HALA HALA ARUSHA! CHADEMA WASUSIA UPATANISHI

CHADEMA
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimesusia upatanisho wa Serikali ya CCM kuwaingiza kwenye maridhiano ya amani yasiyo na tija kwa umma na taifa.

Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Mutungi aliandika barua kuhusu maridhiano ya amani kati ya vyama vya siasa, polisi, na taasisi za kidini pamoja na wananchi wa Arusha.

Taharifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema Chadema kama chama cha siasa na kama taasisi inayoitumikia jamii kinatambua nia njema kabisa ya Jaji Mutungi, na inamuunga mkono kufanya maridhiano haya yanayogusa jamii.
Hata hivyo nia hii njema ya jaji Mutungi imetiwa doa tena mbaya kabisa na serikali ya ccm na jeshi la polisi. Tukianzia na Jeshi la polisi ambalo ni sehemu ya maridhiano ya amani, december 4 walifanya uchunguzi wa tukio la kuchomwa moto ofisi yaa chadema mkoa wa Arusha, habari za uhakika zinadai kabla hata hawajamaliza uchunguzi wakaitisha mkutano na waandishi wa habari, wakatoa taarifa za uchunguzi ambayo ilionekana kutokamilika, taarifa iliyoonyesha udaifu na kuidhalilisha jeshi la polisi. Kwa taarifa ambayo jeshi la polisi imetoa  inaonyesha chadema wameichoma ofisi yao wenyewe, yaani mchezo ule ule wa kusema chadema walijilipua wenyewe Soweto, Kijana Ally Zona(RIP) aliuawa na kitu chenye ncha kali, Daudi Mwangosi (RIP) alirushiwa kitu chenye ncha kali …………
Serikali ya ccm kwa upande wake ilitegemea maridhiano/mapatano ya Jumamosi yawe sehemu ya chadema kumtambua meya Gaudence Lyimo, meya ambaye alichaguliwa kwa njia ya hila, meya ambaye ndiye chanzo cha mauaji ya January 5 2011, meya ambaye ni chanzo cha kufukuzwa kwa madiwani wetu Arusha, meya ambaye ni chanzo cha mlipuko wa bomu soweto, eti chadema tukae meza moja na ccm!!!!

Nia na dhamira ya CHADEMA ni kila mtanzania kuwa na amani, lakini amani haiji bila kuwa na haki, kwani CHADEMA inatambua kuwa Amani ni tunda la haki, na kwamba CHADEMA itaendelea kupigania haki ya watanzania wote wakati wote ili wawe na amani.

Hata hivyo kwa taarifa nilizopata ni kwamba chadema itaandika barua kwa taasisi zote za dini na za kiraia kuelezea sababu za msingi za kususia mkutano wa Msajili unaohusu upatanishi baada ya kutiwa doa na serikali ya ccm.

CHADEMA inatamka kwamba kabla ya wao kukutanishwa na ccm mambo yafuatayo yafanywe:
1. Meya feki ajiuzulu ili uchaguzi wa haki ufanyike,
2. Serikali iwawajibishe wale wote waliolipua bomu na kupiga risasi za moto soweto Arusha,
3. Serikali itueleze mabomu yaliyotumika soweto yalitoka wapi na yaliingia vipi nchini, na kwa makusudi gani, nani aliingiza, na hatua gani anatakiwa kuchukuliwa.
4. Serikali iwachukulie hatua polisi wote waliowaua raia kwenye mauaji ya Jan 5 2011
5. Serikali iwashushe vyeo polisi wote waliopandoishwa vyeo baada ya kutekeleza mauaji ya raia ya january 5, mauaji ya Daudi Mwangosi na mauaji ya kijana Ally Zona aliyeuawa Morogoro na maeneo mengine ambayo polisi wametekeleza mauaji ya raia wasio na hatia, halafu wapelekwe mahakamani.

Baada ya hapo CHADEMA watakuwa tayari kukaa meza moja na ccm.

Kwa habari zaidi CHADEMA Arusha watazungumza na waandishi wa habari kuelezea zaidi

Advertisements

KICHUPA KIPYA KABISA CHA GAL BLADDER – BABY MADAHA

Tazama kichupa kipya kabisa cha  mwana dada Baby Madaha kiitwacho Gal Bladder, ikiwa ni soundtrack ya upcoming movie iitwayo Gal Bladder pia, ambayo msanii huyu mahiri atakuwa kama main character katika movie hiyo ambayo ipo katika maandalizi ya mwisho mwisho.

KIKWETE ZIARANI TENA UGHAIBUNI

Jakaya-Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wiki hii atahudhuria mikutano miwili mikubwa ya kimataifa ukiwamo wa kujadili amani na usalama Barani Afrika kwa mwaliko wa Rais Francois Hollande wa Ufaransa.

