KAULI YA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KWA WAZIRI WILLIAM LUKUVI NA HALI YA USALAMA MKOANI ARUSHA TAREHE 19 JUNI 2013

Tanzania

Mtandao wa Wateteziwa Hakiza Binadamu unaounganisha asasi za kiraia zinazotetea haki za binadamu zaidi ya mia moja, pamoja na mashirika wananchama Mkoani Arusha, tumesikitishwa na kushtushwa sana na kauli iliyotolewana Waziriwa Nchi, Ofisiya Waziri Mkuu (Sera, Uratibuna Bunge) William Lukuvi dhidi ya asasi zakiraia.

Katika kauli yake Bungeni tarehe 17 mwezi Juni, akizungumzia tukio la bomu dhidi ya wafuasi wa Chama cha Demokrasiana Maendeleo (CHADEMA), Lukuvi ameendeleza kile ambacho kwa muda mrefu serikalii liyopomadarakani imekuwa ikikifanya yaani kutumia lugha mbaya za kuwachonganisha wateteziwa hakizabinadamu na asasiza kiraia kwa ujumla na kuwaita kwamba ni wachochezi, vibaraka wa upinzani na lugha nyingine zenye dhihaka.

Katika siku za karibuni, zimekuwepo jitihada za makusudi za baadhi ya vyama vya siasa, makundi ya kijamii na watu binafsi kupandikiza chuki kwa raia dhidi ya vijana wetu wa Jeshi la Polisi, kuwafanya raia wawachukie askari, kuwafanya raia wasiwaamini askari, kuwafanya raia wasiwape ushirikiano askari na hatimaye kuwa na taifa ambalo halitawaliki,” alisema Lukuvi

Kauli kama hii kutolewa kiongozi mkubwa wa serikali tena katika Bunge la Tanzania ni kejeli kwa waliopoteza ndugu zao Mjini Arusha, na ni kauli ya vitisho dhidi ya asasi zisizo za kiserikali nchini. Nchi yetu imekumbwa na kasumba ya viongozi kuacha kutatua dalili zinazoashiria upotevu wa amani na kutaka kuonyesha kuwa asasi za kiraia na makundi mengine ndio chanzo cha matatizo hayo. Kauli kama za Mh Lukuvi zimeshatolewa ndani ya miezi sita iliyopita na mawaziri na viongozi wenginewasiopungua watano. Waziri Kagasheki alizishutumu wazi wazi asasi za kirahia zinazotetea haki za wafugaji Loliondo kuwa ni wachochezi wa mgogoro huo, wakati huo huo Naibu waziri wa Ardhi aliendeleza shutuma na vitisho hivyo dhidi ya Asasi zinazotetea rasimali ardhi nchini. Tunamsihi Lukuvi, atambue kuwa imani ya wananchi dhidi ya jeshi la polisi nchini haijawahi kuondolewa na asasi za kiraia, bali huondolewa na matendo ya kidhalimu ya jeshi hilo dhidi ya wanachi na vyama vyao. Jeshi la polisi litaweza kurudisha imani kwa wananchi endapo tu litaacha kutumika na watawala kwa maslahi binafsi na kisiasa na sio kwa kauli za kubeza zitolewayo na viongozi wa serikali dhidi ya asasi za kiraia na makundi mengine. Itakumbukwa kwamba hivi karibuni katika uchaguzi wandani wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. JakayaKikwete, aliwatahadhrisha wana –CCM wasiendelee kulitegemea Jeshi la Polisi kamanguzo yake kisiasa. Viongozi waache mzaha katika hali ya usalama wa Taifa kwa sasa kwani hakuna anaependa amani ya Taifa itoweke. Hadi sasa matukio ya kutishia amani ya Nchi yamekuwa yakishika kasi bila kuona jitihada za makusudi za kukomesha hali hiyo. Toka kushambuliwa kwa wahariri Saed Kubeneana Ndimara Tegambwage, kutekwa na kuteswa kwa Dk. Stephen Ulimboka, kuuwa kwa Mwangosi, Mwenyekitiwa Jukwa la Wahariri Absalom Kibanda, kuuwa kwa mapadre na mashekh, mlipuko wa Olasit dhidi ya waumini wa Kanisa katoliki, migogoro ya kidini na mengineyo, hakuna hata limoja lillilopatiwa ufumbuzi wa kudumu. USALAMA WA WAANDISHI WA HABARI

Mtandao pia unalaani kitendo cha Jeshi la Polisi kuwanyima uhuru waandishi wa habari, na kuwafukuza waandishi wa habari katika mikusanyiko ya mjini Arusha.Mtandao unalisihi jeshi la Polisi kumwachia mwandishi wa Chanel Ten Ashiraf Bakari, aliyekamatwa tarehe 18/6/2013 katika eneo la Soweto alipokuwa akichukua picha za matukio ya jeshi la polisi dhidi ya raia waliopiga kambi katika viwanja. Tunaalani kitendo cha jeshi la polisi kumkamata bwana Ashirafu aliekuwa na vitendea kazi pamoja na kitambulisho chake cha uandishi wa habari.

WITO WETU

  1. Tunamsihi Waziri Lukuvi aifute kauli yake dhidi ya asasi za kirai aambazo kimsingi kwamujibu wa utendaji kazi zao ni Watetezi wa Hakiza Binadamu katika fani mbalimbali na hawahusiki kwa namna yoyote ile katika hali ya sasa ya uvunjufu wa amani unaondelea nchini.

  2. Aidha tunaomba asasi kwa upande wao zisijihusishe naitikadi yoyote ya kisiasa baliwaendelee kuwatumikia Watanzania waitikadizote bilaubaguzi wowote.

  3. Jeshi la polisi mkoani Arusha limwachie mwandishi wa chanel Ten bwana Ashiraf Bakari, na kuwapa uhuru waandishi kureport habari yoyote.

  4. Viongozi wote wakiwemo wa madhebu mabalimbali walaani vikali hali inaoyoendelea Arusha kwa sasa.

  5. Balozi mbalimbali na Mashirika mbalimbali kukemea hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea Mjini Arusha.

  6. Viongozi watambue kazi za asasi za kirai na kuzieshimu na kuacha kuwaita wachochezi

Tarehe, 19/06/2013

Advertisements

One thought on “KAULI YA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KWA WAZIRI WILLIAM LUKUVI NA HALI YA USALAMA MKOANI ARUSHA TAREHE 19 JUNI 2013

Comments are closed.