JOURNALISTS URGED TO UPDATE ON OIL,GAS AND MINING ISSUES

Mr Amani Mustafa Mhinda, a lawyer & executive director of HakiMadini in Tanzania, during one of the sessions.

Mr Amani Mustafa Mhinda, a lawyer & executive director of HakiMadini in Tanzania, during one of the sessions.

Journalists in resource-rich countries in Africa have been asked to understand slangs of the industry to enrich their reportage and to protect the interest of their countries.

Various speakers at this year’s oil, gas and mining training for 30 journalists from Ghana, Uganda and Tanzania in Dar es Salaam stressed the need for editors and correspondents to be up-to-date with issues bordering on environment, social and human rights impacts of the extractive industries.

They said it was only when journalists show commitment and learn about the industry that they will be better positioned to question the operations of industry players.

The organizers, Thomson Reuters Foundation, PenPlusbytes, Africa Center for Media Excellence and Revenue Watch Institute, said the training was designed to introduce journalists to some of the critical issues on the exploitation, management, and utilization of oil, gas and mineral resources.

The Media Programme Officer of Revenue Watch, Mr. George Lugalambi, said with the emergence of hydrocarbons and other resources along the coasts and inland of African countries demands that journalists be equipped to do a good job.

The course therefore, he said “will reinforce the knowledge and skills of the journalists to stimulate and feed public debates on how best to ensure that the proceeds from these resources are used in the best interest of their respective countries citizenry.”

For his part, Mr. Nike Phythian of the Thomson Reuters Foundation took journalists through the fiscal system and how it was expected to capture all revenue that should come to the state in the form of corporate taxes, royalties, interests, bonuses and rents.

He said it was therefore very important that resource owners were made to control the income and expenditure of international oil companies who operate and exploited their natural resources to ensure that they did not overspend to eat into final profits.

Mr. Phythian said journalists should also concern themselves with the value of the resource produced in their countries, and demand clarification from the companies and governments sources to ensure transparency and accountability.

He said all resource rich countries in Africa had a right to use its oil for domestic purposes and even though it does not happen immediately, it was important for journalists to have the full understanding of issues on the domestic supply obligation.

“It was important to know about the rent or windfall profit, withholding taxes and other issues to help the journalist to write well,” he said.

Other trainers took journalists through various loopholes such as transfer pricing which at the end inflate prices at the expense of the resource owners. In Ghana it was estimated that about $36 million is lost every year through transfer pricing.

The participants were also taken though the various segments of the resource governance value chain – a decision to extract, extraction, value enhancement and most importantly, revenue management.


Picture & Story: By Moses Dotsey Aklobortu, Dar es Salaam, Tanzania

Advertisements

MTANGAZAJI WA REDIO 5 SEMIO ATUNUKIWA ZAWADI YA PIKIPIKI

 Mkurugenzi wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis (kulia) akimkabidhi Pikipiki Mfanyakazi Bora wa Kituo hicho Semiyo Sonyo.
Mkurugenzi wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis Amewataka watangazaji na wanahabari wanaofanya kazi katika vituo vya Radio na Televisheni hapa nchini kuzingatia weledi wa kitaaluma wanapofanya shughuli zao za kila siku ili kusaidia jamii ya kitanzania kukabiliana na changamoto katika kipindi hiki ambacho dunia inabebwa na utandawazi. 
 
Akikabidhi pikipiki kwa mtangazaji bora wa kipindi cha usiku cha LOVE CUTTS kinacho rushwa Radio 5 katika Hafla fupi iliyofanyika jijini Arusha, Mkurugenzi Robert amesema vyombo vya habari vya kielectonic yaani Televisheni,Radio, na mitandao ya kijamii vinafikia watu kwa haraka zaidi na kwa unafuu wa gharama kuliko machapisho na kwamba vikitumika bila miiko ,weledi na kuzingatia kanuni za kitaaluma vinaweza kuwa sehemu ya tatizo badala ya kuwa vyombo vya kusukuma kasi ya maendeleo.
 
