RAIS OBAMA AVUNJA UKIMYA NA KUSEMA SABABU ZA KUTOTEMBELEA KENYA

Barack na Michelle Obama walipo wasili katika jiji la Pretoria, South Africa jana

Barack na Michelle Obama walipo wasili katika jiji la Pretoria, South Africa jana

Barack Obama avunja ukimya na kusema kwanini alisisitiza kwa nini aliamua katika ziara yake ya pili ya Afrika kama Rais wa Marekani kutotembelea KENYA .

Alikuwa akijibu swali kutoka Kenya kwa njia ya tekhama ya mawasiliano, juu ya ahadi yake aliyoitoa kutembelea nchi ya baba yake wakati wa urais wake. Kauli hiyo alizungumza wakati akiwautubia vijana zahidi ya mia moja walio kuwa wamekusanyika katika kitongoji cha Soweto katika Chuo Kikuu cha Johannesburg Juni 29 2013.

“Mimi bado naendelea kuwa rais kwa miaka mitatu na nusu zaidi,” alisema alipoulizwa kupitia kiungo video kutoka Nairobi kwa nini hakupanga kutembelea nchi hiyo “. Nimeweza kujifunza kama rais kwamba watu si tu wanataka wewe kutimiza ahadi yako, lakini wanataka kutimiza ahadi yako jana. “

Lakini Obama alikiri kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ambayo bado inasikiliza kesi dhidi ya rais wa Kenya na makamu wake ni moja ya ushawishi wa uamuzi wake. “Mimi nafikiri si wakati muafaka wa kutembelea Kenya,” alisema lakini aliahidi bado anaweza kufanya safari ya kutembelea Kenya kabla ya wakati wake akiwa rais.

Mapema katika mkutano wake na wanahabari mjini Pretoria, Obama alisema akutembelea Kenya katika ziara yake kwa sababu ya migogoro ya kimataifa, ambao ni Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari kwa kumshtaki Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji, mateso na matendo ya kinyama yanayo daiwa kufanywa na wafuasi wake katika ghasia baada ya uchaguzi wa Kenya 2007.

Muda huu siyo muafaka kwangu kama rais wa Marekani kutembelea Kenya wakati masuala hayo bado hayaja patiwa ufumbuzi“.

Lakini alibainisha yeye alitembelea Kenya mara kadhaa hapo awali na anatarajia pia kutembelea katika siku zijazo.

Advertisements

2 thoughts on “RAIS OBAMA AVUNJA UKIMYA NA KUSEMA SABABU ZA KUTOTEMBELEA KENYA

Comments are closed.