“WAHENGA WALINENA UTAVUNA ULICHOPANDA, MAPENZI TELE KWA KILA MTU”, LADY JAYDEE

Lady Jaydee

Lady Jaydee  July 27 alitangazwa kuwa washindi katika tuzo za AFRIMMA 2014 nchini Marekani alipo shinda kipengele cha mwanamuziki bora wa kike Afrika mashariki. Tuzo hizo ziliwashindanisha wanamuziki mbalimbali wakubwa wa Afrika.

Lady Jaydee kupitia ukurasa wake wa Facebook aliwashukuru mashabiki wake, aliandika:

“Nashukuru wote mnaokubali kazi zangu, wote mnaosimama na kutetea JayDee bila kusita, nashukuru kwa Tuzo nyingine tena toka AFRIMMA . Wahenga walinena kuwa utavuna ulichopanda, mapenzi tele kwa kila mtu”

jide afrimma

Katika post nyingine Jide amepost picha ya tuzo yake na kuandika:

“Tuzo yangu ya 30. Asanteni kwa ushirikiano, nimeipokea na ninarudi nayo nyumbani. Shhhhhh! !!! Kimya Kimya”.

Advertisements

MOVIE REVEW;- KITU CHA COVERT AFFAIRS SEASONAL 1

Covert-Affairs-USA-Network-poster-season-1-2010

Kitu cha Covert Affairs mpaka sasa kinaendelea kuonyeshwa kwenye TV network za marekani ambapo imefikia Seasonal 5. Kwa maana hiyo unaweza kujipatia mpaka Seasonal 4.

Seasonal 1 ina jumla ya Episodes 11, Story hii inaanza pale mwanadada mwenye umri wa miaka 28 Annie Walker, anapoitwa ghafla kutoka mafunzoni ya upelelezi na shirika la kijasusi la CIA nchini Marekani ili kufanya kazi maalum. Ofisi ya CIA ilieleza kuwa walimchagua kutoka miongoni mwa wanafunzi wenzake kutokana na umakini katika mafunzo maalum, Sifa nyingine ya ziada ni uwezo wake wa kuzungumza kwa ufasaha lugha za Kirusi, kitaliano, Kihispania, Kijerumani, Kifaransa, Kiajemi, Kireno na lugha nyingine kadhaa.

Alipo wasili CIA alikabidhiwa kwa Jasusi Agosti Anderson, jina la utani “Auggie” ambaye amepoteza uwezo wake wa kuona alipokuwa kwenye operation nchini Iraq, Idara hiyo ikiongozwa na jasusi Joan Campbell, ambapo yeye alikuwa na wajibu wa kumpa msaada wa kiufundi.

Original Title: Covert Affairs
Country, Channel: USA, USA Network
Release Date: June 13, 2010
Genres: Action, Crime, Drama, Mystery, Thriller
Creators: Chris Ord, Matt Corman
Cast: Piper Perabo as Anne Catherine “Annie” Walker, Christopher Gorham as August “Auggie” Anderson, Kari Matchett as Joan Campbell, Anne Dudek as Danielle Brooks, Sendhil Ramamurthy as Jai Wilcox, Peter Gallagher as Arthur Campbell, Emmanuelle Vaugier as Liza Hearn, Gregory Itzin as Henry Wilcox, Eion Bailey as Ben Mercer, Noam Jenkins as Vincent Rossabi, Oded Fehr as Eyal Lavin

Runtime: 60 min
Language: English

Kama unaitaji movie hii au nyingine zozote wasiliana nasi kwa simu +255 732 981 189

MGOMBEA URAIS WA MSUMBIJI AKUTANA NA MAMA MARIA NYERERE KUOMBA BARAKA.

Mgombea huyo wa Urais Filipe Nyusi akimsalimia Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia alifika Uwanja wa Ndege pamoja na Kinana. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.

Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Filipe Nyusi akisalimiana na wana-CCM waliofika kumlaki Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Kulia ni Mwenyeji wake, Abdulrahman Kinana.

PRINCE AKISHINO NA MKEWE WAFURAHI WIKENDI YAO SERENGETI NA NGORONGORO

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (MP) inamkaribisha Prince Akishino na mke wake Princess Kito kutoka Japan kwenye kiwanja kidogo cha ndege cha Manyara tayari kwa ziara yao ya Ngorongoro Crater na Serengeti National Park mwishoni mwa wiki.

 

 

Princess Kito wa Japan akipokea shada la maua kutoka kwa Bi. Lilian Sukhe wa Bodi ya Utalii Tanzania wakati wa mapokezi yao kwenye uwanja mdogo wa ndege wa Manyara tayari kwa ziara yao ya Ngorongoro Crater na Serengeti National Park mwishoni mwa wiki.

 

 

Kikundi cha utamaduni cha kabila ya Wamasai wakimburudisha Prince Akishino na mke wake Princess Kito walipofika Loduare Gate, Ngorongorto Conservation Area.

 

 

Prince Akishino na mke wake Princess Kito waliamua kufanya matembezi ya miguu kwa muda mfupi ndani ya mbuga za Serengeti National Park.

 
Kaimu Mkuu wa Mkoa Mara Bi. Angelina Mabula akimkabidhi zawadi ya kinyago cha tembo Prince Akishino mara baada ya kumaliza dhihara yao Serengeti National Park.

