WAITAKA SERIKALI KUFANYIA KAZI RIPOTI YA APRM

APRM 1

Msemaji wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM Tanzania), Hassan Abbas akifafanua jambo kwa wanafunzi waliotembelea banda la APRM/AICC Nane Nane Dodoma. APRM na AICC zote ni taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje

APRM 2

Wananchi mbalimbali wakipata maelezo kuhusu kazi za APRM na AICC Nane Nane Dodoma.

APRM 3

Mmoja wa maofisa kutoka AICC, Linda Nyanda akifafanua kuhusu shughuli za AICC kwa wananfunzi wa Chuo Kikuu cha Sint John’s Nane Nane Dodoma

APRM 4Maofisa wa APRM, Praxida Gasper na mwenzake kutoka AICC, Andes Seiya wakishuhudia Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu bada ya kutembelea banda lao Nane Nane Dodoma

APRM 5 Mmoja wa maofisa wa AICC, Catherine Kilinda akifafanua masuala mbalimbali kwa wananchi waliofika katika banda la APRM/AICC Nane Nane Dodoma

Na mwandishi wetu Dodoma

Wananchi wa kada mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mjini Dodoma wamesema katika kuboresha na kuinua utawala bora nchini ni vyema Serikali ikafanyiakazi tafiti mbalimbali zinazofanywa na taasisi zake hasa tafiti za utawala bora zinazofanywa na APRM.

Wananchi hao walitoa maoni hayo kwa nyakati tofauti walipotembelea banda la Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) kwenye Maonesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzughuni  mjini Dodoma.

APRM ni Mpango wa Bara la Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora na hapa nchini taasisi hiyo imepewa dhamana ya kukusanya maoni ya wananchi katika nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania kuhusu hali ya utawala bora ili kuisaidia Serikali kufanyiakazi changamoto zinazojitokeza.

“Nimesikia kuhusu kukamilika kwa Ripoti ya kwanza ya APRM na Mheshimiwa Rais ameijadili Ripoti hii na wenzake wa Afrika, lakini mna mkakati gani wa kufanyiakazi maoni yetu,” alihoji mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu cha Saint John cha mjini Dodoma akisisitiza kuwa Serikali inapaswa kufanyiakazi maoni hayo.

Mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina la Mwalimu mstaafu Joseph Nkomwa naye alihoji kutaka kueleweshwa wananchi watashiriki vipi katika mchakato wa kuona na kufuatilia utekelezaji wa Ripoti hiyo.

Akifafanua baadhi ya kero za wananchi, Ofisa Habari na Mawasiliano wa APRM Tanzania, Bw, Hassan Abbas alisema mchakato huo ulipoanza nchini wananchi walielimishwa kupitia mikutano iliyofanyika hadi vijijini na pia kupitia semina za makundi na vyombo vya Habari nakazi hiyo ni endelefu husasani wakati huu nchi inapoelekea kuanza utekelezaji.

“Kuhusu Serikali kufanyiakazi maoni ya wananchi, huo ndio msingi wa Tanzania kujiunga na Mpango huu. Serikali ilitamka bayana kuwa imejiunga na APRM ili kusaidiana na wananchi wake katika kuboresha Taifa letu.

“APRM inakamilisha Mkakati wa Utekelezaji ambao kwa kiasi umeanza kufanyiwakazi na Serikali lakini kazi itaanza rasmi baada ya Ripoti kuzinduliwa Oktoba mwaka huu,” alisema.

Bw. Abbas aliongeza kuwa hata hivyo kabla ya hatua hiyo kufikiwa nchi haizuiwi kuanza kufanyiakazi maoni ya wananchi wake yaliyotolewa katika ripoti. “Hapa nchini ukiangalia maoni yaliyotolewa na wananchi kuhusu masuala kama katiba na matakwa ya kudhibitiwa matumizi holela ya fedha katika chaguzi, haya yameshafanyiwa kazi au yanaendelea kufanyiwa kazi,” alisema Bw. Abbas.

Advertisements