ELIMU: MAFUNZO YA U DJ NA FIELD ZA WATANGAZAJI

IMG-20140612-WA0000

Advertisements

LADY JAY DEE AFUNIKA SHOW YA MASAKU RUGBY 7S AFTER PARTY NAIROBI

Lady Jaydee alikuwa mmoja wa wasanii waliotumbuiza kwenye show ya Masaku Rugby 7s After Party lililofanyika Jumamosi jijini Nairobi. Takriban watu 40,000 walihudhuria kwenye show hiyo iliyodhaminiwa na Tusker Lager. Wasanii wengine walitumbuiza ni pamoja na Jua Cali, Radio n Weasel, Wyre, Kidum, Keni wa Maria.

Copy of image

Copy of image(7)

Copy of image(6)

Copy of image(5)

Copy of image(4)

Copy of image(3)

Copy of image(2)

Copy of image(1)

CHADEMA WAJIBU MAPIGO, SASA WAMTAKA CAG KUWEKA WAZI RIPOTI ZA HESABU ZA MAPATO NA MATUMIZI YA VYAMA VYA SIASA

CHADEMA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtaka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuweka wazi ripoti za hesabu za mapato na matumizi ya vyama vyote vya siasa nchini, kwa ajili ya kusimamia misingi ya uwajibikaji.

Kimesema siku zote kimekuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ufisadi ndani na nje ya chama, hivyo kwa upande wake hakina hofu yoyote ya ripoti za ukaguzi wa hesabu hizo kuwekwa wazi.

Pia kimemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kujiandaa kupokea maandamano ya wanachama na viongozi halali wa CHADEMA watakaofika ofisini kwake kumpatia ukweli na kukitetea chama chao dhidi ya propaganda ambazo zimefikishwa kwake na watu kiliodai ni mamluki na masalia ya wasaliti, baada ya viongozi wao kufukuzwa uanachama mapema mwaka huu.

Akizungumza na Tanzania Daima mjini Dodoma jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa chama hicho, John Mnyika, alisema kama Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ameamua kuwa ‘mpokeaji’ wa maandamano, basi ajiandae kwa maandamano makubwa ambayo yatabeba ujumbe wenye hadhi ya CHADEMA badala ya hoja za kipuuzi alizopelekewa hivi karibuni.

Mnyika alikuwa akijibu maswali ya gazeti hili, lililotaka ufafanuzi zaidi kutokana na kauli zake alizotoa mbele ya waandishi wa habari juzi mjini Dodoma alipokuwa akitoa msimamo wa CHADEMA kuhusu madai ya kundi la watu waliofika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini na CAG, wakidai wao ni wajumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa chama hicho.

Kabla ya kwenda ofisi hizo mbili, watu hao walifanya mkutano na waandishi wa habari Juni 23, mwaka huu ambapo pia, bila kuonyesha vielelezo, walidai kuwa wao ni wajumbe wa vikao vya CHADEMA.

Katika hali ambayo inatia shaka uhalali wa ujumbe wao, siku moja baada ya mkutano huo, baadhi ya watu ambao majina yao yalionekana kuandikwa kwenye orodha, walianza kukanusha kuwa hawahusiki na kundi hilo, na kwamba wao ni wanachama watiifu kwa CHADEMA, na kwamba hawajui majina yao na saini zao viliwekwa kwenye orodha hiyo kwa nia gani.

“CHADEMA kama taasisi, si chama cha ufisadi wala ubadhirifu. Ni chama kinachoshirikiana na vyama vingine kuongoza Watanzania kwenye mapambano dhidi ya ufisadi na ubadhirifu. Chama hiki hakiwezi kuvumilia ufisadi na ubadhirifu wa aina yoyote, iwe nje au ndani ya chama, ndiyo maana sisi ndio tuliotaka sheria ibadilishwe, utaratibu ubadilishwe, ili CAG akague mahesabu ya vyama vya siasa.

“Baada ya sheria kutungwa, udhaifu wa Ofisi ya Msajili, Ofisi ya CAG na Serikali ya CCM, umefanya kwa miaka mingi mahesabu yasikaguliwe. Zilipozuka hoja za ukaguzi wa hesabu, mzigo ukitaka kuhamishiwa kwa vyama, kama vile vyama havitaki, tukalielezea suala hili. Hatimaye CAG akafanya ukaguzi.

“Sasa hawa wamemuandikia mkaguzi wakitaka ripoti ya CHADEMA, mimi kama msemaji wa chama, nitoe mwito kwa CAG kuweka wazi ripoti za vyama vyote alivyovikagua.

“Aweke wazi kwa haraka kadiri inavyowezekana. Kwa sababu Bunge limeshaarifiwa kuwa mkaguzi amemaliza kufanya ukaguzi kwa baadhi ya vyama na vingine havijakaguliwa. Vile ambavyo havijakaguliwa vitajwe kwa majina na vikaguliwe. Halafu sasa tuone  hayo madai ya mara Mbowe hivi, mara Slaa hivi,” alisema Mnyika.

“LEO SAA MBOVU IMEPATA MAJIRA?” FID Q

Farid Kubanda ‘Fid Q’

MKALI wa muziki wa hip hop nchini, Farid Kubanda ‘Fid Q’, amesema tuzo za mwaka huu za Kili zilikuwa za mwisho kushiriki endapo waandaaji wasingetambua mchango wake tangu mwaka 2004.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Fid Q alisema miaka mingi amekuwa akishiriki tuzo hizo bila mafanikio yoyote. Kwamba tangu alivyopata mwaka 2004 hajawahi kupewa tena wakati kazi alikuwa anafanya na kuambulia kushiriki tu.

“Sijawahi kumwambia mtu, nilikuwa nasema mwenyewe moyoni na ndiyo maana hata siku ile nilishindwa kuongea nilipotakiwa kuongea, nilitaka kuwauliza leo saa mbovu imepata majira? Lakini nikaona kwa sababu wenyewe wamejiongoza na kuona mchango wangu, basi niwaache tu,” alisema.

Fid Q alisema kutokana na upinzani uliopo katika soko la muziki kwa sasa, wasanii wengi wamekuwa hawapendani, na yeye hana mpango wa kugombana na mtu na anayemchukia hana mpango naye.

“Sijawahi kugombana na msanii yoyote, mimi kila msanii ni mshikaji wangu, ambaye ataona ana chuki na mimi kwa mambo yake binafsi mimi sijali, mimi kila msanii ni ndugu yangu,” alisema.

Fid Q mwaka huu alitwaa tuzo mbili za msanii bora wa kiume hip hop na mtunzi bora wa mashairi ya hip hop.

{PICHA} TUZO ZA WATU ZILIZOFANYIKA JUNE 27 SERENA HOTEL, JIJINI DAR

Picha za Tuzo za watu zilizo fanyika Usiku wa June 27 Jiji Dar Es Salaam katika Hotel ya Serena

Jakobo Steven aka Jb

Jacob Stephen aka JB

B12 Mtangazaji wa Clouds Fm

Mtangazaji wa Clouds FM, B12

Batuli akiwa na Bond

Waigizaji wa filamu, Batuli na Bond

Faraja Nyarandu

Faraja-Nyalandu

Fezza kessi

Feza Kessy

Joshi Murunga na Salama Jabir

Josh Murunga na Salama Jabir

Madam Rita

Madam Rita

Mameneja BabuTale na Mkubwa Fella

Mameneja, Babu Tale na Mkubwa Fela

Mariam Kitosi akiwa na Mmewake Criford Ndimbo

Maryam Kitosi wa Times FM akiwa na mume wake Clifford Ndimbo

Mariam Kitosi Kutoka Time Fm

Maryam Kitosi wa Times FM

Martini Kadinda

Martin Kadinda

Meck Kaloka Muongozaji wa Video

MeckY Kaloka Muongozaji wa Video

Mh.Jerry Slaa

Mh.Jerry Slaa Meya wa Ilala

Millard Ayo wa Clouds Fm

Millard Ayo wa Clouds FM

Mkurugenzi Mtendaji wa Bongo5 Media Nancy Sumari

Mkurugenzi Mtendaji wa Bongo5 Media Group Nancy Sumari

Msanii Asia

Msanii Asia

Mzee King Majuto akiingia

Mzee King Majuto akiingia

Salim Kikeke kutoka BBC Swahili

Salim Kikeke kutoka BBC Swahili

Sammi Misago wa  EA Radio

Sam Misago wa EA Radio

Wastara Juma

Wastara Juma

Young Killer akiwa Rafiki yake

Young Killer akiwa rafiki yake

1

2

5

7

8

9

12

13

18

19

20

27

30

31

CEO Wa Bongo5 Media Luca Neghest

33

35

36

37

38

39

40

42

43

45

46

47

49

50

52

53

54

55

56

57

58

59

//

SERIKALI YALEGEZA MSIMAMO, SASA KUFUTA MISAMAHA YOTE YA KODI

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum.PICHA KUTOKA MAKTABA

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum.PICHA|MAKTABA

Dodoma. Waziri ya Fedha, Saada Salum Mkuya jana aliwasilisha Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2014, ambao umefuta misamaha ya kodi katika maeneo yaliyokuwa yakilalamikiwa na watu wa kada mbalimbali nchini.

Katika muswada huo Serikali imefuta misamaha ya kodi ya mapato inayotokana na  michezo kubahatisha na ukodishaji wa ndege nje ya nchi.

“Muswada umependekeza  waziri husika kutotoa msamaha wa ushuru wa mafuta kwenye mafuta isipokuwa mafuta ya petroli yanayotumika kwenye miradi mbalimbali inayofadhiliwa na washirika wa maendeleo,” alisema Mkuya.

Mkuya alisema kuwa katika muswada huo, Serikali imeondoa saruji, nondo na mabati katika orodha ya bidhaa zinazochukuliwa kuwa ni bidhaa za mtaji ambazo kwa sasa hupata msamaha wa kodi kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

“Lengo ni kuhamasisha uzalishaji wa saruji, nondo na mabati pamoja na kulinda viwanda vya uzalishaji wa bidhaa hizo hapa nchini dhidi ya ushindani wa bidhaa za aina hiyo zinazoingizwa nchini kutoka nje ya nchi,”alisema Mkuya.

Alisema kuwa Serikali imefuta msamaha wa kodi ya mapato yanayotokana na ukodishaji wa ndege nje ya nchi ili kupunguza misamaha isiyokuwa na tija.

“Marekebisho haya yanalenga kutoza mapato yanayotokana na ukodishaji wa ndege nje ya nchi, badala ya kusamehe kodi ya mlipakodi asiye mkazi, ambaye hatimaye hulazimika kulipa kodi itokanayo na mapato hayo nchini kwake,”alisema Mkuya.

Marekebisho hayo yanapendekeza kufuta misamaha ya kodi inayotolewa kwa kampuni ya simu isipokuwa vifaa vya ujenzi wa minara ya simu.

Pamoja na marekebisho hayo muswada huo unapendekeza kuongeza kifungu cha 3(d) ili mtu yoyote asiruhusiwe kutoa misamaha ya kodi kwa miradi nayohusu upanuzi na ukarabati wa miradi inayofanywa na wawekezaji.

Aidha ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji baridi (soda) pamoja na kwenye maji ya matunda (juice), iliyotengezwa kwa matunda yanayozalishwa hapa nchini utabaki kama ulivyo sasa ili kuimarisha viwanda vya ndani.

Mkuya alisema vinywaji baridi vimefanyiwa marekebisho ambapo ushuru kwenye vinywaji hivyo utapunguzwa kutoka Sh 91 kwa lita hadi Sh 55 kwa lita.

{VIDEO} KAMA ULIKOSA SHOW NZIMA YA TUZO ZA WATU ILIYOFANYIKA IJUMAA TAZAMA HAPA.

Tuzo za watu za Tanzania au Tanzania People’s Choice Awards zimetolewa Ijumaa hii kwenye ukumbi uliopo Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Jumla ya vipengele 11 vilikuwa vinashindaniwa. Mshindi katika kila kipengele ameibuka na zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na trophy. Host wa tuzo hizo alikuwa mtangazaji mkongwe wa radio, Jimmy Kabwe.

SAMAHANI KWA USUMBUFU…. LINK YETU NA VIDEO HII INAMATATIZO KWA SASA, MAFUNDI WETU WANASHUGULIKIA SWALA HILO…

WASHINDI

1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA

Millard Ayo – Clouds FM

2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA

Amplifaya – Clouds FM

3.MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA

Salim Kikeke – BBC Swahili

4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA

Mkasi – EATV

5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA

Juma Kaseja – Yanga

6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA

Nisher

7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME

My Number – Diamond

8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE

Yahaya – Lady Jaydee

09. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA

King Majuto

10. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA

Elizabeth ‘Lulu’ Michael

11. FILAMU INAYOPENDWA

Ndoa Yangu

//

VIINGILIO VYA SABASABA MWAKA HUU KULIPWA KWA M-PESA.

001 SABAZMeneja bidhaa na Maendeleo ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Moses Krom  akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusiana na kulipia viingilio kwa njia ya M-Pesa katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)Dar es Salaam yatakayo anza rasmi kesho na kumalizika julai 8 mwaka huu. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Anna Bulando.

003 SABAZKaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Anna  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kulipia viingilio kwa njia ya M-Pesa na usalama katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)Dar es Salaam yatakayo anza rasmi kesho na kumalizika julai 8 mwaka huu. Kulia ni Meneja  bidhaa na Maendeleo ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Moses Krom.

Ni kupitia huduma ya M pesa

-Watu wazima kulipa 2500/- kwa siku na watoto 500/-

-Tiketi za kupaki magari madogo kwa siku ni 4000/-  maroli ni 40000/-

Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania ( TanTrade) imetangaza viingilio vipya vya watu na magari katika maonesho ya kimataifa ya Dar es salaam, (DITF) yatakayoanza tarehe 28 ya mwezi juni hadi tarehe 8 mwezi julai.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Bi. Anna Florence Bulondo amesema viingilio vya mwaka huu havina tofauti na vya mwaka jana lakini sasa yamefanyika maboresho ikiwa ni pamoja na ukataji wa tiketi kwa njia ya Kielectroniki na kwa njia ya M -pesa.

“Viingilio vya mwaka huu ni Shilingi elfu 2500 kwa watu mzima na shillingi 500 kwa watoto kila siku isipokuwa siku maalum ya tarehe 7 ambapo viingiio vitakuwa shilingi 3000 kwa watu wazima na watoto shilingi 1000.” Alisema Bulondo.

“Kwa watakao hudhuria maonyesho hayo na magari madogo watatakiwa kununua tiketi kwa shilingi 4000, kama ambavyo mchanganuo wa malipo unavyobainisha malipo ya huduma nyingine zikiwemo za kupaki magari kama malori na magari makubwa pamoja na huduma nyingine.”

Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo aliongeza kuwa, katika maonesho ya Mwaka huu, Usalama umeimarishwa kwa kiasi kikubwa na kutakuwa na Ulinzi wa Uhakika pamoja na Camera maalum zitakazo wekwa katika mageti na sehemu mbalimbali kuzunguka maeneo yote ya maonesho.

Kwa Upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, amesema kwa mwaka wa pili sasa wameendelea kuwawezesha watu, kufanya malipo ya tiketi kwa njia ya M pesa.

“M pesa inaendelea kurahisisha maisha ya Watanzania na mwaka huu, watu wote watakao kuja katika maonesho haya tumewawezesha kulipa viingilio kupitia M pesa na pia kufanya manunuzi na kulipa kwa M pesa katika banda letu la Vodacom.” Alisema Twissa.

Malipo ya ada binafsi.

1. Kwa siku – watu wazima (siku za kawaida) – 2,500/-

2. Kwa siku- watoto (siku za kawaida) – 500/-

3. Kwa siku – watu wazima (siku ya SabaSaba) – 3,000/-

4. kwa siku – Watoto (siku ya SabaSaba) – 1,000/-

5. malipo kwa kipindi chote cha maonyesho – Beji kwa wahusika wa maonyesho   – 20,000/-

6. Beji kwa wahusika wa maonyesho (maeneo) – 3,000/- 

Tiketi za uegeshaji magari.

1. Kwa siku (magari madogo)  – 4,000/-

2. kwa kipindi chote cha maonyesho – 30,000/-

3. Malipo kwa pamoja – 200,000/-

4. Tiketi za maegesho maalum – 400,000/-

5. Maroli na magari makubwa – 500,000/-

6. Malipo ya kuegesha magari nje ya viwanja vya saba saba – 1,500/-

Maonesho ya kimataifa ya Dar es salaam ni maonesho pekee yanayoongoza katika huduma za masoko Tanzania, maonesho hayo yanayodumu kwa siku kumi, huvutia watazamaji zaidi ya laki tatu na nusu na kutoa fursa kwa makampuni kuonyesha bidhaa zao na wanaohudhuria kununua vitu mbalimbali kwa gharama nafuu na kupata fursa ya kuuliza maswali na kulinganisha ubora wa bidhaaa kadha wa kadha.

MTEMVU AWADHIAKI WAPINZANI…..

Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akifungua Kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi ya CCM, wilaya ya Temeke, leo katika ukumbi wa Manispaa ya wilaya hiyo jijini Dar es Salaam.

Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, akimkabidhi hati ya pongezi , Zaitun Lukinga, ya kuwa kiongozi wa Jumuia ya Wazazi awamu zaidi ya moja katika nafasi ya Katibu wa Jumuia ya wazazi Kata ya Kurasini, wakati wa mkutano huo

 Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.

“NITAMSHUGHULIKIA KAFULILA”, WEREMA

Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu (kushoto) akijaribu kuwasuluhisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kulia) na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila katika Viwanja vya Bunge Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu (kushoto) akijaribu kuwasuluhisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kulia) na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila katika Viwanja vya Bunge Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

Dodoma. Mvutano kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila umechukua sura mpya baada ya mwanasheria huyo kugoma kupatanishwa huku akitishia ‘kumshughulikia’ mbunge huyo.

Ugomvi baina yao uliendelea jana asubuhi nje ya Ukumbi wa Bunge muda mfupi baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuahirisha kikao cha Bunge hadi leo.

Licha ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kumwita Jaji Werema na Kafulila akiwataka kupeana mikono kama ishara ya kuzika tofauti zao, Jaji Werema alikataa na nusura amvamie mbunge huyo.

Juzi asubuhi baada ya Zungu kuahirisha kikao cha Bunge, muda mfupi baada ya Jaji Werema na Kafulila kurushiana maneno bungeni, mwanasheria huyo alitaka kumtia adabu Kafulila kwa kumwita mwizi.

Kafulila alimwita Jaji Werema mwizi akijibu mapigo baada ya awali kuitwa tumbili na mwanasheria huyo.

Ilivyokuwa jana

Wakati akizungumza na gazeti hili mara baada ya Bunge kuahirishwa jana, Jaji Werema alikutana uso kwa uso na Kafulila katika Viwanja vya Bunge na kuanza kumlalamikia mbunge huyo kwa kitendo chake cha kumwita mwizi.

“Unamuona huyo jana (juzi), aliniita mimi mwizi. Yaani mtu mzima kama mimi naitwa mwizi, kwa kweli sikupendezwa kabisa na kauli yake,” alisema Jaji Werema huku akimfuata Kafulila ambaye alitembea harakaharaka kumkwepa mwanasheria huyo.

Jaji Werema alisema juzi alishikwa na jazba baada ya kuitwa mwizi lakini akasema hakuwa na nia ya kumpiga ndani ya Ukumbi wa Bunge.

Wakati Jaji Werema akiendelea kumlalamikia Kafulila, alitokea Zungu na kumtaka mwanasheria huyo kumsamehe mbunge huyo… “Mheshimiwa naomba mpeane tu mikono kama ishara ya kusameheana, yale mambo ya jana (juzi) yamekwisha.”

Lakini badala ya kukubaliana na ombi la Zungu, Jaji Werema alihamaki huku akitaka tena kumvamia Kafulila… “Mimi nakwambia Kafulila nitakukata kichwa, we subiri tu labda ukiniomba msamaha.”

Kafulila naye alijibu mapigo… “Huwezi kunikata kichwa Werema, huwezi, yaani uniue, hapana huwezi tena nakwambia huwezi.”

Wakati wakiendelea kurushiana maneno, Zungu alikuwa katikati yao, huku akiwasihi wapeane mkono na kusameheana bila mafanikio… “Haya mambo yamekwisha jamani, malizeni tofauti hizi.”

Kama vile alijua kuwa kauli ya kuua ilimchanganya Kafulila, Jaji Werema huku akitembea kuelekea katika Jengo la Utawala la Bunge alisema: “Siwezi kukuua kwa maana hiyo unayodhani, maana kufa utakufa kwa mapenzi ya Mungu, ila tutapambana tu, nitakuonyesha.”

 Kauli ya Kafulila

Akizungumza baadaye, Kafulila alisema: “Kutokana na hali ilivyo sasa, nimeandika barua Ofisi ya Spika juu ya vitisho nilivyopewa na Jaji Werema, kwanza jana (juzi) alitaka kunivamia pale bungeni na kunipiga, leo (jana) asubuhi amenitishia kuwa atanikata kichwa.”

Kafulila alisema barua hiyo pia ataipeleka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa maelezo kuwa siku za hivi karibuni yamekuwa yakitokea matukio ya watu kutekwa, kuteswa na kutupwa porini… “Kwa nafasi yake, Werema anaweza kufanya lolote, hivyo barua hizo zinalenga kueleza alichokusudia kunifanyia.”

Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alipoulizwa kuhusu mvutano uliotokea juzi bungeni na barua za Kafulila alisema Ofisi ya Bunge haijapata malalamiko yoyote.

“Jana sikuwapo bungeni lakini mpaka sasa hakuna malalamiko yoyote yaliyoletwa katika Ofisi ya Bunge. Kama wangeshikana mashati ndani ya Bunge  hilo lingekuwa kosa la kufanya fujo bungeni na adhabu zake zipo wazi,” alisema Joel.

Juzi, baada ya kurushiana maneno, Jaji Werema alinyanyuka alipokuwa amekaa na kuanza kumfuata Kafulila kabla ya kuzuiwa na kundi la mawaziri.

Mbali na kumzuia, mawaziri hao walimsindikiza hadi nje ya Ukumbi wa Bunge ambako alipanda gari lake na kuondoka.

BALOZI OMBENI SEFUE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WAKURUGENZI WA RASILIMALI WATU SERIKALINI

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni mgeni rasmi akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu serikalini katika ukumbi wa St. Gasper mjini Dodoma.

 Kaimu Mkuu Mkoa wa Dodoma Bi Fatma Salum Ally (katikati) akiwakaribisha wageni waalikwa wa mkutanomkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mkoani Dodoma, kabla ya mgeni rasmKatibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kulia) kufungumkutano huo katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu .

Katibu Mkuu Ofisi Rais, Utumishi wa Umma Bw.George D. Yambesi (katikati) akimkaribisha mgeni rasmi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.Kulia ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi.Claudia Mpangala.

 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wizarani, Idara za serikali zinazojitegemea, taasisi za umma na zinazojitegemea.

TAZAMA KICHUPA KIMPYA CHA 2FACE IDIBIA; “LET SOMEBODY LOVE YOU”

2Face Idibia ameachia kichupa kipya {Official Video} ya wimbo wake “Let Somebody Love You” ambae amemshirikisha msanii maarufu Bridget Kelly. Nyimbo hii ni moja ya vibao vyake sita ambavyo vinapatikana kwenye santuri (Album) yake inayo julikana kama Ascension. Kichupa hiki kimeongozwa na Luke Biggins na kimeshutiwa kwenye sehemu mbalimbali ya jiji la Lagos.

Source:- MTV Base.

RISASI TATU ZA MAJAMBAZI ZASABABISHA MAUTI KWA SISTA PRISENCIA KAPULI

Mwili wa Sista baada ya kupigwa risasi.

Majambazi watatu  wamemuua kwa kumpiga risasi kichwani  Mhasibu wa Kanisa Katoliki, Usharika wa Makoka,  jijini Dar es Salaam, Sista Prisencia Kapuli na kisha kumpora fedha zinazokadiriwa kuwa zaidi ya Sh milioni 10 alizokuwa nazo.  

Tukio hilo ni la jana saa 9 alasiri katika eneo la Ubungo Riverside wakati Prisencia, mtawa mwenzake pamoja na dereva wao, Mark Mwarabu, walipokwenda katika eneo  hilo  kununua mahitaji.

