MTANGAZAJI WA REDIO 5 SEMIO ATUNUKIWA ZAWADI YA PIKIPIKI

 Mkurugenzi wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis (kulia) akimkabidhi Pikipiki Mfanyakazi Bora wa Kituo hicho Semiyo Sonyo.
Mkurugenzi wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis Amewataka watangazaji na wanahabari wanaofanya kazi katika vituo vya Radio na Televisheni hapa nchini kuzingatia weledi wa kitaaluma wanapofanya shughuli zao za kila siku ili kusaidia jamii ya kitanzania kukabiliana na changamoto katika kipindi hiki ambacho dunia inabebwa na utandawazi. 
 
Akikabidhi pikipiki kwa mtangazaji bora wa kipindi cha usiku cha LOVE CUTTS kinacho rushwa Radio 5 katika Hafla fupi iliyofanyika jijini Arusha, Mkurugenzi Robert amesema vyombo vya habari vya kielectonic yaani Televisheni,Radio, na mitandao ya kijamii vinafikia watu kwa haraka zaidi na kwa unafuu wa gharama kuliko machapisho na kwamba vikitumika bila miiko ,weledi na kuzingatia kanuni za kitaaluma vinaweza kuwa sehemu ya tatizo badala ya kuwa vyombo vya kusukuma kasi ya maendeleo.
 
Katika tafrija hiyo Mtangazaji Semio Sonyo amekabidhiwa pikipiki ikiwa ni sehemu ya motisha zinazo tolewa na kituo cha Radio five kwa wafanyakazi wake waofanya vizuri katika majukumu yao.

Semio Sonyo akijaribu pikipiki aliyokabidhiwa na mkurugenzi wa Tan Communication Media,bwana Robert Francis

Advertisements

BUYA KUWAKILISHA MKOA WA MANYARA MODO WA UTALII….SINGIDA ZAMU YENU SASA

MANYARA 2 PICS 252Kushoto Mkurugenzi wa Event Planners na muandaaji wa shindano la Modo wa Utalii Graysson Kijo a.k.a Chinaa akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa shindano hilo Bi.Buya Ernest(19) wa pili ni Simon na Jairos kutoka kampuni ya Megatrade Investment, wadhamini wakuu wa shindano hilo kupitia kinywaji chake cha K-vant gin lililofanyika mjini Babati

MANYARA 2 PICS 255Mkurugenzi Graysson Kijo akiwa na mshindi wa shindano hilo Buya Ernest mara baada ya kutangazwa mshindi wa modo wa utalii ambaye atawakilisha Mkoa wa Manyara

MANYARA 2 PICS 256Kulia ni mshindi wa pili katika shindano hilo Veronica Christopher(20),mkurukenzi wa Event Planners Graysson Kijo,Buya Ernest(19)mshindi wa shindano hilo

MANYARA 2 PICS 259

MANYARA 2 PICS 262

MANYARA 2 PICS 283Wafanyakazi wa Events Planner wakiwa katika pozi na mshindi Buya Ernrst atakaye wakilisha Mkoa wa Manyara

Manyara pics 013Jamaa akiwa anatoa vichekesho katika shindano hilo