Katika tafrija hiyo Mtangazaji Semio Sonyo amekabidhiwa pikipiki ikiwa ni sehemu ya motisha zinazo tolewa na kituo cha Radio five kwa wafanyakazi wake waofanya vizuri katika majukumu yao.

Semio Sonyo akijaribu pikipiki aliyokabidhiwa na mkurugenzi wa Tan Communication Media,bwana Robert Francis

BUYA KUWAKILISHA MKOA WA MANYARA MODO WA UTALII….SINGIDA ZAMU YENU SASA

MANYARA 2 PICS 252Kushoto Mkurugenzi wa Event Planners na muandaaji wa shindano la Modo wa Utalii Graysson Kijo a.k.a Chinaa akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa shindano hilo Bi.Buya Ernest(19) wa pili ni Simon na Jairos kutoka kampuni ya Megatrade Investment, wadhamini wakuu wa shindano hilo kupitia kinywaji chake cha K-vant gin lililofanyika mjini Babati

MANYARA 2 PICS 255Mkurugenzi Graysson Kijo akiwa na mshindi wa shindano hilo Buya Ernest mara baada ya kutangazwa mshindi wa modo wa utalii ambaye atawakilisha Mkoa wa Manyara

MANYARA 2 PICS 256Kulia ni mshindi wa pili katika shindano hilo Veronica Christopher(20),mkurukenzi wa Event Planners Graysson Kijo,Buya Ernest(19)mshindi wa shindano hilo

MANYARA 2 PICS 259

MANYARA 2 PICS 262

MANYARA 2 PICS 283Wafanyakazi wa Events Planner wakiwa katika pozi na mshindi Buya Ernrst atakaye wakilisha Mkoa wa Manyara

Manyara pics 013Jamaa akiwa anatoa vichekesho katika shindano hilo

NAMNA YA KUTUMIA WHATSAPP KWENYE COMPUTER YAKO.

Wengi wanalalama kuwa cm zao hazina whatsapp au wanashanga vipi mie napatikana kwenye hiyo mambo wakati na cm yangu ni ya Tochi tu.

Hebu cheki maelekezo  hapo chini ukimaliza kumbuka kuni Add na mimi ili tutumiane ma picha na mambo mengine….

Download App inaitwa Bluestack Kutoka hapa Run Mobile Apps on Windows PC or Mac with BlueStacks | Android App Player then Run Hyo app so Utakua na Access na Playstore so utaweza Kudownload App zote Ikiwemo Whatsapp Instagram, viber, tango, na nyingineee tu.

ila Hyo App Ni ina Mb 8 tu ila inahtaji Specs kubwaaa kwanza Ram Lazma Iwe 2gb Pia Graphic accelerator lazma ziwe Updated… So Kabla Ya Kudownload Na Kuinstall Fix Hzo kwanzaaa

Ukisha insall bluestack, ingia kwenye google play install go launcher ex, itaifanya hiyo bluestack iwe na mwonekano mzur wa android kama za cm, bt kunakua hakuna mwingiliano wwte kati ya pc na bluestack mfano ukitaka kutuma picha kwa kutumia watsapp na kama hiyo picha imo kwenye pc, inatakiwa ui install dropbox kwenye pc yako.

Kumbuka, youwave ni yakulipia (Ingawa unaweza kuichakachuwa) ila bluestack ni ya bure, isipokuwa ina ishu za ram, vga drivers etc ndo maana siipendi.

Later tukutane kwenye whatsapp….

VIDEO:- HATUTAPIGWA, HATUTALIA WALA KULALAMIKA TENA; CHADEMA

 • Wasema Watashinda Kwa Kishindo na kutaja asilimia.

 • Wamshanga Mwigulu Nchemba kwa siasa ambazo zinamuhusisha Mwenyekiti wa chama chake.

 • Wataja vikosi vyao vya kujilinda na kusema ndiyo mwisho wa kuonewa.

