DIAMOND KUWASHA MOTO ARUSHA “USIKU WA WASAFI”

diamond.....
Msanii  maarufu wa muziki wa Kizazi kipya Diamond Platnum anatarajiwa kufanya  shoo ya aina yake jijini  Arusha  siku ya Jumamosi  ya  tarehe 30 katika viwanja vya Hoteli ya Mount Meru ijulikanayo kama “ usiku wa wasafi”
 
Muandaaji wa shoo hiyo,Mkurugenzi wa kampuni ya Mwandago Investment Faustine Mwandago akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Arusha jana alisema kuwa maandalizi  ya awali ya shoo hiyo yamekamilika kwa kiasi kikubwa 
 
Mwandago alisema kuwa  shoo hiyo itakuwa ya kukata na shoka  na itawapa burudani ya kutosha mashabiki wa msanii huyohivyo kuwataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi siku ya jumamosi
 
 “kwa hapa Arusha Diamond tumezoea kumuona  kwenye shoo za Mamiss kama Miss Arusha na nyinginezo lakini kwa sasa hivi anakuja kwa ajili ya kutoa burudani tu kwa mashabiki wake hivyo naamini kuwa shoo hiyo itakata kiu kwa watakaohudhuria.”alisema mwandago
 
Mbali na burudani kutoka kwa msanii huyo wasanii chipukizi kutoka jijini hapa watapata nafasi ya kumiliki jukwaa hali itakayopelekea vipaji vyao kutambulika
Wasanii hao chipukizi ni Marry,Kandisi,Roggerz na madansa wa boda 2 boda waliopo chini ya Mwandago Investment watapamba shoo hiyo.
 
Katika kunogesha shoo ya Diamond  dress code itakuwa vazi jeupe kuendana na jina la shoo la Usiku wa Wasafi
Advertisements

TAARIFA KWA WATANZANIA JUU YA UAMUZI WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO KUHUSU KUWAVUA NYADHIFA ZA UONGOZI NAIBU KATIBU MKUU, MH. ZITTO ZUBERI KABWE NA WENZAKE

CHADEMA
UTANGULIZI
Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA,
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyokutana Ubungo Plaza, Dar es Salaam kuanzia asubuhi ya siku ya Jumatano ya tarehe 20 Novemba, 2013 hadi alfajiri ya leo Ijumaa tarehe 22 Novemba, 2013 imetafakari na kujadili kwa kina taarifa mbali mbali juu ya hali ya kisiasa ndani na nje ya Chama chetu ambayo kwa muda mrefu imegubikwa na tuhuma kubwa na nzito dhidi ya Chama chetu na viongozi wake wakuu, yaani Mwenyekiti wa Taifa, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe (MB), na Katibu Mkuu, Dk. Wilbrod Peter Slaa. Tuhuma hizi zilikuwa na malengo na athari ya kuwapaka matope na kuwachafua viongozi wakuu wa Chama na Chama chenyewe, kutengeneza mtandao wa siri ndani na nje ya Chama ambao hatimaye ungefanikisha sio tu lengo la kufanya mapinduzi nje ya utaratibu wa kikatiba wa Chama, bali pia ungekipasua Chama vipande vipande na hivyo kuua matumaini ya Watanzania juu ya uwezekano wa kufanya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi na kijamii katika nchi yetu kwa kukiondoa madarakani Chama cha Mapinduzi (CCM).
Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA,
Uchunguzi wa Kamati Kuu umebaini kuwepo kwa mkakati mkubwa wa kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013.’ Mkakati huu uliandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’ ambacho vinara wake wakuu ni wanne, yaani Naibu Katibu Mkuu na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ambaye kwenye waraka huo anajulikana pia kama ‘MM’ au ‘Mhusika Mkuu’; mjumbe wa Kamati Kuu na mwanazuoni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitilla Mkumbo ambaye kwenye waraka anajulikana pia kama M1; Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha ambaye kwa sasa amesimamishwa uongozi, Bwana Samson Mwigamba na ambaye kwenye waraka anaitwa M3; na mtu mwingine ambaye hadi sasa jina lake halijajulikana lakini kwenye waraka anajulikana kama M2 na anatajwa kuwa yuko ‘ukingoni kupigwa nje’ katika mageuzi ya kiutendaji yanayoendelea katika Sekretariat ya Chama hapa Makao Makuu.
Kwa mujibu wa waraka wenyewe, “Mkakati huu umeandaliwa kwa pamoja na M2 na M3 na kupitiwa na kurekebishwa na M1 ili upelekwe kwa MM kwa maoni ya mwisho na kuanza utekelezaji.” Mbele ya Kamati Kuu, Dk. Mkumbo alikiri kwamba MM au Mhusika Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe; M1 ni yeye mwenyewe Dk. Mkumbo na M3 ni Bwana Mwigamba. Dk. Mkumbo alikataa kata kata kumfahamu M2. Aidha, Dk. Mkumbo alikiri mbele ya Kamati Kuu kwamba yote yaliyoandikwa katika ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ yametoka kwenye ‘Mtandao wa Ushindi’ na hayajabadilishwa.
Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA,
Mkakati wa Mabadiliko 2013 ni mpango wa kuipasua pasua CHADEMA na kuiangamiza kabisa kwenye uso wa siasa za Tanzania. Huu sio mkakati wa kufanya mabadiliko ya kiuongozi ndani ya Chama kwa njia za kidemokrasia na za kikatiba. Ni mpango wa kukiteka nyara Chama na kukiua. Ndio maana watunzi wa waraka huu wamesema kwenye waraka wao: “Tunahitaji kutekeleza mkakati huu kwa siri kubwa ili mkuu aliyepo aendelee kubweteka na ndio maana hata lugha iliyotumika ndani hapa ni ya pekee.” Kamati Kuu inaamini mkakati wenye malengo halali ya kufanya mabadiliko ndani ya Chama kwa njia halali za kikatiba usingependekeza kwamba: “Vikao vyetu na yeye (MM aka Mhusika Mkuu aka Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe) vitafanyika mara chache sana na mahali pa faragha kupita kiasi ikiwezekana hata nchi jirani.” Aidha, Kamati Kuu inaamini kwamba kama mkakati huu ungekuwa na malengo mazuri ya kukijenga Chama na sio kukiteka nyara na kukiua, wanamtandao hawa wasingependekeza utaratibu ufuatao wa utekelezaji wa mpango: “M1 (Dk. Mkumbo) ndiye atakayekuwa anawasiliana na tunayemtaka ambaye ataitwa MM (Mhusika Mkuu). Tumepanga kwamba kusiwe na mawasiliano mengi kati ya kamati na mhusika mkuu kuepuka tracking ya wapinzani wetu. M1 ni mtu wa karibu na MM kwa hiyo mawasiliano yao hayataweza kutiliwa shaka na mtu yeyote hata wangewasiliana mara nyingi kiasi gani. Hata hivyo, linapokuja suala la mkakati huu tunasihi mawasiliano yawe kwa kuonana uso kwa uso ama kwa simu na si sms. M1 ndiye atakayewasilisha mambo yote yanayotoka kwenye kamati ya kitaifa na endapo kuna haja ya MM kukutana na kamati ya kitaifa, mipango yote ya kikao itafanywa na M1 kwa usiri mkubwa.”

Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA,
Mkakati wa Mabadiliko 2013 ni mpango haramu na ambao unaichana chana Katiba ya Chama chetu. Ni mkakati wa vita dhidi ya Chama chetu na utaratibu wetu wa kikatiba.
1. Wakati ibara ya 10.1(iv) ya Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama ambazo ni sehemu ya Katiba ya Chama chetu ya mwaka 2006 inamkataza kiongozi wa CHADEMA asijihusishe na vikundi vyenye misingi ya ukabila, udini, au ukanda ambavyo vina makusudi ya kubaguana ndani ya Chama na miongoni mwa jamii kisiasa au kijamii”, wanaMtandao wa Ushindi wameonyesha wazi kuwa wanaendekeza siasa za udini kwa kusema yafuatayo juu ya waliemwita ‘mtu tunayemtaka’, yaani Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe: “Kwa kuwa ni Mwislamu, hii ni fursa katika kupata kuungwa mkono na wanachama waislamu ambao wamekuwa na kigugumizi wakidhani waislamu hawatakiwi katika uongozi wa taasisi yetu.”

2. Wakati ibara ya 10.1(viii) ya Kanuni za Uendeshaji inamtaka kila kiongozi wa CHADEMA “… kuwa mkweli na muwazi wakati wote … na aachane na vikundi vya majungu na wadanganyifu (rumour mongers) …”, wanaMtandao wa Ushindi wameeleza kwenye waraka wao kwamba mipango yao ya utekelezaji wa Mkakati wa Mabadiliko 2013 ‘itafanyika kwa usiri mkubwa.’

3. Wakati ibara ya 10.1(ix) ya Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama inamtaka “kiongozi asijihusishe na vikundi na vitendo vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama au wanachama wake”, wanaMtandao wa Ushindi wamesambaza tuhuma za uongo dhidi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa (ambaye wanamwita kwenye waraka wao kuwa ni ‘Mpinzani wetu’) kuwa “… hana mahusiano mema na mazuri na viongozi wa ngazi za chini kutokana na dharau nyingi anazozionyesha pale anapokutana na viongozi wa ngazi za chini akiwa katika kuijenga taasisi hii…. Hii imemfanya kutopendwa na viongozi wengi wa ngazi za chini hivi sasa na kutoa fursa ya pekee kwa tunayemtaka.”

4. Wakati ibara ya 10.1(x) ya Kanuni za Uendeshaji inamtaka “kiongozi asitoe tuhuma zozote juu ya viongozi wenzake pasipo kupitia vikao halali na kuzingatia taratibu na ngazi zilizowekwa kwenye Kanuni”, tuhuma zote zilizotolewa na wanaMtandao hawa dhidi ya viongozi wakuu wa Chama chetu hazijawahi kutolewa na yeyote kati ya wanaMtandao hawa katika kikao chochote halali cha Chama cha ngazi yoyote.

5. Wakati ibara ya 10.1(xii) ya Kanuni za Uendeshaji inaeleza kwamba “itakuwa marufuku kwa kiongozi wa CHADEMA kukashifu Chama, kiongozi au mwanachama yeyote wa Chama …”, Mkakati wa Mabadiliko 2013 umejaa kashfa kubwa, matusi mengi na udhalilishaji mkubwa wa Chama, viongozi wake wakuu na wanachama kwa ujumla. Hivyo, kwa mfano, Mwenyekiti wa Chama Taifa ametuhumiwa na wanaMtandao hawa kuwa ni mtu mwenye ‘uzalendo unaotia shaka’, mwenye ‘elimu ya magumashi’, ‘mzito kujieleza’, ‘mtu mwenye akili ndogo’, n.k.

