KAMISHNA WA MAGEREZA NAMIBIA ATEMBELEA GEREZA LA KARANGA MOSHI

imageKamishna wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Tuhaferi(suti nyeusi) akisalimiana na Maafisa Waandamizi wa Magereza Mkoani Kilimanjaro alipotembelea Kiwanda cha Viatu, Gereza Kuu Karanga Moshi, Juni 21, 2014 Mkoani Kilimanjaro. image_1Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Rafael Tuhaferi(wa pili kushoto) akiangalia viatu vya ngozi vinavyotengenezwa na Kiwanda cha viatu, Gereza Karanga Moshi(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa. image_2Wafungwa wa Gereza Kuu Karanga Moshi wakishona viatu vya ngozi katika Kiwanda cha Viatu, Gereza Kuu Karanga Moshi. Wafungwa hao wamepewa Mafunzo ya Ufundi wa kutengeneza viatu vya aina mbalimbali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu mbalimbali za Urekebishaji wa Wafungwa ambapo kutokana na ujuzi huo pindi wamalizapo vifungo vyao watakuwa wamepata ujuzi ambao utawasaidia huko katika jamii zao. image_3Viatu aina ya Buti ambavyo hutumiwa na Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa Nchini vinavyotengenezwa na Kiwanda cha Viatu, Gereza Kuu Karanga Moshi. Kiwanda hicho pia hutengeneza viatu vya ngozi vya aina mbalimbali ambavyo hutumiwa pia hata na raia. photoKamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Tuhaferi(suti nyeusi) akiteta jambo na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(vazi la drafti) alipotembelea Kiwanda cha Viatu, Gereza Kuu Karanga Moshi, Juni 21, 2014. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoani Kilimanjaro.

Advertisements