JESHI LA POLISI NA SERIKALI WAJIULIZE WAMETUFIKISHA VIPI HAPA?
Badala ya kuipiga mikwara CHADEMA na kuwatishia viongozi wake uongozi wa jeshi la polisi na Ikulu inapaswa wawe na ujasiri wa kusimama mbele ya vioo na kujiuliza maswali ambayo majibu yake yagonge visogo vyao. Maswali hayo baadhi yake ni haya:

 1. Kwanini CHADEMA imefikia mahali pa kutaka kujilinda?

 2. Vyombo vya usalama vimepungukiwa nini kiasi kwamba chama kikuu cha upinzani nchini haiviamini?

 3. Je, uongozi wa vyombo vya usalama una mahusiano gani ya kikazi na viongozi wa CHADEMA?

 4. Je, ni kwanini matukio yaliyotokea na kugusa CHADEMA hayachunguzwi kwa kasi ile ile kama matukio mengine – mfano mauaji ya Padre Mushi kule Zanzibar yamepewa uzito wa uchunguzi (Hadi Rais kaingilia kati) kuliko mauaji ya wanawake na mtoto mdogo Arusha?

 5. Je vyombo vya usalama vinaweza kuchukua hatua gani kurudisha imani ya CHADEMA na wanachama wake kuwa vinafanya kazi kwa weledi na siyo kama sasa ambavyo vimebatizwa majina ya CCM kama PoliCCM (badala ya Polisi), na TICCM (Badala ya TISS) n.k?

 6. Rais Kikwete ajiulize kwanini wale aliowakabidhi dhamana ya kusimamia usalama nchini wameifikisha nchi hapa – kuwalaumu CHADEMA kwa kujilinda ni kukosa umakini na kuwa na usahaulifu unaobagua (selective amnesia).

BY:- Mwanakijiji….

Haki ya kujilinda ni miongoni mwa haki za msingi kabisa za binadamu ambazo zinatokana na mtu kuwa binadamu na haziwezi kuondolewa au kufutwa na chombo chochote. Ni haki ambayo mwanadamu anayo kwa kuzaliwa kwake. Haki hii kwa kadiri tunavyokua tunaiacha kwenye vyombo mbalimbali lakini mwisho wa siku bado ni haki yetu ya msingi kama binadamu. Mwanadamu anaposhambuliwa ana haki ya kujikinga kukinga maisha yake na mali yake; na kama ni familia yake inashambuliwa ana haki ya kulinda familia yake. Huwezi kumwambia mtu kuwa akipigwa ainame na kukubali kipigo bila kujilinda.

Haki hii ni tofauti na haki ya kujitetea au kulipiza kisasi – japo ni haki zinazoendana pamoja katika ile haki ya msingi ya kutokudhulumiwa. Haki ya kujilinda ni haki ambayo mtu si lazima alipe kisasi lakini ni haki ya kuzuia kutendewa vibaya. Hii ndiyo sababu watu wamejenga kuta kwenye nyumba zao, wameweka vyombo vya ulinzi na kuajiri walinzi. Wote hawa wanatumia haki yao ya kujilinda bila kulazimika kulipa kisasi. CHADEMA kama chama cha siasa ambacho tayari kimeshadhurika mara kadhaa sasa na kwa niaba ya wanachama wake kimeamua kutoa mafunzo ya ukakamavu na kujilinda; wanatumia haki hii ya msingi.

Jeshi la Polisi na vyombo vya usalama na wale wote wanaobeza wanahitaji kutafakari upya kama wao wangekuwa upande wa pili kama wasingetafuta mbinu ya kujilinda. Kama wale watu waliowekwa kutoa ulinzi ndio hao hao wanaoharibu ulinzi utakuwa ni ujinga wa hali ya juu kuwategemea. Bila mabadiliko ya msingi ya mfumo na utendaji wa jeshi la polisi katika mazingira ya vyama vingi vya siasa ni vigumu kwa chama cha upinzani kama CHADEMA kuweka maisha yake na maisha ya viongozi wake mikononi mwa chombo hicho. Ni wajibu na ni haki kwa wao kufikiri namna ya kujilinda na kulinda maslahi yake. Hili halihitaji baraka kutoka CCM, Ikulu, au Polisi.