Ndugu wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA,
Hakuna chama au taasisi yoyote duniani inayoweza kunyamazia mkakati wa aina hii dhidi yake na viongozi wake wakuu na ikadumu au kubaki salama. Chama au taasisi yoyote inayoendekeza vitendo vya aina hii miongoni mwa viongozi wake wa ngazi yoyote au miongoni mwa wanachama wake wa kawaida inakaribisha kifo na mauti. Chama chetu na viongozi wake wa juu wamekaa kimya kwa muda mrefu sana; wamevumilia mashambulizi na kashfa nyingi sana dhidi yao binafsi na dhidi ya Chama; wamestahimili matusi makubwa sana dhidi yao. Chama chetu kimevumilia yote haya na viongozi wake wamevumilia yote haya sio kwa sababu walitaka Chama chetu kiuwawe na wanaMtandao hawa. Uvumilivu wote huu ulitokana na haja ya kuwapa wanaMtandao wa Ushindi fursa ya kugundua hatari ya siasa zao na kuwapa muda wa kujirekebisha na kujirudi.

Kama ilivyo kwa binadamu au taasisi yoyote ile, uvumilivu wa Chama chetu na viongozi wake wakuu una kikomo. Na hiki ndio kikomo cha uvumilivu wa Chama chetu, viongozi wake na wanachama wake kama wanavyowakilishwa na Kamati Kuu ya Chama chetu. Hivyo basi, katika kikao chake tajwa, Kamati Kuu ya Chama chetu, kwa kutumia mamlaka yake ya kikatiba ya dharura chini ya ibara ya 6.5.2(d) ya Katiba ya Chama, imeazimia yafuatayo kuhusu Mkakati wa Mabadiliko 2013 na hao wanaojiita wanaMtandao wa Ushindi:
(a) Kwamba, kuanzia sasa, viongozi wote waliohusika ama kuhusishwa na mkakati huu, yaani Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, Mjumbe wa Kamati Kuu Dk. Kitilla Mkumbo na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba wavuliwe nyadhifa zao zote za uongozi ndani ya Chama;

(b) Kwamba timu ndogo ya pamoja ya watendaji wa Sekretariat ya Makao Makuu ya Chama na wajumbe wa Kamati Kuu ifanye uchunguzi wa haraka ili kumtambua mtu anayeitwa M2 na ambaye anadaiwa kuwa mtumishi wa Makao Makuu ya Chama ili hatua stahiki na za haraka zichukuliwe dhidi yake, pamoja na watu wengine wote watakaobainika kuhusika na mpango huu wa uhaini dhidi ya Chama chetu;

(c) Kwamba Kamati ya Chama ya Wabunge inaelekezwa kuchukua hatua za haraka za kuhakikisha Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe anavuliwa madaraka yake yote kama Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, with immediate effect;

(d) Kwamba viongozi waliotajwa katika aya ya (a) waandikiwe hati zenye tuhuma dhidi yao haraka iwezekanavyo na watakiwe kujieleza kwa nini wasifukuzwe kwenye Chama kwa vitendo vyao na wapatiwe fursa kamili ya kujitetea kama inavyotakiwa na ibara ya 6.5.2(a), (b) na (c) ya Katiba ya Chama;

(e) Kwamba mara baada ya utekelezaji wa azimio (d), Kamati Kuu ikutane kwa dharura kwa ajili ya kufanya uamuzi juu ya hatma ya watuhumiwa na hatua nyingine zitakazofuata;
(f) Kwamba waraka wa wanaojiita wanaMtandao wa Ushindi uwekwe hadharani na usambazwe kwa vyombo vya habari vya aina zote ili wananchi wa Tanzania, wanachama na viongozi wa Chama chetu na dunia nzima kwa ujumla iweze kupima uzito wa Mkakati wa Mabadiliko 2013 na uhalali wa maamuzi haya ya Kamati Kuu.

Ndugu wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA,
Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Mjumbe wa Kamati Kuu Dk. Kitilla Mkumbo waliiomba Kamati Kuu iwaruhusu kujiuzulu nyadhifa zao baada ya Mkakati wao wa kukiteka nyara Chama na kukiangamiza kujulikana mbele ya Kamati Kuu. Kwa kuzingatia uzito wa makosa waliyokifanyia Chama, viongozi wake wakuu na wanachama wake kwa ujumla; na kwa kuzingatia uzito na umuhimu wa nyadhifa kubwa walizo nazo ndani ya Chama; na kwa kuzingatia uelewa wao wa Katiba, Kanuni na taratibu za Chama na uzoefu wao katika safu za juu za uongozi wa Chama, Kamati Kuu ilikataa kwa kauli moja kuridhia maombi hayo ya kujiuzulu. Kufanya hivyo ingekuwa ni sawa na kuwaruhusu wajiondoe kwenye uongozi wa Chama wakiwa na heshima wasizostahili hata kidogo.
Chama chetu ni tumaini pekee la Watanzania wote wanaotaka mabadiliko ya kweli na ya kimsingi katika mfumo wa kiutawala, kiuchumi na kijamii wa nchi yetu. Hii ndiyo sababu kubwa na ya pekee iliyosababisha vita kubwa na chafu inayopigwa dhidi ya Chama chetu na viongozi wetu wakuu. Lengo kuu ni kuwachafua viongozi wakuu, kuleta mgogoro na mgawanyiko ndani ya wanachama, viongozi wake na hivyo kukichafua Chama mbele ya macho ya Watanzania. Chama chetu kikishachafuka kwa mtindo huu, matumaini ya Watanzania wanaotaka mabadiliko yatakufa. Vita hii kubwa haijaanza jana, na haitaisha kesho. Kama ambavyo tumekabiliana nayo na kuishinda siku za nyuma, vivyo hivyo tutakabiliana nayo mara hii na kuishinda. Kama Chama chetu kilivyoibuka na nguvu na heshima kubwa zaidi katika mapambano ya siku za nyuma, vivyo hivyo Chama chetu kitaibuka na nguvu na heshima kubwa zaidi katika awamu hii ya mapambano.
Tunawaomba Watanzania, wanachama na viongozi wetu wasife moyo, bali waendelee kukiunga mkono chama chao cha ukombozi. Tunawaomba Watanzania, wanachama na viongozi wetu waendelee kulilinda tumaini lao pekee la mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika nchi yetu. Badala ya kukatishwa tama, kila mmoja wetu aongeze bidii maradufu ili kuwashinda wale wanaotaka kuleta majanga katika Chama chetu na kwa Taifa letu.FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB) WILBROD PETER SLAA
MWENYEKITI, TAIFA KATIBU MKUU

