KI CHUPA KIPYA CHA JUMA KASSIM NATURE FT TUNDA MAN “HAIPOTEI”

Kichupa hiki cha mtunzi, muimbaji na kwasasa mtayalishaji Juma Kassim Mohamed Kiroboto ambacho amemshirikisha Tunda Man Rais wa manzese, kilitufikia Mei 28 2013.

Kichupa ni chakawaida sana ambacho kimenakshiwa na ufundi wa kugani wa wakongwe hao. Kilicho wazi ni kwamba kama kuna walio fikiri Sir Nature amepote au atapotezwa hivi karibuni… jibu liko wazi “HAIPOTEI”

Juma Nature au Sir Nature (amezaliwa mwaka 1980 Jina kamili akijulikana kama  Juma Kassim Mohamed Kiroboto jijini Dar es Salaam) ni mwanamuziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Flava kutoka nchi ya Tanzania. Pia ni muanzilishi wa kundi la Tmk Wanaume.

Nature ni msanii mbunifu katika wa Bongo Flava na Hip Hop ya kiTanzania. Sio mtunzi tu pia ana kipaji na kujaliwa sauti nzuri ya uimbaji. Sababu nyingine zipelekeazo muziki wa Juma Nature kupendwe Afrika Mashariki ni mashairi anayotunga.

Albamu Alizotoa

  • Nini Chanzo (2001)

  • Ugali (2003)

  • Ubinadamu-Kazi (2005)

  • Zote History (2006)

Advertisements