MODO WA UTALII APATIKANA ARUSHA ZOEZI LAENDELEA KATIKA MIKOA MINGINE SASA NI ZAMU YA MANYARA JUMAPILI HII

DSC_8823Mratibu wa Mashindano ya Model of Tourism , Samuel akisoma taarifa fupi ya mashindao hayo kabla ya uzinduzi

DSC_8829Majaji wakifatilia shindano

DSC_8859Mama Doroth Massawe, Mkuu wa idara ya utalii, kanda ya kaskazini, wizara ya mali asili na utalii akitoa risala zake wakatiwa uzinduzi wa mashindano ya model of tourism 2013 katika ukumbi wa blue fame Triple ‘A Arusha

DSC_8886Mgeni rasmi  Samuel Diah akihutubia wageni mbalimbali

DSC_8909Mgeni rasmi katika shindano hilo Samuel  Diah ambaye ni Mkurugenzi wa bodi ya Utalii Tanzania akizindua rasmi shindano hilo pembeni yake ni Mama Doroth Massawe, Mkuu wa idara ya utalii, kanda ya kaskazini, wizara ya mali asili na utalii

DSC_8915 Washiriki nao wakapanda jukwaani na kutoa burudani ya aina yake

DSC_9024

Modo wa kiume Abubakari Hillal akionyesha vazi lake  la asili wakati wa uzinduzi wa model of Tourism 2013

DSC_9044Modo wa kiume wakionyesha vazi la asili jukwaani

DSC_9289Mshiriki wa Modo wa Utalii kwa  (Matha Charles) akisindikizwa na Modo wa kiume (Kenny Wilberd) wakati wakionyesha vazi la jioni kwenye uzinduzi uliofanyka katika ukumbi wa blue fame Triple A jijini hapa

DSC_9304

Washiriki wa Modo wa utalii wakiwa katika vazi la jion

DSC_9467Mshindi akiwa katika pozi

DSC_9475Mshindi wa Model of Tourism Arusha 2013, akiwa  na uso wa furaha mara baada ya kushinda kwenye mashindano na kuvishwa taji la kuwakilisha mkoa wa Arusha kwenye fainali itakayoshirikisha washiriki wengine kutoka mikoa 20 ya Tanzania,pembeni ni Afisa masoko wa kampuni ya Megatrade Bw.Goodluck Kwayu ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano hilo wakiwa katika picha ya pamoja

I will Just Wait For You At the Right Place And I will Hit You, Rwandan General Paul Kagame Threatens Tanzanian Jakaya Kikwete

“Those people [Tanzanian President Jakaya Kikwete] you just heard siding with Interahamwe and FDLR  and urging negotiations… negotiations?  Me, I do not even discuss this topic, because I will just wait for you [Tanzanian President Jakaya Kikwete] at the right place and I will hit you! He[Tanzanian President Jakaya Kikwete]  did not deserve my answer. I did not waste my time answering him…It is well known. There is a line you cannot cross, there is a line, a line that you should never cross. It is impossible…”

It is in these ominous terms that the Rwandan dictator General Paul Kagame threatened to get even with Tanzanian President Jakaya Kikwete, while addressing Rwandan Youth on June 30, 2013 during a summit called “Youth Konnect”“, sponsored by his wife, Janet Kagame.

Relations between Tanzanian President Jakaya Kikwete and Rwandan leaders have soured in the last weeks. On several occasions Rwandan leaders called the Tanzanian President “a genocide and terrorist sympathizer”, “ignorant”, “arrogant”, and “mediocre leader”. The relations have deteriorated following the recommendation by President Jakaya Kikwete of open negotiations between Rwandan, Ugandan and Congolese leaders and their respective armed opposition in order to bring durable peace and security  in the African Great Lakes region.

First the Rwandan Foreign Affairs Minister Louise Mushikiwabo and Defense Minister, James Kabarebe, publicly cursed the Tanzanian President and called him a sympathizer of “genocidaires”,  a “genocide denier”, and other names.

Then, General Paul Kagame, while addressing a closed door meeting with his close aides, called the Tanzanian President “4Bs”, which in Rwandan language means “an opportunist, attention seeker, arrogant and contemptible person.”