P SQUARE NDANI YA DAR

 Wanamuziki wanaotajwa kuwa na mvuto zaidi barani Afrika, P Square, wamewasili usiku huu katika uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere  kwa ajili ya onesho lao linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii katika viwanja va Leaders Club maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Pichani juu ni Petter(wa pili kutoka kushoto na Paul).Kulia ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamini wakuu wa onesho lao ambalo limeratibiwa na East africa Radio na TV
 Hapa wakifanya mahojiano na kituo cha East Africa TV ambao ndio wenyeji wao
Mahojiano na picha za hapa na pale zikiendelea…
Vijana wakielekea kupumzika tayari kwa kazi

ILIVYOKUWA MKUTANO WA CHADEMA NA WANAHABARI JUU YA KUWAVUA WANACHAMA BAADHI YA VIONGOZI WAKE

Baada ya mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)  kuwasili alianza kwa kusema kuwa kamati kuu imemteua kamanda Tundu Lissu kuwa mwanasheria mkuu wa chama na pia kamati kuu imefikia maamuzi ya kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa baadhi ya viongozi.

Mwenyekiti akamkaribisha Tundu Lissu kwa ajili  ya kutoa taarifa ya maazimio ya kamati kuu kwa niaba yake.

Tundu Lissu alianza kwa kusema kuwa kamati kuu imefanikiwa kupata waraka wa siri wenye mpango wa kukipasua chama chini ya uratibu wa Zitto Kabwe,  Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba na mtu mwingine ambaye bado awajafanikiwa kumpata.

Lissu anaendelea kueleza waraka huo uliopewa jina la waraka wa ushindi inavunja  katiba ya chama na wala wahusika awajawahii kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama.

Lissu alieleza kuwa wahusika waliomba kujiuzulu baada ya waraka huo kukamata lakini uongozi wa chama ulikataa kwa vile awakuona sababu ya watu hao kupata nafasi ya kuondoka kwa heshima ambayo awastahili.

Haidha chama hicho kimeagizwa kuwaandikia barua wahusika kuwataka wajieleze kwanini wasivuliwe uanachama kwa kosa kubwa waliofanya.

Mwisho alimaliza kwa kusema waraka huo utasambazwa nchi nzima ili wananchi wausome.

BREAKING NEWS:- CHADEMA YAWAVUA UONGOZI ZITTO, MKUMBO NA WENGINE.

m2s breaking news

Habari kutoka kwenye Kikao cha kamati kuu ya chama cha CHADEMA ambacho kilimalizika leo Alfajiri mida ya saa kumi kimewavua rasmi baadhi ya viongozi wake.

Waliovuliwa vyeo ni Zitto Kabwe, ambaye amevuliwa nafasi ya naibu katibu mkuu wa chama pamoja na nafasi ya naibu kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Dr. Kitila Mkumbo yeye amevuliwa nafasi ya mjumbe wa kamati kuu.

Wakati tunasubiri taharifa ya kurugenzi ya mawasiliano ya chama hicho kwa vyombo vya habari , taharifa zaidi zinadai viongozi hao waliyovuliwa wamepewa siku 14 wajieleze kwanini wasifukuzwe uanachama.

MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHER SASA VITANI KUMSAFISHA KAPUYA.

 • YATUMIA MBINU CHAFU NA VITISHO.

 • YAUKWEPA UKWELI NA USHAHIDI ULIYO WAZI.

Kwa tafsiri yoyote ile, uandishi uliofanywa na magazeti ya UDAKU ya Global Publisher juu ya Binti anayesadikiwa kubakwa na Prof. Kapuya unatia shaka huku ukionyesha nia ya kumsafisha waziri huyo wa zamani.

Kutokana na Nyadhifa huku Prof. Kapuya ni mwajiriwa wa wananchi ambaye fedha zetu za kodi ndizo zinazotumika kumlipia mshahara yeye ni anapaswa kumulikwa zaidi ya mtoto huyo.

Tofauti na Nyadhifa hizo bado nafasi ya Kapuya kama kiongozi wa familia ambaye anatakiwa kuwa mfano kwa maadili kwa  Jamii husika apaswi kukwepa hili kwa namna yoyote hile.

