RISASI TATU ZA MAJAMBAZI ZASABABISHA MAUTI KWA SISTA PRISENCIA KAPULI

Mwili wa Sista baada ya kupigwa risasi.

Majambazi watatu  wamemuua kwa kumpiga risasi kichwani  Mhasibu wa Kanisa Katoliki, Usharika wa Makoka,  jijini Dar es Salaam, Sista Prisencia Kapuli na kisha kumpora fedha zinazokadiriwa kuwa zaidi ya Sh milioni 10 alizokuwa nazo.  

Tukio hilo ni la jana saa 9 alasiri katika eneo la Ubungo Riverside wakati Prisencia, mtawa mwenzake pamoja na dereva wao, Mark Mwarabu, walipokwenda katika eneo  hilo  kununua mahitaji.

Sista  Kapuli ameuwawa kwa kupigwa risasi kichwani na majambazi  hayo  baada  ya  kufuatiliwa nyendo zao wakitokea katika benki ya CRDB ambayo tawi lake halikufahamika mara moja wakati akimsubiri Sista Mwenzie aliyeshuka katika gari walilokuwa wamepanda lenye namba za usajili  T 213 CJZ  Toyota VX kwa ajili ya kwenda kuulizia bidhaa fulani dukani katika eneo hilo la Riverside Ubungo jijini Dar es Salaam.

Gari lenye namba za usajili T 213 CJZ alilokuja nalo marehemu.

Akisimulia tukio hilo dereva wa gari la masister hao Bw Marck Patrick Mwarabu amesema  kuwa majambazi hayo yalikuwa matatu na alipojaribu kuyadhibiti kwa kufunga mlango wa gari walimjeruhi vibaya kwa risasi katika dole gumba lake na kisha kutoweka na pochi ya marehemu Kapuli kwa kutumia usafiri wa pikipiki.

Mmoja wa waendesha Bajaji Bw Godfrey Severine ambaye amenusurika katika tukio hilo bada ya Bajaji yake kupigwa risasi kadhaa amesema  kuwa watu hao walifyatua risasi kadhaa zilizosababisha taharuki kwa wananchi ambao walikuwa wakikimbia hovyo na hivyo kupata upenyo wa kutoweka katika eneo hilo.

Dereva akisimulia tukio zima la yeye  kupigwa risasi na sista aliyekuwa naye kuuawa.

Diwani wa kata ya Makuburi Bw William Mfungo aliyeshuhudia pia tukio hilo amesema wakati umefika sasa kwa jeshi la polisi kujizatiti kudhibiti matukio hayo kutokana na majambazi kutumia silaha nzito ambazo wananchi hawawezi kupambana nao na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pale wanapobaini njama kabla ya tukio kutokea.

 Mwili  wa  Sista  Kapuli  ukipakizwa  ndani  ya  gari la  Polisi

 Diwani wa kata ya Makuburi Bw William Mfungo  akizungumzia  tukio hilo.

Advertisements