Then the Rwandan puppet Hutu Prime  minister Prime Minister  called the Tanzanian President a mediocre leader .

The latest public threats by  General Paul Kagame against the physical person of the Tanzanian President are arguably the most serious sign of how worse the relations among the two countries and the their leaders have become. According to sources in Kigali, General Kagame has also been frustrated by the attention Tanzanian President has been receiving from World powers. Until a few years ago, Rwanda and its dictator was the darling of the West. The attention from the West has since dwindled.

The recent visit by US President Barack Obama to Tanzania may have further increased the frustration and perhaps led to the grave public threats by General Paul Kagame against the Tanzanian President Jakaya Kikwete.

The upcoming days and months promise to be full of anticipation and sursprises in the Great Lakes Region of Africa.

Source :-  AfroAmerica Network.

KI CHUPA KIPYA CHA JUMA KASSIM NATURE FT TUNDA MAN “HAIPOTEI”

Kichupa hiki cha mtunzi, muimbaji na kwasasa mtayalishaji Juma Kassim Mohamed Kiroboto ambacho amemshirikisha Tunda Man Rais wa manzese, kilitufikia Mei 28 2013.

Kichupa ni chakawaida sana ambacho kimenakshiwa na ufundi wa kugani wa wakongwe hao. Kilicho wazi ni kwamba kama kuna walio fikiri Sir Nature amepote au atapotezwa hivi karibuni… jibu liko wazi “HAIPOTEI”

Juma Nature au Sir Nature (amezaliwa mwaka 1980 Jina kamili akijulikana kama  Juma Kassim Mohamed Kiroboto jijini Dar es Salaam) ni mwanamuziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Flava kutoka nchi ya Tanzania. Pia ni muanzilishi wa kundi la Tmk Wanaume.

Nature ni msanii mbunifu katika wa Bongo Flava na Hip Hop ya kiTanzania. Sio mtunzi tu pia ana kipaji na kujaliwa sauti nzuri ya uimbaji. Sababu nyingine zipelekeazo muziki wa Juma Nature kupendwe Afrika Mashariki ni mashairi anayotunga.

Albamu Alizotoa

 • Nini Chanzo (2001)

 • Ugali (2003)

 • Ubinadamu-Kazi (2005)

 • Zote History (2006)

WALAUMUNI WABUNGE WENU KWA TOZO LA 1,000/= KWA KILA LAINI.

Haya ndiyo majibu ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba alipokuwa akijibu maswali katika mtandao wa Twitter kuhusu kodi mpya ya TZS 1000 kwa mwezi kwa kila line ya simu.

 • Amesema kwamba Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia iliipinga kodi hiyo.

 • Amesema kwamba Hazina (Wizara ya Fedha) walikubaliana na maoni ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kuhusu kodi hiyo.

 • Amesema kwamba Bunge ndilo lililopitisha kodi hiyo na si Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

makamba twita

CHADEMA WASUSA KONGAMANO LA AMANI TCD

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

chademaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Ndugu waandishi wa habari, Tumewaiteni hapa mchana huu kwa dharura, kutokana na kujitokeza kwa jambo moja muhimu sana katika mustakabali wa chama chetu na taifa kwa ujumla. Jambo lenyewe ni hili:

Kwa muda wa siku mbili, kuanzia kesho– tarehe 9 Julai 2013 hadi 10 Julai – kutakuwa na “KONGAMANO LA AMANI” lililoitishwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania – Tanzania Center For Democracy (TCD).

Kongamano hilo litajadili na kutafakari Amani ya Taifa, litafanyika kwenye hoteli ya White Sands ya jijini Dar es Salaam. Litafuguliwa na Mwenyekiti wa TCD, Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Mheshimiwa James Mbatia na litafungwa na Rais Jakaya Kikwete.

Baadhi ya washiriki, ni pamoja na mawaziri, viongozi wakuu wa vyama vyenye wabunge ambavyo ni wanachama wa TCD – Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), United Democracy Party (UDP), Tanzania Lebour Party (TLP), NCCR- Mageuzi na CHADEMA.