Mambo Muhimu ya kujadiliwa ni:-

 1. Mwezi Februari mwaka huu, inadaiwa mtu asiyefahamika alienda nyumbani kwa watoto hao na kutelekeza gari aina ya T.199 BGY Mercedes Benzi ya Blue wakati wanafunzi hao wakiwa shuleni, kisha kuacha ufunguo kwa jirani yao kwa maelekezo kuwa wakifika awapatie.
 2. Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, 24 Januari 2013, alifika mtu nyumbani kwao mtu mmoja (jina tunalihifadhi) na kujitambulisha kuwa yeye ni jambazi na kuwa alitumwa kwenda kuwaua

Hapa tunataka ukweli nani anamiliki gari hii, na alikuwa anatuma la nini gari kwa watoto mdogo hawa??.

Ikumbukwe kuwa kama Prof Kapuya haukuwatuma majambazi hawa kwa nini anaendelea kutuma msg za kutishia kua???? 

 1. Alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake ya mkononi yenye namba 0784993930, Profesa Kapuya alituma ujumbe ufuatao kwa mtoto huyo: “chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?” Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: “Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu.

 2. “Mwambieni Mbowe mwenye hilo gazeti awape nyumba ya kuishi. Si mmemuingizia hela leo? Mnatumika bure watu wanaingiza hela nyingi, mmenitibua lazima niwauwe wiki hiii haitaisha, nitapanga kambi popote. “Jana si wamekuficha? Tuone kama utalindwa milele. Kazi ya kulindwa imeisha, maana wameshatengeneza hela. Lazima mvae sanda. Hilo sio ombi, ni wajibu wenu. Mnajitia mafia watoto sio? Watoto wetu wanauza unga, nani anawakamata? Nani atapigana nasi?”

Maneno haya yametolewa na Prof Kapuya tena kupitia simu yake na ushihidi umethibishwa na TCRA kwamba Prof Kapuya ametukana na kutishia kuua.

Kwa ufupi hapa Prof Kapuya hajamtishia Binti huyo peke yake bali kawatishia na waandishi Jambo ambalo ni hatari.

Swali ni kwanini Kapuya anawatishia waandishi wa Tanzania Daima na hawatishii waandishi wa Global Publisher???? Ni kwanini waandishi wa Global wafanye harassment wakati wa kumuhoji binti huyo???

Ni kweli wiki aijahisha je kauli ya prof ya kuwamaliza kabla ya wiki ndiyo hii ya kupitia Global Publisher?

 1. Mwanafunzi huyo alisema baada ya kutambulishwa kwa Prof. aliitwa katika hoteli moja jijini Dar ambapo baada ya kufika mapokezi wafanyakazi wa hoteli hiyo walimkataza kuingia chumbani katika maana kwamba umri wake alikuwa mdogo (mwaka 2011 alikuwa na miaka 14), lakini Kapuya aliamrisha aje chumbani pamoja na dereva na kumwingiza kwa nguvu. Akiwa chumbani alimlazimisha kulala naye kisha kumpa sh laki saba, badala ya sh elfu sitini na saba kiasi ambacho kilikuwa ndio mahitaji halisi ya ada. 

 2. Mwanafunzi huyo amesema baada ya muhula mmoja aliitwa tena na mbunge huyo katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala tarehe 3 June 2012, ambapo pia alimlazimisha kulala naye kwenye zulia la ofisi yake, kisha kumpa sh 350,000/.

 3. Alisimulia kwamba wakati anatoka kwa huzuni ofisini kwa mbunge huyo, mmoja wa wahudumu wa hapo alimuuliza kwanini anatoka kwa huzuni, alimweleza kisa hicho, na huyo mama aliangua kilio kwa kumwambia “mwanangu umekufa pole tu, huyu baba ni muathirika wa ukimwi”. Aliongeza kuwa baada ya kuambiwa vile alilia na kufanya fujo hapo mapokezi hadi alipokamatwa na walinzi wa kisha kupelekwa kituo cha polisi kufunguliwa mashtaka, lakini akiwa polisi alipoeleza mkasa wote, Polisi walilazimika kumwita Kapuya na wakawasuluhisha kwa makubaliano kwamba Kapuya atakuwa anamlipia ada, na kumpa pesa za matumizi sh. laki tatu kila mwezi, jambo ambalo amekuwa akilitekeleza kupitia simu yake ya mkononi 0755993930. Ujumbe huo kutoka simu namba 0784993930 inayomilikiwa na Kapuya kwenda kwa namba inayomilikiwa na binti huyo, unasomeka hivi: “Ni lazima nitakuua wewe na ndugu yako na atakaetaka kuwasaidia, huyo Samweli Sita asijiingize kwenu, yaani nitakuua tena sijui leo mtalala wapi! We unadhani nani atakayenifunga? Ndo nishakupa ukimwi, sasa nakutaka uache mara moja kuongea na mtu, nitakuwinda popote tuone!” inasomeka sehemu ya ujumbe huo unaodaiwa kutoka kwa Kapuya.

Katika kuthibitisha kwamba Kapuya amekuwa na mawasiliano na binti huyo na kwamba anamjua tofauti na anavyodai kuwa hamjui, gazeti hili limenasa mawasiliano ya kutumiana fedha kutoka kwa Kapuya kwenda kwa binti huyo.Baadhi ya mawasiliano hayo ni pamoja na yale yaliyofanyika Agosti 31 mwaka huu kupitia simu ya Kapuya ambapo alituma sh 300,000 kwenda kwa binti huyo kama sehemu ya makubaliano ya kutuma pesa kila mwezi kwa ajili ya matunzo.

