CCM UK WATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA SHAMBULIA LA BOMU NA RISASI KWENYE MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA.

Chama Cha Mapinduzi Logo 86318

Chama cha mapinduzi Tawi la Uingereza kwa masikitiko makubwa tunapinga vikali tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa hadhara wa chadema uliofanyika jijini Arusha hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu watatu na zaidi ya watu 40 kujeruhiwa.

Tunatoa pole zetu za dhati kwa familia za wafiwa na kwa wale wote waliojeruhiwa katika janga hili la kikatili na kuwatakia uponaji wa haraka.

Tukio hili limefuata badala ya lile la awali lililotokea katika kanisa katoliki la mtakatifu Joseph mnamo tarehe 5 mei mwaka huu jijini Arusha, ambapo pia lilisababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi zaidi ya watu 60.

Ni imani yetu kwamba uchunguzi kamili wa mashambulio haya utakamilika haraka na wahusika watakamatwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria.

Tanzania ni nchi yenye hazina ya amani ya muda mrefu. Vitendo vya kigaidi vya aina hii na ambavyo vina mlengo wa kutugawanya kamwe havitavumiliwa na vikomeshwe ili kuondoa wimbi la vurugu zinazoweza kusababisha uvunjikaji wa amani.

Tunawasihi Watanzania wote tuwe pamoja na wenye busara na kuondokana na itikadi zozote za kisiasa au ushabiki wa vikundi , aidha na maneno ya kujibizana pasipo sababu. Ili kuondoa ama kutoamsha hisia za chuki zisizo na manufaa kwa yeyote yule na Taifa kwa ujumla , ni vyema wakati wa majanga kama haya kuachia vyombo vya usalama kufanya kazi yake ya uchunguzi bila kuingiliwa na vyama au kundi lolote kwa maslahi binafsi au umaarufu wa kisiasa .

Tunawasihi WaTanzania tuienzi amani yetu iliyolelewa kwa kipindi kirefu na Waasisi wa Taifa letu wakiongozwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Amani ambayo ni mfano na hadaa kwa wapenda amani kote ulimwenguni.

Imetolewa na idara ya Itikadi Siasa na Uenezi

CCM UINGEREZA – UK.

Advertisements

One thought on “CCM UK WATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA SHAMBULIA LA BOMU NA RISASI KWENYE MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA.

  1. how about getting a Polaroid crmaea and having your guests take pictures of themselves. then paste it to a page of a book and write a note around it. its like a guest book and a photo album.

Comments are closed.