Rais Kikwete ambaye aliondoka nchini usiku wa kuamkia leo, Jumatano, Desemba 4, 2013, atakuwa mmoja wa viongozi wa Afrika ambao watahudhuria Mkutano Kati ya Marais wa Afrika na Ufaransa, ambao utafanyika kwa siku mbili katika Kasri ya Elysee mjini Paris kuanzia keshokutwa Ijumaa, Desemba 6, 2013.

Mkutano huo uliopewa jina la Elysee Summit utakuwa ni mkutano wa 26 wa Mikutano ya Wakuu wa Nchi za Afrika na Ufaransa ambao walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 1973 kwa madhumuni ya kuzikutanisha Ufaransa na makoloni yake ya zamani katika Afrika.

Kwa mikutano miwili ya kwanza, washiriki walikuwa ni marais wa nchi za Afrika zilizokuwa makoloni ya Ufaransa lakini mwaka 1976 zilialikwa nchi zinazozungumza lugha ya Kireno katika Afrika kama watazamaji tu.

Mwaka 1981 jina na madhumuni ya mkutano huo yalibadilika na ukaanza kuitwa The Conference of Heads of States and Government of Africa and France na mwaka 1996 mkutano huo ulifunguliwa kwa nchi zote za Afrika bila kujali zinazungumza lugha gani. Awali mkutano huo ulikuwa unafanyika kila baada ya miaka miwili, sasa ni kila baada ya miaka mitatu.

Kama ilivyokuwa mkutano uliopita uliofanyika mwaka 2010 mjini Nice, Ufaransa, mada kuu ya Mkutano huo ni kujadili amani na usalama katika Bara la Afrika vikiwemo vita ndani ya nchi mbalimbali, uharamia kwenye bahari, biashara ya dawa za kulevya, ugaidi na ujambazi wa vikundi na jinsi mambo hayo yanavyoathiri Afrika na Ufaransa.

Aidha, Mkutano huo utajadili mada nyingine mbili ambazo ni Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo na Mabadiliko ya Tabia Nchi.

Rais Kikwete na mwenyeji wa Mkutano huo, Rais Hollande watakuwa Wenyeviti-Wenza wa kikao kitakachojadili madhara ya Mabadiliko ya Tabia Nchi. Rais Kikwete atakuwa Mwenyekiti-Mwenza wa kikao hicho katika nafasi yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU) Juu ya Mabadiliko ya Tabia Nchi (CAHOSCC).

Rais Kikwete anatarajiwa kuwaeleza viongozi wenzake matokeo ya Mkutano wa COP19/CMP9 uliofanyika karibuni mjini Warsaw, Poland kujadili suala zima la Madhara ya Mabadiliko ya Tabia Nchi.

Mkutano mwingine mkubwa ambao Rais Kikwete atahudhuria ni ule wa marais wa Afrika utakaojadili jinsi ya Jumuiya ya Kimataifa inavyoweza kushirikiana kukomesha ujangili na biashara haramu ya pembe za tembo na faru.

Katika Mkutano huo utakaofanyika Hoteli ya de la Marine, Rais Kikwete aanatarajiwa kuwaeleza viongozi wenzake kuhusu hatua ambazo zinachukuliwa na Serikali yake kukabiliana na ujangili nchini chini ya Operesheni Tokomeza.

NJIA NYEUPE KWA WATENGENEZAJI WA FILAMU WA KITANZANIA KUUZA KAZI ZAO KWENYE MITANDAO

IMG_7030

MKurugenzi wa Kampuni ya Blue Sky, Richard Signeski (kulia), akizungumza  na waandishi wa habari (hawapo pichani), katika ukumbi Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam  kuhusu ushirkiano walioingia na  Kampuni ya Status Communications ya nchini kuwawezesha waandaaji filamu nchini kuuza filamu zao  kwenye mitandao ya kijamii. Kushoto ni Mwakilishi wa Status Communication, Monalisa Shayo.

IMG_7022

Omar Salisbury akizungumza na waandishi wa habari.

Kampuni ya Status Communications imetangaza ushirikiano na kampuni ya usambazaji wa filamu ya Kimarekani Blue Sky Media ili kuwawezesha kuuza filamu kwenye mitandao ya ITunes, Microsoft, You Tube, RAIN na mitandao mingine ya kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Blue Sky, Richard Signeski alisema ushirikiano huu utawafanya watengeneza filamu kutoka Afrika Mashaaiki na kati kuweza kuuza filamu moja kwa moja kwenye mitandao mikubwa ya usambaji dunia nzima.

‘’Lengo la ushirikiano huu ni kuwapa watengeneza filamu kutoka Afrika mashariki na kati kuweza kuuza filamu zao moja kwa moja kwa watazamaji dunia nzima’’ alisema Signeski.

Mwakilishi wa Status Communications, Monalisa Shayo alisema ushirikiano wao na Blue Sky ni moja ya tu ya ushirikano na makampuni ya kimataifa wanaotaka kuingia katika soko la Afrika Mashariki.

