SUMMAYE AWASHUKIA WANASIASA,ASEMA WANAWATUMIA VIJANA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA

DSCF0217WAZIRI Mkuu mstaafu Fredrick Summaye akisoma hotuba kwa vijana waliohudhuria uzinduzi wa taasisi ya Tanzania Youth Development Center jijini hapa,

DSCF0218Vijana wakifatilia hotuba

DSCF0221Mama nice(aliyevalia kitenge)akisikiliza hotuba kwa makini

DSCF0219Waalikwa mbalimbali wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi

DSCF0229Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kikazi zaidi

DSCF0223

DSCF0227WAZIRI Mkuu mstaafu Fredrick Summaye amekemea tabia ya wanasiasa
nchini  kuwachanganya vijana na viongozi wa serikali kwa kuwashawishi
vijana kwa rushwa na na kuwatumia katika kusafirisha madawa ya kulevya
katika maeneo mbalimbli nchini na nje ya nchi.

Akizungumza jana katika uzinduzi wa taasisi ya Tanzania Youth Development Center jijini hapa, Sumaye alisema tatizo la rushwa limekuwa likikuwa kwa kasi kubwa nchini kwa wanasiasa na viongozi wenye nyadhifa serikalini,kwa kutumia fedha zaokuwatumia vijana ambao wamekuwa chambo ya kusafirisha madawa hayo huku wakilipwa fedha ndogo ambapo baada  ya mda wanakamatwa na wao kunufaika mabilionea kupitia njia hiyo.

“hili tatizodawa za kulevya limekuwa likiwaathiri kwa sehemu kubwa
vijana wa nchi hii ambao ndio nguvu kazi ya taifa letu,wanasiasa
tuache hii tabia ya kuhonga vijana na taasisi hii tukiwapa masharti
yenye malengo yetu ya siasa tutakuwa tunajaribu kuwaondoa katika
malengo ya msingi ya taasisi yenyewe”alisema Sumaye

Sumaye alisema rushwa ya madaraka ina athari kubwa kwa umma na nchi ni
ile inayotolewa katika kusaka madaraka ya kisiasa ambapo mara nyingi
anayefanya hivyo amekuwa na uchu na uroho wa madaraka na yuko tayari
kufanya lolote na chochote ili apate  madaraka anayoyahitaji.

“vijana msikubali kutumia miili yenu kubebea madawa ya kulevya kwani
yanawaathiri kwa asilimia kubwa na mara nyingi tumeshuhudia wengine
wakifanyiwa upasuaji na badala yake wamekuwa wakipoteza maisha”alisema
Summaye

Aidha alisema kuwa kitendo cha vijana kutumiwa kama chambo cha
kusafirisha madawa ya kulevya nje ya Nchi ni unyanyasaji
mkubwa,unyama,kwani mwisho wa siku wanaonufaika ni wengine na wao
kubaki kuwa masikini.

Pia alisema rushwa imekuwa ikitumika katika nyakati za uchaguzi na
wananchi wamekuwa wakinunuliwa kwa njia mblimbali na wengine kubaki
wakiwa maskini wakati wana siasa wanapohitaji kupandishwa vyeo.

“ lazima tujiulize unawanunua wapiga kura ili iweje? Kama unajiamini
kuwa wewe unafaa kwa nafasi hiyo kwanini usiwaache wapiga kura
wakaamua bila vishawishi vya rushwa? Dalili kubwa ni kuwa kama
unatumia vishawishi vya rushwa wewe hutoshi katika hiyo nafasi
vinginevyo ungewaacha wapiga kura waamue wapendavyo,”alisema.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa taasisi hiyo Lengai
Sabaya, alisema taasisi hiyo imeshaanzisha matawi kote nchini ili
kuweza kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri wenyewe, kupambana na
magonjwa hatarisi ikiwemo ugonjwa wa Ukimwi.
“Vijana walioshiriki katika uzinduzi huu ndugu mgeni rasmi wanatoka
katika kanda ya kaskazini na ni wenye umri wa kuaznia mika
15-35”alisema Sabaya

Alisema pia malengo mengine ya taasisi hiyo ni pamoja na kupambana na
dawa za kulevya, uchafuzi wa mazingira, rushwa ufisadi na uovu
unaosababishwa na madhara ya dawa za kulevya na kwamba ndoto kubwa ya baadae ni kusaidia vikundi vidogo vya maendeleo na kutoa ushauri wa
kitaalum katika kunufaisha maendeleo kwa vijana.

Advertisements