RASIMU YA KATIBA NA TANZANIA YETU YA KUKURUPUKA.

Rasimu ya Katiba mpya imetoka… Kunamazuri mengi tu lakini vile vile kunamambo ambayo yanaitaji majadiriano ya kina, chakushangaza viongozi wetu na baadhi ya watu ambao wameona kuna umate umate kwenye hili la serikali tatu tayari wameisha anza kuunda tume ya kutengeneza Katiba ya Bara (Tanganyika au Tanzania Bara).

  • Huu ni upuuzi mtupu! kwani hata rasimu hii ya katiba ambayo itapisha muundo huu wa serikali tatu bado haijapita. wamepata wapi uhuhalali wa Kuunda tume ya kutafuta maoni yakatiba ya Tanzania Bara?

  • Watanzania tumekuwa wavivu hata wa kusoma nasaa za wazee wetu… serikali tatu ni kuvunja muungano hitakuwa kama vile ilivyo kuwa urusi, Rejea maoni ya baba wa taifa wakati wa sakata la G5 bungeni. Nani amesema tatu ni karibu na moja? Lengo ni kuwa na serikali moja au ukiwa mbili unapitia tatu kwenda kwenye moja.

  • Na hili la wabunge wawiliwawili (jinsia Tofauti) ni kichekesho cha mwaka, Mbona kwa wenzetu waliotutangulia kwenye maswala ya demokrasia hatujawahi kusikia upuuzi huu? As a matter of fact ni kana kwamba hawajui hesabu za seti! Hivi Mbunge mwanamke atakuwa anawakilisha wanawake tu kwenye hilo jimbo na Mwanaume atawakilisha wanaume watupu?

Advertisements