DIAMOND KUWASHA MOTO ARUSHA “USIKU WA WASAFI”

diamond.....
Msanii  maarufu wa muziki wa Kizazi kipya Diamond Platnum anatarajiwa kufanya  shoo ya aina yake jijini  Arusha  siku ya Jumamosi  ya  tarehe 30 katika viwanja vya Hoteli ya Mount Meru ijulikanayo kama “ usiku wa wasafi”
 
Muandaaji wa shoo hiyo,Mkurugenzi wa kampuni ya Mwandago Investment Faustine Mwandago akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Arusha jana alisema kuwa maandalizi  ya awali ya shoo hiyo yamekamilika kwa kiasi kikubwa 
 
Mwandago alisema kuwa  shoo hiyo itakuwa ya kukata na shoka  na itawapa burudani ya kutosha mashabiki wa msanii huyohivyo kuwataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi siku ya jumamosi
 
 “kwa hapa Arusha Diamond tumezoea kumuona  kwenye shoo za Mamiss kama Miss Arusha na nyinginezo lakini kwa sasa hivi anakuja kwa ajili ya kutoa burudani tu kwa mashabiki wake hivyo naamini kuwa shoo hiyo itakata kiu kwa watakaohudhuria.”alisema mwandago
 
Mbali na burudani kutoka kwa msanii huyo wasanii chipukizi kutoka jijini hapa watapata nafasi ya kumiliki jukwaa hali itakayopelekea vipaji vyao kutambulika
Wasanii hao chipukizi ni Marry,Kandisi,Roggerz na madansa wa boda 2 boda waliopo chini ya Mwandago Investment watapamba shoo hiyo.
 
Katika kunogesha shoo ya Diamond  dress code itakuwa vazi jeupe kuendana na jina la shoo la Usiku wa Wasafi
Advertisements