 ‘’Mwaka 2013 umekuwa mwaka muhimu kwa Status Communications kwani tumeweza kuingia mikataba na makampuni mbalimbali ili kuweza kuingia soko la Afrika Mashariki’’ alisema Monalisa.

‘’Mwanzoni mwa mwaka huu tumeingia mikataba na makampuni kama Media Zone Authority  ya Abu Dhabi (twofour54) pamoja na Qatar’s Media Group International pamoja na Visual Unity ya Abu Dhabi ili kuwawakilisha kwenye masoko yao kwenye miji kama ya Prague’ alisisitiza Monalisa wa Status Communications.

‘’Fursa hii ni muhimu kwa watengeneza filamu wa Afrika Mashariki kuuza filamu kwenye masoko tofauti duniani’’ alisema Monalisa.

Akielezea sababu za kuja nchini, Signeski alisema alichokigundua hapa nchini ni kuwa watengeneza filamu wengi wanahofia kuwekeza fedha nyingi kwenye utengenezaji wa filamu zao kwani wanahofia uchache wamasoko ya kuuza filamu zao.

‘’Hivyo nawaomba watengeneza filamu mjitokeze kwa wingi ili muweze kuuza filamu dunia nzima kwa urahisi’’ alimaliza Signeski.

NDEREMO ZILITAWALA MBALALI MBEYA NI BAADA YA DKT. ASHA MIGIRO KUTEULIWA KUWA MBUNGE

 Dk. Migiro (kulia), akipongezwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa uteuzi wake huo.
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipongezwa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mbunge.
 Dk. Migiro akizungumza na vyombo vya habari, jinsi alivyopokea kwa furaha uteuzi wake huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimpongeza Dk. Migiro kwa kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mbunge.
(Picha zote kwaisani ya Kamanda wa Matukio)

DKT. SLAA AITEKA KAHAMA, WANANCHI WAMNGOJA KWA ZAIDI YA MASAA 4

  • Ni katika ziara ya siku 20 ya kuimarisha chama
  • Sababu ya kuchelewa zaelezwa ni magari ya msafara wake kuwekewa mafuta ya kuchakachuliwa.
  • Asema CHADEMA kiko imara na kinaweza kusimamia misingi yake bila shaka yoyote.

Ziara ya Dk. Slaa imeanza  jana Mjini Kahama kwa kuhutubia mkutano wa Hadhara katika viwanja vya CDT. Dkt. Slaa ambaye ameanza ziara akitokea Dar es salaam alichelewa kuanza mkutano huku watu wengi wakimgonja toka saa 8 mchana.

Sababu ya kuchelewa ameeleza kuwa imetokana na Magari yake ya Msafara kuwekewa mafuta yaliyochakachuliwa Kibaha, hivyo kumfanya kuingia Kahama majira ya 12:08 jioni lakini bado umati wa watu ulikuwa ukimgonja.


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilibrod Slaa akiwahutubia wanachi wa mji wa Kamaha na vitongoji vyake, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua na kuimarisja uhai wa chama katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida, uliofanyika kwenye Uwanja wa CDT mjini Kahama jana. (Picha na Joseph Senga)


Katibu Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema), Dk. Willibrod Slaa akiagana na wananchi wa mji wa Kahama baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa CDT mjini huo jana, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Kigoma na Singida. (Picha na Joseph Senga)

Quote By Kurugenzi ya Habari View Post
Dkt. Slaa “Watanzania tulieni, tulieni, tulieni. Wingi wenu hapa na kunisubiri kwa muda mrefu namna hii tangu mchana kwenye jua kali ni ishara kubwa ya upendo wa dhati kwa chama chenu na viongozi wenu, asanteni sana sana sana Kahama.“Chama hiki ni chenu, kipo kwa ajili ya kuwatumikia na kusimamia maslahi na matakwa yenu. Hakiwezi kuwa chama legelege. Ni lazima ili kiweze kuwasemea watu, kwanza muhimu kiweze kusimamia misingi yake, ikiwemo katiba, kanuni, maadili na itifaki, mambo ambao hata CCM hawana pamoja na ukongwe wao.’

“Wakati wa kampeni 2010 tuliwaambia tutasimama kidete kwa ajili yenu kuwavusha kutoka hapa kwenda nchi ya matumaini. Ni lazima mtuone hivyo bila chembe ya shaka kuwa chama chenu ni imara, kinaweza kusimamia misingi yake ambayo ni pamoja na katiba yake, kisha tutakuwa na ubavu wa kupigania maslahi yenu.”

“Haya mambo tunayopitia sasa wapo wanofikiri yatatukwamisha, tunawaambia ndiyo kwanza yanatukomaza na kutuimarisha kuwa chama imara kwenda kushika dola,” Dkt. Slaa leo mjini Kahama.