Aidha, chama cha UPDP nacho kitashiriki mkutano huo kwa niaba ya vyama vingine ambavyo havina wabunge.

Ndugu waandishi wa habari,
CHADEMA kikiwa mmoja wa wadau wakubwa wa TCD, kimepokea mwaliko wa mkutano huo. Hata hivyo, tunapenda kutumia nafasi hii, kupitia kwenu, kuutangazia umma na Watanzania wote wanaotutakia mema na kulitakia mema taifa hili, kwamba hatutashiriki mkutano huo kwa sababu zifuatazo:

Kwanza, Mwenyekiti wa TCD, Mheshimiwa Mbatia kwa makusudi amekiuka maazimio ya kikao ya kuteuwa Mwezeshaji wa mkutano huo na badala yake akafungamana na CCM kuteuwa watu wanaowataka wao.

Pili, Chadema haitashiriki mkutano huo kwa kuwa Amani haijadiliwi. Amani inatengenezwa na kuwapo kwa mazingira ya haki na usawa; na kwamba aliyebobea katika uvunjaji wa haki hizo, ni serikali yenyewe.

Katika mazingira haya, CHADEMA inaona hakuna umuhimu wa kushiriki kwenye mkutano ambao washiriki ni wale wale wanaotuhumiwa kuvunja haki za binadamu.

Tatu, Amani siyo ya vyama vya siasa pekee yake. Amani inahusisha wadau mbalimbali wakiwamo viongozi wa kidini, taasisi za kiraia na mashirika yasiokuwa ya kiserikali. Taarifa zilizopo, ni kwamba mkutano huu haukushirikisha viongozi wa kidini, na hivyo, tunadhani kuwa siyo jambo zuri kama kweli tunataka kutafuta amani ya taifa.

Nne, Chadema haitashiriki mkutano huo kwa kuwa aliyepanga, aliyefadhili na aliyeitisha mkutano huo kwa mgongo wa TCD, ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mizengo Kayanza Peter Pinda, ambaye ndani ya nafsi yake, haonekani kuwa na dhamira ya dhati ya kuwapo amani katika taifa letu.

Ndugu waandishi wa habari;
Ninyi ni mashahidi wa jinsi Waziri Mkuu Pinda alivyo mstari wa mbele katika kuhubiri kauli za chuki, uhasama, uchochezi, ubabe na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini. Siyo mara moja wala mbili, Waziri Mkuu Pinda amesikika, tena ndani ya Bunge, akihamasiha vyombo vya usalama kuvunja sheria kwa kupiga, kuteka na kung’oa meno watu wanaotumia haki zao za kikatiba kushinikiza serikali kuchukua hatua dhidi ya maovu.

Tano, CHADEMA haitashiriki katika mkutano huo kwa kuwa Serikali ya CCM inayofadhili mkutano huu, imejaa unafiki kwa kuhubiri amani mchana, wakati usiku inachochea uhasama wa kidini, kisiasa na inawagawa Watanzania kwa misingi ya imani za kidini na vyama.

CHADEMA inao ushahidi usio na chembe ya mashaka, kwamba mifarakano mingi inayotokea kwenye jamii, mapigano katika koo mbalimbali, ugomvi wa kugombea ardhi kati ya wakulima na wafugaji, machafuko kwenye mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani, sababisho lake kuu ni CCM kuvitumia vyombo vya dola, ili kukibeba chama hicho.

Tunataka umma utuelewe, kwamba tuna dhamira ya dhati ya kuona Tanzania inakuwa kisiwa cha amani, lakini hatutakubali kushiriki katika vikao ambavyo wanaoviongoza hawana dhamira hiyo. Ili amani iweze kupatikana, ni sharti kuwepo mijadala inayoingia kwenye viini vinavyosababisha amani ikosekane na hatua hiyo ianze kuchukuliwa na ionekane inachukuliwa na serikali.

CHADEMA iko tayari, kufanya kazi ya kutafuta amani na wale wanaopenda demokrasia. Chadema haifanyakazi na wanafiki wa amani.

Imetolewa na:
Benson Singo Kigaila,
Mkurugenzi wa Oganaizesheni ma Mafunzo,
Dar es Salaam.

KILEWO NA WENZAKE KUSUBIRI MAHAKAMA KUU.

 • WASHITAKIWA WARUDISHWA GEREZANI.

 • WAKINAMAMA WAKIONGOZWA NA JOYCE KIRIA WAANGUA VILIO.

 • UPANDE WA MAWAKILI WA UTETEZI WAWASILISHA HATI YA DHARULA KUOMBA KESI IFUTWE.

20130708-M2S-CHADEMA MAHAKAMANI TABORA-0001

Mawakili wa upande wa utetezi wakiongea na wanahabari jumatatu Julai 8 2013 mkoani Tabora.20130708-M2S-CHADEMA MAHAKAMANI TABORA-0002

20130708-M2S-CHADEMA MAHAKAMANI TABORA-0003

20130708-M2S-CHADEMA MAHAKAMANI TABORA-0004

20130708-M2S-CHADEMA MAHAKAMANI TABORA-0005

20130708-M2S-CHADEMA MAHAKAMANI TABORA-0000

washitakiwa walipokuwa wanaelekea na kutoka vyumba vya mahakama mkoani Tabora jumatatu Julai 8, 2013. PICHA zote kwa hisani yaTumaini Makene; Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA

Jumatatu july 8, 2013 Ilishuhudia Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Tabora ikitumia dk. 7 tu kutolea maamuzi shauri lililofikishwa mbele yake linalo husiana na mashitaka dhidi ya Katibu wa Chadema Wilaya ya Kinondoni, Henry John Kilewo na wenzake wanne, kwa madai ya Ugaidi.

HAkitolea maamuzi Hakimu Mkuu Mkazi ilinukuliwa akisema kuwa hoja za upande wa utetezi na kesi yenyewe mahakama yake haina uwezo wa kuzisikiliza, na kudai kuwa ni Mahakamu Kuu Pekee ndiyo yenye uwezo wa kusikiliza kesi za Ugaidi.

Maamuzi hayo yalipelekea washitakiwa hao kurejeshwa rumande katika gereza la Uyuwi, hatuo hiyo ilipelekea sintofahamu baina ya ndugu na wafuasi wengi wa CHADEMA walio kuwa wamejitokeza kwa wingi kusikiliza shauri hilo.

Huku hayo yakitokea zilisikika sauti za kina mama ambao waliongozwa na Mke wa Kilewo {Joyce Kiria} wakiangua kilio huku wakilaani watu wanaotumia sheria vibaya kwa lengo la kuwatesa na kuwanyanyasa wapinzani wao kisiasa.

Baadae Taarifa ilitolewa kupitia Jopo la Mawakili Nguli wa Chadema kuwa wamewasilisha maombi Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora kuiomba mahakama hiyo kupitia upya uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora na Ikiwezekana kuifutilia mbali kesi hii.

Ombi hilo limewasilishwa kwa Hati ya Dharura na Wakili Peter Kibatala ambaye aliwasilisha ombi hilo kwa niaba ya Jopo hilo la mawakili Nguli.

MAKAMU WA RAIS BILAL KUFUNGUA MKUTANO WA 32 WA UMOJA WA POSTA BARANI AFRIKA JIJINI ARUSHA

Makamu wa Rais,Dk Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na PostaMaster Mkuu nchini,Deus Mdeme mara baada ya kuwasili ambapo kesho anatarajiwa kufungua mkutano wa 32 wa umoja wa posta AfriKa  .

