SAFARI YA MWISHO YA MANGWEA LEO MOROGORO, JANA MAELFU YAMSINDIKIZA DAR.

Mamia ya Wakazi wa jiji walijitokeza kumuaga Msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya aliyefariki Mei 28, mwaka huu Nchini Afrika Kusini alikokuwa kwa shughuli za kimuziki. 

Mangwea alisafirishwa mchana wa June 5, 2013 kwenda Kihonda mkoani Morogoro kwa mazishi yatakayo fanyika leo June 6.

 
 
 
 Wanafamilia wakipita kuaga mwili wa ndugu yao….
  Mbunge wa kinondoni  Idd Azzan anamuaga Ngwea
  P. Funky akipita kuaga na kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la Mangwea
 Wasanii wa Bongo Movie wakipita kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa marehemu
Hata wanahabari nao kama Issa Mnali walitoa heshima za mwisho.

 Miraji Kikwete akizungumza machache na Ummy Wenselaus ‘Dokii’ viwanja vya Lidaz
  Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuaga mwili wa marehemu Mangwea
   Sehemu ya waombolezaji waliokwenda kumuaga marehemu Ngwea wakionekana katika viwanja vya Leaders Club leo.
  Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Taifa Chadema (BAVICHA), John Heche wa tatu kutoka kushoto akijadiliana na viongozi wenzake waliokwenda kuaga mwili wa marehemu Albert Mangwea leo viwanja vya Leaders Club leo.
Kamati ya Maandalizi ya Mazishi ya Ngwair ikiwa jukwaani.
Gari ya polisi ikiongoza msafara wa magari mengine kuelekea mkoani moogoro muda mfupi baaada ya mamia ya mashabiki na wananchi wa jiji la Dar es Salaam na Vitongoji vyake kutoa heshima za Mwisho kwa mwili wa msaniii mashukuri nchini albert Mangwe.Picha Zote na Mdau, Muhidini Sufiani, Mroki Mroki na Mdau Kambi Mbwana
Advertisements

One thought on “SAFARI YA MWISHO YA MANGWEA LEO MOROGORO, JANA MAELFU YAMSINDIKIZA DAR.

Comments are closed.