BREAKING NEWS: YA MTWARA SASA YAHAMIA MGODI WA DHAHABU BULYANHULU – KAKOLA NI MWENDO WA MAWE NA RISASI TU…

  • WASUKUMA WAACHANA NA MSEMO WAO WA NDUHU TABU YANI HAKUNA SHIDA WANAPAMBANA NA POLISI.

  • MADAI YAO NI KUPEWA ARDHI YA KUCHIMBA; INADAIWA JANA POLISI WALITEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA KUWAPIGA WAKOLOFI NA KUSABABISHA KIFO CHA MCHIMBAJI MMOJA MDOGO.

  • POLISI WA KITUO CHA BUGARAMA WAZIDIWA SASA WAOMBA MSAADA KUTOKA KAHAMA NA KAKOLA.

Hali ni ya wasiwasi mpaka dakika hii mgodini wa dhahabu wa Bulyanhulu na maeneo ya jirani huku barabara kuu ya kuingia mgodini ikiwa imefungwa na wananchi  kwa kutumia mawe na magogo wakidai na wao wapewe sehemu ya kuchimba kandokando ya mgodi wa Bulyanhulu ili nao waweze kujikimu kimaisha.

Hakuna kuingia wala kutoka, Hakuna gari wala bodaboda. Ni mwendo wa mabomu ya machozi tu ndiyo yanayoendelea kulindima mpaka sasa katika kijiji cha Kakola.

Hali hii imeanza kuanzia saa kumi jioni kabla ya shift ya mchana. Kwa ujumla wafanyakazi wa shift ya usiku hawakuingia na waliokuwa kazini wanajaribu kutafuta mbadala wa kufika makwao.

Habari za sasa hivi zinasema jeshi la polisi kituo cha Bugarama limeomba nguvu kutoka Kahama na Shinyanga kwani vurugu ni kubwa sana kiasi cha kulazimu polisi kutumia risasi za moto.

Hakuna maongezi zaidi ya mawe na risasi. Ila inavyoonekana polisi ni wachache na raia ni wengi isitoshe giza nalo limeingia hivyo hali inazidi kuwa si salama tena.

Inadaiwa jana polisi waliuwa mchimbaji mdogo mmoja aliyekuwa anachimba pamoja na wenzake nje ya fensi ya mgodi, jambo ambalo limepelekea asira miongoni mwa wananchi hasa wale wa asili ya Wasukuma na sasa wamejitutumua! Ule msemo wao wa ‘nduhu taabu’ yaani hakuna shida umekwisha. Uvumilivu wa kuona zao zinaondoka bila kimegewa umefikia mwisho. Wanaambulia vumbi tu.

Ikumbukwe kuwa eneo hilo linalodaiwa na wananchi waliwahi kulichimba yapata miezi kama 5 iliyopita kabla mamlaka ya mgodi wa Barrick kuwafukuza. Mamia kama si maelfu ya polisi nao wako njiani kutoka wilayani na makao makuu ya mkoa usiku huu kuja kurejesha utulivu.

kwa taarifa kamili endelea kutembelea blog yako.

Advertisements