Mawasiliano hayo ni kama ifuatavyo: Juma Kapuya(0755993930)R93NY448 Imethibitishwa Umepokea Tsh505,000  kutoka kwa JUMA KAPUYA. Tarehe 21/6/13 saa 11:07 AM Salio lako la M-PESA ni Tsh 505,000.

U26UG365. Imethibitishwa Umepokea Tsh 300,000 kutoka kwa JUMA KAPUYA Tarehe 31/8/13 saa 3:28 PM Salio lako la M-PESA ni Tsh 300,000 

V04EU470 Imethibitishwa Umepokea Tsh 400,000 kutoka kwa JUMA KAPUYA Tarehe 24/9/13 saa 2:38 PM Salio lako la M-PESA ni Tsh 400,040

First Name: Prof. Juma
Middle Name: Athumani
Last Name: Kapuya
Member Type: Constituency Member
Constituent: Urambo Magharibi
Political Party: CCM
Office Location: P.O. Box 11365, Dar es Salaam
Office Phone: +255 784 993930/+255 776 784185
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail: jkapuya@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Date of Birth 22 June 1945
University College of Wales Aberystwyth
PhD (Botany)
1972
1975
PHD
University of Dar es Salaam
MSc. (Botany)
1971
1972
MASTERS DEGREE
University of Dar es Salaam
BSc. (Education) Hons
1968
1971
GRADUATE
Katholicke University, Nijmegen
Certificate
1982
1983
CERTIFICATE
International Atomic Energy Agency
Certificate
1986
1986
CERTIFICATE

MAMBO YA KUJIULIZA

 1. Kapuya anasema huyo Binti ni mtu mzima nayeye amegundua hilo sasa kwa nini anaendelea kusadia mtu mzima wakati tayari ameshagundua hilo.

 2. Kapuya anasema Binti ni tapeli sasa kwa nini anaendelea kumutumia msg tapeli?? Anaendelea kumtumia M-Pesa mtu tapeli???

 3. Kwa nini akubali harakaharaka kuwa Binti ni tapeli???

 4. Kama kapuya ambaye ni Prof na aliyewahi kuwa waziri anaweza kutapeliwa kirahisi namna hiyo basi nchi hii ipo Gizani!!!

 5. Ni kwa nini serikali isichukue hatua kwa lugha za vitisho za kuua zinazotolewa na Mtu wao???

 6. Kwa nini Bi Helen Bisimba yupo Kimya kwa vitisho vya mauaji kama haya???.

ZITTO SASA KUWATAJA VIONGOZI WENYE FEDHA NJE YA NCHI

Mbunge wa kigoma kaskazini, Naibu katibu Mkuu (CHADEMA) Zitto Kabwe

Mbunge wa kigoma kaskazini, Naibu katibu Mkuu (CHADEMA) Zitto Kabwe

Baada ya kutembea na list mfukoni kwa miaka, Mh. Zitto amefunguka, amesema yupo tayari hata kuuawa kama sababu yenyewe ni kuokoa fedha za watanzania. Amekiri kuwa walioficha fedha nje wamezorotesha uchumi wa nchi. Zitto atawataja Mafisadi na wezi walioficha fedha nje kwenye kikao kijacho cha bunge.

Tunampongeza kwa ujasiri huo, atleast anaweza kurudisha imani kwa wananchi.

Zitto amesema hatuwezi kukomboa nchi hii bila chadema, mambo yanayotokea kamati kuu itafanya jitihada kuyamaliza ili tuwatetee watanzania.

Kumtaja Mwizi hadharani haihitaji itifaki.

source: DW

CHADEMA KUWEKANA SAWA LEO UBUNGO PLAZA.

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA chini ya M/Kiti wake Mh. Freeman Mbowe inatarajiwa kukutana kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 20-21/11/2013 katika Hotel ya Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam.

Kamati Kuu hii ni ya kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ambapo pamoja na mambo mengine inatarajia kupokea taarifa za utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya kikao cha Kamati Kuu iliyopita.

Taarifa hii inaweza kuchukuliwa kuwa ni afueni kwa chama hicho ili kuondoa hali ya sintofahamu iiliyo jidhihirisha hivi karibuni.

Mimi nawashauri viongozi wa Juu wa Chadema katika agenda zao wasije wakasahau kujadili Barua ya Siri ya CHADEMA kuhusu Zito Kabwe kuchafuliwa,kesi ya Mwigamba na John Shibuda Madale.

MASIKINI KAPUYA, TAMWA, TGNP NA LHRC WAMWANDAMA

Mh. Kapuya hakiwa katika moja ya harakati zake za kula raha... mkono wa prof. unaelekea wapi? kweli majanga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa,Valerie Msoka Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na Kituo cha Msaada wa Kisheria (LHRC), kimelaani viongozi wanaotumia madaraka yao, nafasi zao na nguvu zao kisiasa kuwadhalilisha watoto wa kike.

Mashirika hayo yanayotetea haki za wanawake na watoto, yamesema yamesikitishwa na habari zilizozoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu wasichana wawili wanaotafuta haki yao dhidi ya kiongozi wa kiserikali anayetuhumiwa kuwadhalilisha.

“Mashirika hayo yanafahamu kuwa vitisho vilivyotolewa na kiongozi huyo vimewasababishia wasichana hao kuogopa kuishi nyumbani kwao kwa kuhofia maisha yao,” ilisema sehamu ya taarifa ya pamoja ya mashirika hayo.

