FILAMU YA I LOVE MWANZA YAZINDULIWA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akisadiwa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba, kukata utepe kuzindua filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’ iliyoandaliwa na Lake Zone YouthEmpowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wa watatu kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonyesho na Waigizaji Tanzania (TDFAA), Mkoani Mwanza, Anitha Kagemulo. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akionyesha CD ya  filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’, iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, baada ya kuizindua katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wa watatu kushoto), Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba (kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonyesho na Waigizaji Tanzania (TDFAA), Mkoani Mwanza, Anitha Kagemulo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto), akinunua CD ya filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’, iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, baada ya kuizindua katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Waziri Membe aliwezesha filamu hiyo kununuliwa na wadau kwa zaidi ya Milioni 50/- katika hafla hiyo. Kulia ni Msanii wa Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’.
Advertisements