MAPOKEZI YA OBAMA YAKAMILIKA, TASWIRA ZA IKULU ASUBUHI HII

huu ndiyo ujumbe wa Tanzania

Taswira mbalimbali zinazoonesha maandalizi ya mapokezi makubwa ya Rais wa Marekani Barack Obama atapowasili Ikulu jijini Dar es salaam mchana huu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama ilivyo kawaida yake amepita kila mahali kuangalia kwamba mambo yanaenda mswano, ikiwa ni pamoja na kusaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki.


Bendera zikiwa zimepangwa na kupangika katika upande wa lango kuu la Mashariki,Ikulu.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Kibao cha Barabara wa Barack Obama.

Jengo la Ikulu.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe akisoma ratiba.

Advertisements

OBAMA KARIBU! UKWELI HATU-PENDI KUANGAMIA BILA MAHALIFA

?????

Karibu!, Barack Obama. nilipenda kuja mwenyewe kukulaki utakapo fika, ila tumekatazwa kuja Dar. Mpaka sasa maandalizi ya kukupokea tayari yamekamilika. Mr President ukweli haikuwa kazi rahisi, tumetumia rasilimali watu na vijisenti ambavyo ndiyo ilikuwa akiba yetu ili ushindwe kujuwa maisha yetu ya kawaida.

Mr. President najuwa kwa kutumia interijensia yako tayari hilo unalijuwa, bila shaka vijana wako wa CIA na FBI watatusaidia kukwambia tunalo itaji, Mr. President wewe ni mweusi kama wengi wetu na bilashaka unajuwa jadi yetu ya kujitutumua mbele za watu, ila tafadhali huku sisi tunaangamia kwa kukosa mahalifa siyo tu Elimu ya juu bali hata kusoma na kuandika, kama unisadiki jaribu kupitia hata mabango yetu ya kukukaribisha.

Mr. President! wajuzi wachache ambao tunao wameingia jana usiku kutokea Mtwara na Arusha ambako jahazi letu linaelekea kuzama, kwa kweli hilo bango la kukukaribisha la hapo Airport ambalo lina makosa ya spelling ya jina lako wameliona kupitia ITV jana usiku kwenye taarifa ya habari. Tumejaribu sana  kufanya masahihisho lakini wanausalama wako wametuzuia kwa madai eti tumechelewa.

Mr President, hata hivyo ni kakosa kadogo tu. BARACK si inafanana fanana na BARAK.

ila si usafi tumejitahidi lakini? karibu sana Mr President.