Iliongeza: “Tunashangazwa kuona hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na mamlaka husika wakati wasichana hao wakitafuta msaada,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Valerie Msoka, katika taarifa hiyo.

Masharika hayo yametoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kuwalinda wasichana hao dhidi ya mtuhumiwa.

Aidha, ili kujenga imani na utawala bora, mashirika hayo yamemtaka mbunge huyo kujiuzulu mara moja.

Alisema Tamwa, TGNP na LHRC, yanawataka Watanzania kuungana na kupinga viongozi wanaotumia madaraka yao vibaya. Watanzania wapige vita vitendo visivyo vya haki kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheri.

Prof. Hakiwa katika mawindo yake huku akitathimini mizigo....

CHANZO: NIPASHE

POLISI WAMWAMULU ZITTO KUFIKA POLISI KWA MAOJIANO….

Hiyo ndiyo barua ya polisi kwa Kabwe Zuberi Zitto iliyo muhamulu kufika polisi kwa maojiano

Hiyo ndiyo barua ya polisi kwa Kabwe Zuberi Zitto iliyo muhamulu kufika polisi kwa maojiano

Leo kuna uvumi amao ulizaga kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Maendeleo na Demoklasia (CHADEMA) Kabwe Zuberi Zitto kwenda kwa ridha yake polisi makao makuu kuandika maelezo kwa kile anachoita ripoti ya siri. Ukweli ni kuwa Zitto aliandikiwa barua na polisi makao makuu kufuatia kuchapishwa kwa habari katika gazeti la majira toleo la tarehe 11/11/2013. Polisi wamefungua jarada “SAKATA LA UFISADI: ZITTO NATISHIWA MAISHA” na siyo “ripoti ya siri” kama aliyoandika kwenye kwenye mitandao mengi ya kijamii.

Mbunge wa Kigoma Kaskazni ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demoklasia na maendeleo (CHADEMA) Kabwe Zuberi Zitto akiwa polisi akitoa maelezo.

Mbunge wa Kigoma Kaskazni ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demoklasia na maendeleo (CHADEMA) Kabwe Zuberi Zitto akiwa polisi akitoa maelezo.

BURIANI Dr. SENGODO MVUNGI

Picha hii ilipigwa baada ya marehemu kufikishwa hospitali kutokana na majeraha haliyopata kufwatia kipigo kutoka kwa watu wasio julikana maeneo ya nyumbani kwake, hata hivyo polisi wamesema wanawashikilia watu tisa kutokana na mkasaa huo

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyekuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid leo jioni (Jumanne, Novemba 12, 2013), Dkt. Sendongo Mvungi majira ya saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya Milpark.

“Kwa masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg-nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo (Jumanne, Novemba 12, 2013) saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini,” amesema Bw. Rashid katika taarifa yake fupi ya awali.

“Taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini kwa mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa kesho (Jumatano, Novemba 13, 2013),” ameongeza.

Marehemu Dkt. Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.

Katika taarifa yake, Tume pia imewaomba watanzania wote kuungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dkt. Mvungi katika kuomboleza msiba huo.

CHADEMA WATOA RAMBIRAMBI

Quote By Kurugenzi ya Habari View Post
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ametuma salaam za rambirambi ya kifo cha Dkt. Edmund Sengondo Mvungi, akitoa pole kwa familia, uongozi na wanachama wa NCCR-Mageuzi, Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya na wananchi wote walioguswa na msiba huo.Akitoa kauli hiyo kwa niaba ya CHADEMA na wanachama wa chama hicho, Mwenyekiti Mbowe amesema kuwa amepokea kwa masikitiko na mshituko mkubwa taarifa za kifo cha Dkt. Mvungi, akimwelezea kuwa alikuwa mwanasiasa mwenye msimamo ambaye hakuwahi kutetereka kusimama na chama chake tangu alipojiunga nacho na kuanza kushiriki siasa za mageuzi nchini.“Kwa niaba ya CHADEMA na wanachama wetu nchi nzima, napenda kutoa salaam za pole sana kwa familia ya marehemu, mjane na watoto. Natoa pole kwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na wanachama wa chama hicho, pia tunatoa pole kwa Jaji Mstaafu Joseph Warioba na makamishna wote wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwakifo cha Dkt. Mvungi. Tunaomba Mwenyezi Mungu awatie nguvu sana wakati huu wa majaribu na majonzi makubwa.

“Dkt. Mvungi alikuwa mwanasiasa mwenye misimamo ambaye hakuwahi kukihama chama chake tangu alipoanza siasa za mageuzi nchini. Ni kati ya wasomi wachache waliokuwa na ujasiri na kuthubutu kujiunga na vyama vya upinzani tangu mapema.

“Mvungi pia alikuwa mmoja wa wanasiasa wa mwanzo kabisa kupigania nchi yetu iwe na Katiba Mpya, ili hatimaye siasa zetu, hususan demokrasia ya vyama vingi nchini iendeshwe kwa misingi iliyo imara,” amesema Mwenyekiti Mbowe na kuongeza;

“Mwenyezi Mungu alimjalia marehemu akaweza kushiriki kutimiza ndoto hiyo baada ya kuteuliwa kuwa mmoja wa makamishna wa Tume ya Mpya, kazi ambayo ameifanya hadi siku alipokutwa na tukio lililosababisha mauti yake.”

