BREAKING NEWS:- SUGU AMEKAMATWA

m2s breaking news

Habari zilizotufikia hivi punde zinadai  Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi amekamatwa kwa kile kinachoitwa uchochezi na kumkashifu Waziri Mkuu Mzengo Pinda.

habari kamili kuwajia hivi punde.

update:- ametolewa nje kwa dhamana

Quote By Godbless Lema
Ninasikitika na Jeshi la Polisi kumkamata Sugu na kumhoji juu ya kauli yake kuwa Waziri Mkuu ni Mpumbavu kwa maana ya maneno aliyosema Waziri Mkuu Bungeni juu ya kuruhusu Polisi kushambulia raia.Napenda kusisitiza kuwa alichosema Sugu sio matusi bali ni sifa kwa Waziri Mkuu juu ya kauli yake ya kinyama aliyotoa Bungeni.

Sugu, uko sawa na Mungu anatambua hilo.

Lema

Advertisements

BREAKING NEWS: SASA UCHAGUZI WA MADIWANI ARUSHA MPAKA 14/07/2013

m2s breaking news

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi muda huu ametangaza kuahirishwa kwa uchaguzi wa Udiwani katika kata za Elerai, Themi, Kaloleni na kimandolu Manispaa ya Arusha hadi tarehe 14/7/2013. Amesema sababu kuu ni hali ya amani bado sio nzuri ya kuruhusu uchaguzi kufanyika kwa sasa. Itakumbukwa kuwa Uchaguzi wa Kata Hizi ambao ulikuwa ufanyike tarehe 16/6 uliahirishwa hadi tarehe 30/6 kutokana na mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kufunga kampeni wa CHADEMA. Kampeni hazitakuwepo kwa kipindi hiki hadi tarehe ya Uchaguzi.

Habari kamili kufuata baada ya muda mfupi.

KAMA UKUBALIANI NA KAULI YA PINDA KUHUSU KUPIGA RAIA SAINI HAPA

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA

Wito ni kuwataka wananchi wa Tanzania waandike na kuweka saini kumtaka mheshimiwa waziri mkuu kufuta kauli yake inayoruhusu polisi kupiga raia katika hotuba yake ya kufunga Bunge la bajeti tarehe 27 Juni 2013.

Naomba tufuate hii link hapa chini na ku-saini

Wito kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania