Muigizaji mkongwe nchini, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small amefariki dunia usiku huu akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar. Mzee Small amefariki kwa ugonjwa wa presha baada ya kuugua kwa muda mrefu kabla ya kuzidiwa jana na kupelekwa Muhimbili. Mtoto wa marehemu aitwaye, Muhidin amethibitisha kifo cha Mzee Small. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

Waombolezaji wakiwa na simanzi nyumbani kwa marehemu Said Ngamba ‘Mzee Small’ aliyefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Dada ya marehemu Mzee Small, Sauda Ngamba akiwa na majonzi baada ya kuondokewa na kaka yake.

Sauda akilia kwa uchungu.

PICHA NA SHANI RAMADHAN, GLADNESS MALLYA NA GABRIEL NG’OSHA

Advertisements