CCM BUKOBA YAWATIMUA MADIWANI WAKE WA NANE KWA MADAI YA UKOROFI

Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Bw Avelin Mushi amenukuliwa wakati alipokutana na wanahabari kuwa kikao cha Halmashauri Kuu ya mkoa wa Kagera kimeamua kuwafukuza uwanachama madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba pamoja na kuwafutia nyadhifa za udiwani huku akitaja sababu kuwa ni mgogoro uliokuwa ukiendelea kwa muda mrefu sasa.

Waliofukuzwa ni:

1. Richard Gaspar (Miembeni )

2. Murungi Kichwabuta (viti maalum)

3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)

4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)

5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)

6. Robert Katunzi (Hamugembe)

7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na

8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).

Katibu huyo ameongeza kuwa madiwani hao wanaweza kukata rufaa kwa ngazi za juu za chama wakiona hawakutendea haki na kuwa ngazi ya mkoa ina mamlaka ya kufanya hivyo kwa madiwani wa ngazi hizo.

Aidha amesema kwa Bw Yusuph ngaiza amabye ni mwenyekiti wa CCM bukoba,nafasi yake hiyo inasubiriwa ngazi za juu amabazo ndizo zenye mamlaka juu yake(kwa cheo hicho)

Manispaa ya Bukoba ina kata 14 na kati ya hizo kata 4 zinaongozwa na CDM(2) na CUF(2) hivyo kwa Bukoba mjini CCM imebakiza madiwani 3 TU wa kuchaguliwa .kama ifuatavyo

1.Kashai-Amefukuzwa
2. Miembeni-Amefukuzwa
3.Miembe-Amefukuzwa
4.Nyanga-Amefukuzwa
5.Hamugembe-Amefukuzwa
6.Kitendaguro-Amefukuzwa
7.Ijuganyondo-Amefukuzwa
8.(1)Kagondo-Amebaki (CCM) (Meya Amani)
9.(2)Nshambya-Amebaki(CCM)
10.(3)Kahororo-Amebaki(CCM)
11.Bilele-Amebaki(CUF)
12.Kibeta-Amebaki(CHADEMA)
13.Bakoba-Amebaki(CUF)
14.Rwamishenye-Amebaki(CHADEMA)
XXXXXXXXXXXXX

Kujua historia ya chanzo cha yote hapa fungua hapa chini.

Mangula kazima moto kwa petrol Bukoba

Ufisadi wa Meya wa Bukoba Anatory Aman

Jeuri ya Kagasheki: Madiwani walipwa posho kususia bajeti ya Manispaa ya Bukoba!

Vita ya Kagasheki na Dk Aman ngoma nzito,madiwani waburuzwa Takukuru

Mgogoro wa Umeya Bukoba: Mangula ageuka mbogo; awataka wasiomtaka Amani kurudisha kadi

Advertisements

MADIWANI ARUSHA WAAMURU HALMASHAURI ING’OE MABANGO YA BIASHARA YASIYOLIPIWA

a

b

c

d

e

f

Halmashauri ya jiji la Arusha imeanza zoezi la kung’oa mabango yote ya Matangazo ambayo yalikuwa ayajalipiwa kwa muda mrefu jijini Arusha huku ikidaiwa ni shinikizo kutoka kwa Madiwani wapya.

Pichani juu ni baadhi ya mabango yanayoendelea kutolewa (WANANG’OA NA NGUZO), huku magari yanayomilikiwa na jiji yakipakia mabaki ya nguzo hizo.

Sehemu ya mzunguko wa mnara wa saa iliyokuwa na ‘jam’ ya mabango hasa za kampuni ya vinywaji na mabenki sasa inaonekana kupumua kama inavyoonekana hapo juu.

ANNUAL GONGA’S WHITE ‘BEACH’ PARTY DAR 2013 SAT. 17TH AUGUST AT LEDGER PLAZA

white party

ANNUAL Gonga’s WHITE ‘Beach’ PARTY DAR 2013 Sat 17th AUGUSt 2013 at LEDGER PLAZA BAHARI BEACH HOTEL from 1300Hrs Till Dawn… White FLIP FLAPS,White Swimm Suits, White LINENS, White Shorts, White VESTS, WHITE Panties is All what we DO on This… Save the DATE so U Don’t Miss Out… We DO At SWIMMING POOL at THE BEACH…. Proudly Sponsored By JACK DANIELS, 100.5 TIMES FM, Valley SPRINGS.. C U There