MTANGAZAJI MKONGWE JULIUS NYAISANGA AFARIKI DUNIA

 

Marehemu Julius Nyaisanga wakati wa uhai wake
Kutoka kushoto kwenda kulia,Richard Maabadi,Sauda Simba,Rukia Mtingwa,Manambi Ismail
Uncle J Julius Nyaisanga (Marehemu)John Ngahyoma (Chanzo:bongocelebrity.com)

Habari zilizothibitishwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari mkoa wa Morogoro, Aziz Msuya kwa njia ya simu zinaeleza kuwa mtangazaji mkongwe nchini Tanzania Julius Nyaisanga ‘Uncle J” amefariki dunia  Siku ya Jumapili 21 October 2013 asubuhi katika hospitali ya Mazimbu iliyoko katika Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) eneo la Mazimbu alikokuwa amelazwa.

Msuya ameeleza kuwa Mwili wa Marehemu utahamishiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro asubuhi hii kwa ajili ya taratibu zingine.

Nyaisanga alikuwa ameshaomba likizo ya mapumziko kutokana na kutoka Radio Aboud ambako alikuwa akifanyakazi kutokana na kuugua Kwa mujibu wa chanzo chetu taarifa za kifo chake zimezagaa asubuhi hii na bado haijafahamika zaidi sababu za kifo chake

Julius Nyaisanga  alijulikana sana tangu akifanya kazi Redio Tanzania sasa hivi inajulikana kama TBC Taifa,ITV na Redio One stereo kabla ya kwenda Morogoro kujiunga na Radio Aboud.

Advertisements

2 thoughts on “MTANGAZAJI MKONGWE JULIUS NYAISANGA AFARIKI DUNIA

  1. Usually I don’t learn post on blogs, but I would like to say that this write-up very forced me to take a look at and do it! Your writing style has been surprised me. Thank you, quite great post.

Comments are closed.