 

Makamu wa Rais,Dk Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na baadhi ya viongozi waliofika katika uwanja mdogo wa kia(kisongo)kumlaki
DSCF9761
Hapa kikundi cha ngoma cha asili cha kabila la kimaasai kikitumbuiza kumkaribisha makamu wa Rais leo uwanja wa ndege kisongo
DSCF9770
Makamu wa Rais Gharib Bilal akiwa na mwenyeji wake mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo katika uwanja wa kisongo leo
DSCF9750
DSCF9762Waandishi wa habari wakibadilishana mawazo
DSCF9755 DSCF9765
DSCF9764 Hii ndiyo ndege aliyokuja nayo makamu wa Rais Ghari Bilal
DSCF9773
Meneja  wa mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Inocent Mungi akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa mkutano huo utafunguliwa na makamu wa Rais Gharib Bilal na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali duniani

SPIKA WA BUNGE LA OMAN ATEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO

DSCF9562
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akimkaribisha Spika wa bunge la Oman Khalid Maulid hivi karibuni katika Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro
DSCF9545
DSCF9548Naibu spika wa Tanzania Job Ndugai kushoto,katikati Spika wa bunge la jamuhuri ya watu wa Oman Khalid Maulid na kulia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu mara baada ya kushuka katika uwanja wa ndege wa manyara airpot wakiwa na viongozi mbalimbali
DSCF9570Spika wa bunge la jamuhuri ya watu wa Oman Khalid Maulid akiongea na vyombo vya habari ambapo alisema kuwa atachukua jukumu la kuhamasisha wawekezaji kutoka oman kuja kuekeza nchini Tanzania
DSCF9572Spika wa bunge la jamuhuri ya watu wa Oman Khalid Maulid akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu hivi karibuni
DSCF9586Naibu spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai akipokea zawadi yake kutoka kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu hivi karibuni mara baada ya kutembelea hifadhi ya ngorongoro
DSCF9579
DSCF9577Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kulia akimkabidhi mmoja wa wageni aliyevalia tishet nyeupe na blue ni Mbunge wa Mafia Abdulkarim Shah
SPIKA wa bunge la jamuhuri ya watu wa Oman Khalid Maulid ametembela Mamlaka ya hifadhi ya Taifa ya ngorongoro pamoja na mbuga ya Serengeti ilikujionea vivutio mbalimbali vinavyopatiakna ndani ya hifadhi hizo zinazopatikana katika maajabu saba barani Afrika

Akiwakaribisha  wageni hao ndani ya hifadhi ya ngorongoro hivi karibuni, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu alisema kuwa ujio huo umekuja kuimarisha mahisiano ya kibunge,kiserikali pamoja na kuwahimiza watu wa oman kutembelea Tanzania kwaajili ya kuongeza idadi ya watali
 
Alisema kuwa endapo watatembela Tanzania wateweza kujionea vivuti vyingi ikiwepo hifadhi ya Ngorongoro yenye wanyama wengi pamoja na binadamu wanaoishi na wanyama kwa kushirikiana bila kudhuriana
 
“Binadamu hawa wanashirikiana na wanyama kwa kuishi pamoja na wala hawadhuriani,wanajua namna ya kupisha na dunia nzima inakuja kushaanga maajabu haya”alisema Nyalandu

Hata hivyo alisema kuwa serikali kupitia wizara yake inaboresha miundombinu katika hifadhi hiyo ili kuweza kuhakikisha wataii wanafurahia huduma bora na kujifunza mambo mbalimbali
 
Kwa upande wake spika wa bunge la Oman Khalid Maulid alisema kuwa amefurahishwa na mapokezi aliyoyapata hapa Nchini haswa ukarimu uliopo kwa watanzania hali iliyowafanya wajione wapo nyumbani
Aidha alisema kuwa serikali yake itashirikiana bega kwa began a serikali ya Tanzania kuhamasisha wawekezaji nchini Oman kuja kuwekeza hapa nchini
“Nimefurahishwa sana na ziara hii iliyotuwezesha kujionea maajabu ambayo yanapatikana katika hifadhi ya Ngorongoro haswa bonde la ufa(creater) wanyama wa aina tofauti ikiwemo jamii ya watu ya wafugaji ambao wanaishi na wanyama bila kudhuriana”alisema Khalid
 
Katika ziara hiyo Spika huyo aliambatana na Naibu spika wa Tanzania Job Ndugai,wabunge pamoja na viongozi wengine wa hapa nchini pamoja na Oman
Na Pamela Mollel,Ngorongoro
community-herder-2.gif