CHADEMA KIVUTIO ZIARA YA KIKWETE MWANZA

  • GARI LA MOVEMENT FOR CHANGE (M4C) LAONEKANA KWENYE MSAFARA  WA RAIS.

  • MAAFISA USALAMA WATAKA KULIZUIA WASHINDWA.

  • WAZIRI WA UJENZI, MAGUFULI AZOMEWA BAADA YA KUMTAJA MATATA.

  • WANANCHI WAPAZA SAUTI WAKITAKA MBUNGE WAO ATAMBULISHWE KAMA KIONGOZI KWENYE ZAIRA HIYO.

  • MBUNGE WA NYAMAGANA AWASALIMIA WANANCHI MBELE YA RAIS KWA KIBWAGIZO CHA PIPOZ….. WENYEWE WALIPUKA  POWER!!!!

Ziara ya RAIS Jakaya Kikwete jana ilishuudia nguvu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Mwanza baada ya viongozi na matukio yanayo usisha cha hicho kuonekana kuwavutia zaidi wananchi wa jiji hilo.
Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje, alivunja mwiko baada ya kujiunga katika msafara huo wa raia akiwa na gari lenye alama za Movement for Change (M4C) lililokuwa limefungwa bendera mbili za CHADEMA. hatua ambayo iliwakwaza maofisa wa usalama ambao walipata wakati mgumu kulizuia gari hilo lisiwepo katika msafara huo, jambo lililozua tafrani kidogo katika uwanja wa Furahisha ambapo Kikwete alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara.
Awali wakati wa uzinduzi wa wodi ya wazazi iliyoko eneo la Butimba, Rais alilazimika kumpa Wenje nafasi ya kuwasalimia wananchi baada ya Mkuu wa Mkoa, Evarist Ndikilo, kutaka kufanya hila ya kumnyima haki hiyo kama mbunge wa jimbo husika. Baada ya viongozi wote kutambulishwa bila Wenje kutajwa, wananchi walianza kupaza sauti wakitaka mbunge wao naye atambulishwe.
Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje baada ya kusimama alimshukuru Rais Kikwete kwa kumpa nafasi hiyo lakini akamwomba amvumilie kidogo atoe salamu maalumu ya wana Mwanza. Kama kawaida ya CHADEMA kwenye salamu yao, Wenje aliwaomba wananchi wakunje ngumi kisha akawasalimu kwa kibwagizo cha peoples… nao wakamwitikia power!
Akiwa katika viwanja vya Furahisha ambapo Rais Kikwete alichelewa kuanza mkutano wake, Wenje alifika hapo na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi huku polisi wakiwazuia bila mafanikio. Ilipofika saa 12 jioni kabla Rais hajaingia uwanjani, wananchi hao walimtaka Wenje awahutubie huku wakidai bendera ya taifa ishushwe kwani muda wake ulikuwa umefika.
Kikwete aliingia uwanjani hapo saa 12:10 akiongozana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali lakini wananchi hawakuonyesha kumshangilia badala yake walikuwa wakimwonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na CHADEMA wakiimba ‘peoples…power’. Viongozi wa CCM walionyesha kushangazwa na wananchi wa mwanza baada ya kumshangilia kwa nguvu mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, aliyekuwa ameongozana na Rais kwenye mkutano huo.
Katika hatua nyingine Waziri wa Ujenzi, Dk. Magufuli, alikumbana na jinamizi la kuzomewa mbele ya Rais baada ya kusimama jukwaani na kutaja jina la Matata (ambaye ni Meya wa jiji la Mwanza mwenye mgogoro na CHADEMA) , ambapo wananchi wengi walimzomea kwa miluzi huku wakimnyooshea vidole viwili.
Wananchi walizidi kuzomea pale Magufuli aliposema wabunge wa Ilemela na Nyamagana jijini hapa ni wana CHADEMA lakini ndani ya roho zao ni wana CCM. wananchi hao walizidi kukeleka pale waziri huyo aliposema kuwa iwapo Rais angehitaji kupokea kadi za CHADEMA zilizorudishwa angepokea nyingi.
Akizungumza katika mkutano huo, Rais Kikwete alimpongeza mbunge wa Nyamagana kwa uchapakazi mzuri hasa kusimamia sekta ya elimu na kwamba wabunge wa namna hiyo wanastahili kuigwa.
Hata hivyo, alisema serikali yake imejipanga vizuri kuhakikisha usafiri wa reli, ndege, majini na barabara za lami vinaboreshwa maradufu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
“Serikali yangu imeweka nguvu kubwa katika kuboresha sekta ya uchukuzi, ujenzi na nyinginezo. Hii ni kutaka kuwaletea wananchi wetu maendeleo ya kisekta,” alisema.
Baadhi ya mawaziri walioongozana na Rais mbali na Magufuli ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Kitwanga, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, Naibu Waziri wa Ujenzi na Dk. Charles Tizeba.
Advertisements

5 thoughts on “CHADEMA KIVUTIO ZIARA YA KIKWETE MWANZA

  1. haaaaa matata anakubalika sana ilemela kama angekuwa akubaliki asingechanguliwa hilo ni jembe cku nyingi sana

Comments are closed.