MWILI WA MSANII ALBERT MANGWEAR KUWASILI JIJINI DAR LEO SAA NANE MCHANA.

Msanii Albert Mangwea enzi za uwahi wake

Msanii Albert Mangwea enzi za uwahi wake

Wapenzi na mashabiki wa msanii wa kizazi kipya aliyefariki majuzi marehemu  Albert  Mangwear jana jioni huko  Johannesburg, Afrika Kusini wakiwa katika harakati za kuusafirisha mwili wa msanii huyo. Ratiba zinaonesha mwili huo utawasili leo saa 8 mchana  jijini Dar es salaam.

Afisa Mwandamizi wa Vodacom Nchini Afrika ya kusini Bi Mwamvita Makamba, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu Albert Mangwea.

Baadhi ya watanzania waishio Afrika Kusini wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa  marehemu Albert Mangwea, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo, ambapo ilikuwa ni maalum kwa watanzania waishio nchini Afrika ya Kusini.

Advertisements