPUKO YA RISASI MWENYEWE…, MPAKA POLISI WANARUDI NA KURUSHA MABOMU KUNA ZAIDI YA DK. 5 NZIMA HAZIKUONYESHWA KUTOKANA NA KUZIMIKA KWA CAMERA NA HOFU YA MPIGA PICHA WETU KWA MAANA RISASI ZILIKUWA ZINAELEKEZWA UPANDE ALIPO KUWA.
 • HAYA NI MAISHA YA WATU YALIYO POTEA… PAMOJA NA WANAHABARI KUWA WAATHIRIKA NA KAZIA HII… TUNAOMBA SANA VYOMBO VINAVYO HUSIKA VIACHE KUTOA KAULI ZA DHIHAKA.
 • HAKUNA POLISI AU CHOMBO CHOCHOTE KILICHO TOA MSAADA KWA WAADHIRIKA BALI NI WANANCHI WENYEWE.
 • MPAKA MWISHO PAMJA NA WALINZI WA KAMANDA MBOWE KUMTAKA KUMUONDOA HENEO HILO ALIGOMA MPAKA MWISHO.
 • MWISHO TUNAWAPA POLE WALE WOTE WALIYO ATHIRIKA.

PUMZIKA KWA AMANI KAMANDA JUDY! DHURUMA DHIDI YAKO HAIWEZI KUPOTEA BURE

 • MAELFU WAMUAGA MPENDWA WAO….

 • AMANI NA UTULIVU VYATAWALA

 • WATU WAPUUZA TISHIO LA KUSHAMBULIWA, WAJITOKEZA KWA WINGI

Mkuu wa jimbo la Arusha magharibi na Mchungaji wa kanisa la KKKT, Mch Kisiri amesema kuwa anasikitika kwa Kifo cha Judith Moshi kilichokatizwa na watu/ mtu  alie waita Wanyama na Magaidi kwa kurusha Bomu katika mkutano wa CHADEMA.

Alisema kwamba Amani na utulivu tulionayo ipo mashakani kutoweka kwa ajili ya viongozi wanaoshindwa kusoma Alama za Nyakati huku wakiendeleza Porojo na Hadithi badala ya kujibu kero za wananch, Badala yake kutumia Risasi na mabomu kuwatisha wananchi.

Katika ibada hiyo ya mazishi ya Marehemu Judith Moshi aliwaambia watu waliojitokeza kwa wingi kanisani hapo wasife Moyo wala kuogopa maana Mungu yupo upande wao.

Aidha aliwaasa polisi kuwa njia ya kutumia risasi na mabomu kuwaua watu wanaodaiwa kuwa ni wakorofi sio suluhisho kwani wakiuwawa hawa wengine watainuka.

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

?????????????????????? ??????????????????????

??????????????????????

?????????????????????? ??????????????????????

?????????????????????? ??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????