UCHAGUZI MKUU CHADEMA SASA NI SEPTEMBER 2014

KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa

KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga kufanya uchaguzi mkuu ngazi ya taifa Septemba, mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema uchaguzi huo utafanyika baada ya kuijenga CHADEMA kuanzia ngazi ya msingi nchi nzima.

Dk. Slaa alisema ili kuhakikisha wanapata misingi mingi, uchaguzi huo ulifanyika kwa zaidi ya mwaka na kuendelea hata sasa kufikisha asilimia 75 ya misingi nchi nzima.

Alisema katika uchaguzi huo wamefanikiwa kupata zaidi ya misingi laki 1.9 na kwamba itaongezeka idadi watapokamilisha zoezi hilo Juni 30.

Sambamba na uchugazi wa misingi, Dk. Slaa alisema uchaguzi wa matawi nao unaendelea na kwamba kati ya matawi 18,000 waliyokuwa nayo nchi nzima, uchaguzi umeshafanyika katika matawi 16,000.

Alisema kuanzia Julai, uchaguzi kwa ngazi ya jimbo, wilaya na mkoa utaendelea hadi Agosti, ili kupisha uchaguzi wa ngazi ya kitaifa.

Dk. Slaa alisema kwa sasa timu ya viongozi kutoka makao makuu ya chama hicho, wanazunguka katika mikoa yote nchini kuhakiki chaguzi ambazo zimekwishafanyika kama zimefuata katiba ya chama hicho na hakuna malalamiko.

Advertisements