AFRIKA KUSINI HAIJAWA MTELEMKO KWA BARACK OBAMA

Baadhi ya wachambuzi kisiasa nchini Afrika Kusini na wamemtuhumu Barack Obama kuto toa mchango wa kutosha kwa ajili ya bara la Afrika, ingawa baba yake ni mkenya.

Baadhi ya wachambuzi wa kisiasa nchini Afrika Kusini wamemtuhumu Barack Obama kwa kuto toa mchango wa kutosha kwa ajili ya bara la Afrika, ingawa baba yake ni mkenya.

Ziara ya rais mweusi wa kwanza wa Marekani kwenye mji mdogo wa Soweto Afrika Kusini, mji ambao ulikuwa chachu ya mapambano dhidi ya utawala wa wazungu wachache, imepokewa kwa hisia tofauti huku ikitarajiwa kuwa swala na tukio la kihistoria lenye kuvutia umati mkubwa wa watu.

Badala yake Barack Obama alilakiwa na kundi dogo la watu huku wakosoaji wake wakijikusanya kwa maadamano ya kupinga sera za kigeni za Marekani.

Obama aliepushwa na kadhia hiyo, huku yeye mwenyewe asijuwe kile kilichojili kutokana na kazi kubwa iliyo

Polisi wakipika risasi na mabomu ya tahadhari wakati wa maandamano nje ya Chuo Kikuu cha Soweto jijini Johannesburg chuo ambacho Rais Obama alikuwa anakitembelea

Polisi wakipiga risasi na mabomu ya tahadhari wakati wa kutawanya maandamano nje ya Chuo Kikuu cha Soweto jijini Johannesburg chuo ambacho Rais Obama alikuwa anakitembelea

fanywa na polisi wa Afrika Kusini walio lazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji muda mchache kabla ya msafara wake kupita kuelekea katika Chuo Kikuu cha Johannesburg, ambapo uliofanyika mkutano pamoja na maswali na majibu kutoka kwa watazamaji wa bara zima la Afrika.

Moja ya sababu ya kuchukulia ugeni huu kuwa wa kawaida, imeelezwa ni kukosa msisimko baada ya kutopata manufaha kutoka kwa  huyo kiongozi mweusi wa White House.

Kijana mmoja wa Afrika Kusini aliniambia alifanya sherehe wakati Obama alipochaguliwa kwa mara ya kwanza lakini, “sasa tumeona kwamba hakuna tofauti kati yake na marais walio mtangulia wa Marekani“.

Miongoni mwa watu wachache ambao walijitokeza kumlaki Obama lakini hawakuridhika ni pamoja na mfanyabiashara Alex Motloung, 40.

Motloung alisubiri kwa zaidi ya lisaa limoja ili kumuona rais wa Marekani akipita mitaa ya Pimmville Soweto kama ilivyokuwa imepangwaya bila kukata tamaa, ingawa, kama ilivyo pangwa msafara wa rais ulipita ila magari yalikuwa kwenye mwendo kasi wa zaidi ya km 140 kwa saa hivyo kumfanya ashindwe kumuona habiria yoyote ndani ya magari hayo.

Awali katika mkutano wa pamoja na wanahabari viongozi hao wawili Obama wa Marekani na mwenyeji wake Rais Zuma ambaye alimliganisha Obama na Nelson Mandela, ambaye kwa sasa ni mgonjwa huku swala la afya yake ikigonga  mawazo ya wananchi wote wa Afrika Kusini bila jawabu.

Zuma alibainisha kuwa wote walikuwa ni marais wa kwanza weusi wa nchi zao, na hivyo kuchochea “ndoto ya mamilioni ya watu wenye asili ya Afrika na Waafrika wanaoishi nje, ambao hapo awali walidhulumiwa“.

Motloung kwa kufuata ulinganifu huu yeye alisema ni yamkini Obama alikuwa na mafanikio ya kuvutia zaidi kuliko Madiba (Mandela).

“Obama amefanya kile ambacho kina onyesha kwamba hakuna lisilowezekana” – hata nchi yenye  idadi kubwa ya watu weupe wanaweza kupiga kura kwa ajili ya mtu mweusi.

“Hii ndiyo tunataka Afrika Kusini, pale watu wanavyo weza kumuukumu mtu juu ya uwezo wake na si rangi ya ngozi, na hii ndiyo ndoto ya Madiba.”

Msisimko wa ziara ya rais Obama ulikuwa mdogo mahali pengine katika vitogoji vya Pimmville, kwa mfano maeneo kama ya Small  Kopie  (hill) karibu kabisa na  chuo kikuu ambacho ilifanya mkutano, wananchi waliendelea na shuguli zao kama kawaida.

Wanandoa walionekana wakiwa wamejilaza kwenye jua nyakati za alasiri ikiwa ni njia ya kupambana na baridi kali nyakati za usiku ambayo ni kawaida ya maeneo haya ususan nyakati hizi za majira ya baridi, makundi ya vijana walionekana kwenye migahawa wakinywa wengine kwenye vijiwe vya vinyozi.

Baadhi ya vijana wa Kiafrika walioalikwa kushiriki katika Mr Obama mkutano "ukumbi wa mji" walikuwa msisimko kuwa kuna

Baadhi ya vijana wa Kiafrika walioalikwa kushiriki kwenye mkutano na Obama “ukumbi wa Town Hall”.

Ntuthuko NzimandeDlamini, (24), mwanafunzi wa sheria alisema kwa hali yoyote ile uwezi kumliganisha Obama na  Mandela, ambaye alitumia miaka 27 jela kwa kupinga utawala wa wazungu wachache.

Lerato Mahasha kwa upande wake alisema yeye alifurahia ujio wa ziara ya rais wa Marekani lakini amekelwa na hatua za usalama, ambazo zimepelekea barabara na chuo kikuu karibu chote kufungwa.

Wakati Rais Zuma alianza kutoa maoni yake kwa kumsifu Obama, yeye pia akumungunya maneno pale  alipo weka hadharani ubabe wa sera za kigeni za nchi hiyo kubwa duniani.

Alibainisha kwamba ongezeko la wanamgambo wa Kiislam katika nchi jirani ya Mali na nchi za Afrika Magharibi ilikuwa ni matokeo ya kuanguka Kanali Gaddafi kutoka madarakani.

Advertisements