CHOPA YA DR. SLAA KUKUSANYA MAONI YA KATIBA GONGOLAMBOTO LEO JUMAMOSI

  • DR. SLAA KUAMBATANA NA MARANDO, MNYIKA, MDEE NA WAITARA.

  • WANANCHI WAJIPANGA KUTOA MAONI YAO HUKU WAKIDAI KUKUMBWA NA MATATIZO MAKUBWA JIMBONI MWAO

Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa Leo Jumamosi anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara Dar es Salaam katika uwanja maarufu wa Kampala ulioko Gongolamboto.

Katibu wa Jimbo la Ukonga Juma Mwaipopo amenukuliwa akisema, Dr Slaa ataunguruma katika viwanja hivyo ikiwa ni maalum kwa ajili ya kukusanya maoni ya Katiba mpya.

taarifa zinadai kuwa Katibu Mkuu huyo wa Chadema ataongoza kikosi cha makamanda akiwemo Mjumbe wa Kamati Kuu Mabere Marando,Wabunge John Mnyika na Halima Mdee,Mkurugenzi wa sera na utafiti Mwita Waitara pamoja na viongozi mbalimbali walioko makao makuu.

Kwa siku za karibuni Chadema imekuwa ikipata ufuasi mkubwa jimboni Ukonga na hii ni kutokana na jimbo hilo kuwa kama vile halina mbunge kutokana na matatizo makubwa yaliyopo jimboni humo.

Kumekuwa na ubovu mkubwa wa miundombinu jimboni Ukonga hasa kipindi cha mvua ambapo nauli ya daladala imekuwa ikifika hadi shilingi 1000/-

Tayari kuna shamrashamra nyingi kusubiri ujio huo wa Dr Slaa ambaye ana mvuto wa kipekee nchini.

Advertisements