HALA HALA ARUSHA! CHADEMA WASUSIA UPATANISHI

CHADEMA
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimesusia upatanisho wa Serikali ya CCM kuwaingiza kwenye maridhiano ya amani yasiyo na tija kwa umma na taifa.

Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Mutungi aliandika barua kuhusu maridhiano ya amani kati ya vyama vya siasa, polisi, na taasisi za kidini pamoja na wananchi wa Arusha.

Taharifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema Chadema kama chama cha siasa na kama taasisi inayoitumikia jamii kinatambua nia njema kabisa ya Jaji Mutungi, na inamuunga mkono kufanya maridhiano haya yanayogusa jamii.
Hata hivyo nia hii njema ya jaji Mutungi imetiwa doa tena mbaya kabisa na serikali ya ccm na jeshi la polisi. Tukianzia na Jeshi la polisi ambalo ni sehemu ya maridhiano ya amani, december 4 walifanya uchunguzi wa tukio la kuchomwa moto ofisi yaa chadema mkoa wa Arusha, habari za uhakika zinadai kabla hata hawajamaliza uchunguzi wakaitisha mkutano na waandishi wa habari, wakatoa taarifa za uchunguzi ambayo ilionekana kutokamilika, taarifa iliyoonyesha udaifu na kuidhalilisha jeshi la polisi. Kwa taarifa ambayo jeshi la polisi imetoa  inaonyesha chadema wameichoma ofisi yao wenyewe, yaani mchezo ule ule wa kusema chadema walijilipua wenyewe Soweto, Kijana Ally Zona(RIP) aliuawa na kitu chenye ncha kali, Daudi Mwangosi (RIP) alirushiwa kitu chenye ncha kali …………
Serikali ya ccm kwa upande wake ilitegemea maridhiano/mapatano ya Jumamosi yawe sehemu ya chadema kumtambua meya Gaudence Lyimo, meya ambaye alichaguliwa kwa njia ya hila, meya ambaye ndiye chanzo cha mauaji ya January 5 2011, meya ambaye ni chanzo cha kufukuzwa kwa madiwani wetu Arusha, meya ambaye ni chanzo cha mlipuko wa bomu soweto, eti chadema tukae meza moja na ccm!!!!

Nia na dhamira ya CHADEMA ni kila mtanzania kuwa na amani, lakini amani haiji bila kuwa na haki, kwani CHADEMA inatambua kuwa Amani ni tunda la haki, na kwamba CHADEMA itaendelea kupigania haki ya watanzania wote wakati wote ili wawe na amani.

Hata hivyo kwa taarifa nilizopata ni kwamba chadema itaandika barua kwa taasisi zote za dini na za kiraia kuelezea sababu za msingi za kususia mkutano wa Msajili unaohusu upatanishi baada ya kutiwa doa na serikali ya ccm.

CHADEMA inatamka kwamba kabla ya wao kukutanishwa na ccm mambo yafuatayo yafanywe:
1. Meya feki ajiuzulu ili uchaguzi wa haki ufanyike,
2. Serikali iwawajibishe wale wote waliolipua bomu na kupiga risasi za moto soweto Arusha,
3. Serikali itueleze mabomu yaliyotumika soweto yalitoka wapi na yaliingia vipi nchini, na kwa makusudi gani, nani aliingiza, na hatua gani anatakiwa kuchukuliwa.
4. Serikali iwachukulie hatua polisi wote waliowaua raia kwenye mauaji ya Jan 5 2011
5. Serikali iwashushe vyeo polisi wote waliopandoishwa vyeo baada ya kutekeleza mauaji ya raia ya january 5, mauaji ya Daudi Mwangosi na mauaji ya kijana Ally Zona aliyeuawa Morogoro na maeneo mengine ambayo polisi wametekeleza mauaji ya raia wasio na hatia, halafu wapelekwe mahakamani.

Baada ya hapo CHADEMA watakuwa tayari kukaa meza moja na ccm.

Kwa habari zaidi CHADEMA Arusha watazungumza na waandishi wa habari kuelezea zaidi

Advertisements