Sista  Kapuli ameuwawa kwa kupigwa risasi kichwani na majambazi  hayo  baada  ya  kufuatiliwa nyendo zao wakitokea katika benki ya CRDB ambayo tawi lake halikufahamika mara moja wakati akimsubiri Sista Mwenzie aliyeshuka katika gari walilokuwa wamepanda lenye namba za usajili  T 213 CJZ  Toyota VX kwa ajili ya kwenda kuulizia bidhaa fulani dukani katika eneo hilo la Riverside Ubungo jijini Dar es Salaam.

Gari lenye namba za usajili T 213 CJZ alilokuja nalo marehemu.

Akisimulia tukio hilo dereva wa gari la masister hao Bw Marck Patrick Mwarabu amesema  kuwa majambazi hayo yalikuwa matatu na alipojaribu kuyadhibiti kwa kufunga mlango wa gari walimjeruhi vibaya kwa risasi katika dole gumba lake na kisha kutoweka na pochi ya marehemu Kapuli kwa kutumia usafiri wa pikipiki.

Mmoja wa waendesha Bajaji Bw Godfrey Severine ambaye amenusurika katika tukio hilo bada ya Bajaji yake kupigwa risasi kadhaa amesema  kuwa watu hao walifyatua risasi kadhaa zilizosababisha taharuki kwa wananchi ambao walikuwa wakikimbia hovyo na hivyo kupata upenyo wa kutoweka katika eneo hilo.

Dereva akisimulia tukio zima la yeye  kupigwa risasi na sista aliyekuwa naye kuuawa.

Diwani wa kata ya Makuburi Bw William Mfungo aliyeshuhudia pia tukio hilo amesema wakati umefika sasa kwa jeshi la polisi kujizatiti kudhibiti matukio hayo kutokana na majambazi kutumia silaha nzito ambazo wananchi hawawezi kupambana nao na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pale wanapobaini njama kabla ya tukio kutokea.

 Mwili  wa  Sista  Kapuli  ukipakizwa  ndani  ya  gari la  Polisi

 Diwani wa kata ya Makuburi Bw William Mfungo  akizungumzia  tukio hilo.

SERENGETI BREWERIES LIMITED (SBL) YAPATA MWENYEKITI MPYA WA BODI YA WAKURUGENZI

Kampuni ya Serengeti Breweries Limited ( SBL ) inatangaza utuezi wa Ndg. Nehemia Mchechu kama Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya SBL. Uteuzi wa Ndg. Mchechu unafuata ukamilisho wa umiliki wa Mhe. Jaji (mstaafu) Mark Bomani . Katika nafasi yake mpya , Bw Mchechu pia atakukwa memba ya bodi ya kampuni ya bia ya East Africa.

Ndugu Nehemia Mchechu kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba la Taifa( NHC) . Bw. Mchechu anauzoefu mkubwa katika masuala ya fedha na usimamizi. Hapo awali alishika nafasi muhimu katika sekta ya benki , hasa kama Mkuu wa Masoko Kimataifa na mkurugenzi msaidizi benki ya Standard Chartered, na kuwa Mkurugenzi Mtendaji benki ya Commercial Bank of Africa Tanzania (CBA) .

Ndugu Mchechu ana Shahada ya Biashara (Fedha) na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Yeye pia ni Rais wa Umoja wa wanfunzi waliomaliza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Biashara na mwanachama wa ACI – Financial Market Association Tanzania.

Miongoni mwa nafasi nyingine muhimu, Ndugu Mchechu pia ni Mkurugenzi na mwanachama wa CEORT na pia ni Mkurugenzii wa TIC.

SBL inachukua fursa hii kumkaribisha na kumpongeza Mwenyekiti wake mpya wa bodi na kuwashukuru mwenyekiti wa bodi Mheshimiwa Bomani kwa mchango wake bora na wa kipekee wakati wa uongozi wake.

Mwenyekiti wa Bodi ya SBL aliemaliza muda wake,Mh. Mark Bomani akimpongeza mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo,Ndg. Nehemia Mchechu mara baada ya hafla ya kumpongeza.

Picha ya pamoja na Sehemu ya Wakurugeni wa SBL.

Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya SBL,Ndg. Nehemia Mchechu akizungumza machache kwenye hafla hiyo.