SEMA “HAPANA SERIKALI 3”; NDIYO KWA SERIKALI MOJA – MWANAKIJIJI

Sema hapana Serikali “Tatu”, Sema ndiyo “Serikali moja”. Nchi moja, Taifa Moja, Watu wamoja – nje ya hapo Hapana!!! Tumeshatengeneza ulaji na ukiritimba wa kutosha kwenye serikali mbili halafu tunataka kuongeza serikali ya tatu? Mizigo miwili midogo imetushinda (tunahangaika nayo) halafu magenius wetu wanataka kutupa mizigo mitatu mikubwa!? Kwanini tusiamue kutengeneza mzigo mmoja tu tukaubeba!?

Pamoja na jaribio dhaifu la Tume ya Warioba kupendekeza kuikataa majimbo, pendekezo lao la Katiba Mpya kimsingi linatengeneza majimbo yale yale (States) ambapo kutakuwa na majimbo mawili – Tanganyika na Zanzibar! Kwa sababu kama nchi mbili zimeungana na kuunda ‘Shirikisho” basi zile zilizoungana haziwezi kuendelea kuwa nchi tena; zinahamisha hakimiya (sovereignty) yake kwenda kwenye federal government isipokuwa kama kilichoundwa (Shirikisho) siyo nchi!

Kwa kuanzisha mfumo wa Majimbo – Jimbo la Tanganyika litakuwa na nguvu kubwa sana kuliko jimbo la Zanzibar. Lakini kama wakiamua kufanya hali ya sawa katika kuendesha serikali ya Jamhuri ya Muungano Zanzibar itaonewa kwani ikitakiwa kuchangia nusu ya gharama za kuiendesha serikali ya Muungano italalamika mno na sidhani kama Wazanzibari watatakiwa kukubali mfumo huo.

Kwa sababu hiyo njia ya kuimarisha “Muungano” kama lengo ndio hilo basi ni kuingia Serikali Moja ya Kitaifa na Nchi Moja – siyo serikali tatu za kitaifa. Chini ya serikali hiyo moja ya kitaifa (federal government) kutakuwa na serikali za Majimbo (States) ambapo Zanzibar itabakia kama ilivyo (Visiwa vya Mafia, Bagamoyo, Pangani vinaweza kuongezwa huko… I know.. I know.. au ikagawanywa Unguja ikawa kivyake na Pemba kivyake!.) halafu Tanganyika igawanywe kwa States saba hivi ambazo zitaunda ‘Regional Governments). Chini ya Regional Governments kutakuwa na “Local Governments” za Miji, Majiji, Vijiji na mifumo mingine ya kujitegemea.

Na maneno mengine mengi….

In short.. Tusikubali serikali tatu za nchi; bali serikali moja, nchi moja, taifa moja na watu wamoja.. Mapendekezo ya Tume ya Warioba kuwabebesha Watanzania mizigo hii ni ya kupingwa, kukataliwa na kupuuzwa.

SOURCE:- jamiiforums.com
Advertisements