Mwenyekiti Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, amesisitiza kuwa kwa namna ambavyo Dkt. Mvungi alikuwa mstari wa mbele katika suala hilo, Tume ya Katiba Mpya inao wajibu wa kuthamini mchango wake katika hatua iliyofikia sasa ya mchakato huo nyeti hadi utakapofika mwisho.

“Wakati tukimwombea marehemu kwa Mungu, alazwe mahali pema peponi, ni matumaini yetu kuwa serikali kupitia vyombo vyake itahakikisha kuwa wale wote waliohusika katika tukio la lililosababisha kukatisha uhai wa Dkt. Mvungi wanapatikana na kuchukuliwa hatua zote zinazostahili kisheria,” amesema Mwenyekiti Mbowe.

Hizi picha hapa chini ni za Wafanyakazi wenzake baada ya kupata taarifa za msiba ofisini.
kifo cha Sengondo Mvungi Nov 12 2013 2

kifo cha Sengondo Mvungi Nov 12 2013

KITILA MKUMBO AJITOKEZA NA UFAFANUZI JUU YA SHUTUMA ZANAZOMKABILI

Dk. Kitila Mkumbo ni Mhadhiri Mwandamizi katika Saikolojia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa UDASA.

Dk. Kitila Mkumbo pichani ni Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, Mhadhiri Mwandamizi katika Saikolojia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa UDASA.

Kufuatia taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuhongwa kwa Zitto naye kuhonga watu wengine, nikiwemo mimi, ili kutoa siri za chama chetu (CHADEMA) kwa lengo ya kukivuraga watu, wengi sana wameniandikia email, sms na hapa fb ili nitoe ufafanuzi kuhusu ukweli wa mimi kuhongwa na Zitto na mahusiano yangu na mwanasiasa huyu nguli. Mwanzoni nilipuuzia na sikutaka kabisa nitoe maoni kuhusu jambo hili kutokana na kiwango cha ujinga kilichomo ndani ya waraka huo unaosambazwa. Hata hivyo kwa kuwa watu wengi wamenitaka nitoe ufafanuzi, napenda kueleza haya yafuatayo:

i) Mimi Kitila Mkumbo, pamoja na umaskini wangu, sijawahi kuhongwa popote na sitarajii kuhongwa. Taarifa zinazosambazwa juu yangu ni za uwongo wa kijinga na uzushi wa kitoto kwa malengo ya siasa nyepesi. Ni wazi kwamba wanaosambaza habari chafu juu yangu hawanijui na ndiyo maana wanaweza kudiriki kuzusha kwamba mie Kitila Mkumbo naweza kuhongwa sh. 200,000/=. Hakuna namna nyingine ya kuthibitisha kwamba waraka huu na maudhui yake ni mambo ya kutunga zaidi ya hilo la kuzusha kwamba nami ni miongoni mwa watu waliohongwa.

ii) Kuhusu mahusiano yangu na Zitto ni kwamba kijana huyu ni rafiki yangu wa miaka mingi tuliyejuana na kuanza urafiki kabla ya hata mie kuijua CHADEMA. Urafiki wetu ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo ndani na/au nje ya siasa. Wasiopenda hili poleni sana. Mie ni mtu mzima na hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kunichagulia marafiki na/au maadui.

iii) Wanaosambaza waraka huu ni watu woga wa demokrasia na wasioijua CHADEMA. Chama hiki kimejipambanua kwa miaka mingi kwamba ni chama kinachopigania demokrasia ndani na nje ya chama. Matatizo yetu hushughulikiwa kikamilifu ndani ya vikao ambapo huwa tunajadili mambo kwa upana. Watu wenye makosa husutwa, huonywa na ikibidi huadhibiwa. Kama kweli haya yanayosambazwa yangekuwa na hata chembe ya ukweli, na kama kweli waraka huu umetoka makao makuu ya chama, sioni ni kwa nini jambo hili zito kiasi hiki haliletwi kwenye vikao vya chama na sisi tunaotuhumiwa kukivuruga chama tushughulikiwe kwa mujibu wa taratibu kama ambavyo watu wengi wamewahi kushughulikiwa ndani ya chama chetu kwa makosa waliyotenda.

iv) Ni vizuri tukajenga utamaduni wa kuhoji mambo badala ya kuyameza kana kwamba tunasoma msaafu. Hivi huyo mtu anayemhonga Zitto bilioni mbili (2,000,000,000) ili atoe siri za chama, ni siri gani hizo ambacho chama cha siasa kinazo ambazo ni za hatari hata itolewe hongo kama hiyo?

v) Ninasikitishwa na idara ya uenezi wa chama chetu kukaa kimya bila kutoa maelezo juu ya jambo hili, hasa pale ambapo tumeambiwa waraka huu umetoka makao makuu. Hii si kawaida kwa idara yetu hii nyeti iliyosheheni watu mahiri. Mara zote huwa wepesi kabisa kwa vijana wetu katika idara hii kutoa ufafanuzi, tena kwa mambo mepesi kabisa yanayokigusa chama, vipi makamanda kwenye jambo hili imekuwaje?

v) Mwisho kama kuna watu walidhani kwamba kwa uzushi huu watanikatisha tamaa na kunirudisha nyuma katika kutoa mchango wangu wa kuimarisha siasa ya vyama vingi hapa nchini, na kuijenga CHADEMA kama chama mbadala imara wamekosea. Nipo imara na nitaendelea kutoa mchango wangu kikamilifu. Poleni sana wote mliokwazwa na jambo na ufafanuzi wangu ndio huo.