WAKAZI MTO WA MBU NA WAFANYAKAZI WA HIFADHI YA ZIWA MANYARA WASHIRIKI KUTUNZA MAZINGIRA

DSC_0281

DSC_0285

DSC_0286

DSC_0290

DSC_0292

DSC_0296

DSC_0301
Baadhi ya wananchi wa kata ya mto wa mbu wakiwa na wafanyakazi wa hifadhi ya ziwa Manyara wakishiriki kufanya usafi wa mazingira kwenye mji wa Mto wa Mbu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku ya uhifadhi duniani

WAKAZI HAO WA KATA YA MTO WA MBU waliwapongeza wafanyakazi hao kwa kujitolea na kuacha shughuli zao kwenda kuhimiza usafi wa mazingira ya mji wao huku wakiwataka wenzao kujali usafi wa mazingira ilikuepuka magonjwa ya milipuko

Kwa upande wake kaimu mhifadhi wa hifadhi ya ziwa manyara Ibrahimu Yamola alisema kuwa wakazi hao ambao ni jirani na mbuga hiyo wnapaswa kuyajali mazingira wanamo ishi kwa kyaweka katika hali ya kuvutia kwani mji wao unapokea wageni mbalimbali kutoka mataifa mbalimbal;i wanaokuja kutembelea mbuga hizo

Aktanabaisha kuwa siku ya uhifadhi duniani inasherehekewa duniani kote na hapa nchini imekuwa ikisherehekewa kwa kufanya shughuli mbalimbali za ujirani mwema kama tulivyofanya leo kufanya usafi wa mazingira kuzunguka kata ya mto wa mbu.

SOURCE:- MAHMOUD AHMAD

VIDEO INTERVIEW: JIMMY KABWE AELEZA MATARAJIO YAKE KAMA MTANGAZAJI MPYA WA KIPINDI CHA THE BIG EASY CHA CHOICE FM

Mtangazaji mkongwe wa redio nchini na mmoja wa watangazaji wa kwanza kabisa wa Clouds FM, Jimmy Kabwe, amechukua nafasi ya Chris Lugoe aka ML Chris kwenye kipindi cha The Big Easy cha Choice FM ambapo atakuwa akishirikiana na Abby.

“Kwakweli Choice FM is my choice,” Kabwe ameiambia Bongo5 kwenye mahojiano maalum. “Muda ulipofika wa mimi kurudi kwenye media napoangalia sasa radio stations ambazo zipo ni ipi inayoweza kunicompliment zaidi na Choice ilikuwa number one kwasababu Choice ni bilingual, mimi ni mtangazaji ambaye napenda kuwa free with languages na napenda niwe huru kutumia lugha zote mbili,” ameongeza.

Jimmy amesema kipindi cha Big Easy sio kigeni kwake kwakuwa hata wakati ML Chris anakianzisha kuna masuala alikuwa akimuomba ushauri kwakuwa ni marafiki wazuri.

“Nina excitement mara mbili, kipindi chenyewe nakipenda sana, nilikuwa msikilizaji mkubwa, nilikuwa mchangiaji mkubwa na sio kipindi ambacho utaenda kukichezea tu, nipo committed, dedicated to make sure kinaenda another level,” amesema Kabwe.

Kabwe ataanza kusikika kwenye kipindi hicho kuanzia Jumatatu ijayo.

MILIPUKO (UGAIDI) UNATUPITISHA ARUSHA KATIKA KIPINDI KIGUMU SANA; LEMA

Sheikh alijeruhiwa miguu yake yote na mapajani huku Kifea akipata majeraha makubwa miguuni na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote

Sheikh alijeruhiwa miguu yake yote na mapajani huku Kifea akipata majeraha makubwa miguuni na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote

  • “Arusha tunapita katika kipindi kigumu sana. Kwanza tulishuhudia mlipuko wa bomu kanisani, ikafuatiwa na lile la mkutano wa hadhara wa Chadema, kabla ya mwingine kulipuka kwenye baa na sasa nyumbani kwa Sheikh,” Lema.

Arusha. Sheikh wa Msikiti wa Qiblatan,Sood Ally Sood (37) uliopo Kilombero jijini hapa amejeruhiwa kwa bomu la kurushwa kwa mkono alipokuwa akila daku nyumbani usiku wa kuamkia jana.

Pamoja na Sheikh Sood, mtu mwingine aliyekuwa nyumbani kwake,aliyetajwa kwa jina la Muhaji Kifea (38) mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam pia amejeruhiwa katika tukio hilo na wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa matibabu.

Sheikh alijeruhiwa miguu yake yote na mapajani huku Kifea akipata majeraha makubwa miguuni na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote.

Akizungumza hospitalini hapo, Sheikh, Sood alisema tukio hilo lilitokea nyumbani kwake eneo la Majengo ya chini, usiku wa kuamkia jana saa 5:00 wakati yeye pamoja na mgeni wake walikuwa wakila chakula sebuleni.

“Nikiwa sijui hili wala lile nilishtushwa na mlipuko ulioambatana na vyuma mbalimbali vilivyokuwa vikiruka hewani ambapo bomu hilo linaelezwa kuwa ni guruneti lililorushwa kupitia dirishani baada ya watu wasiofahamika kufanikiwa kuvunja kioo cha dirisha la chumba tulichokuwamo,” alisema Sheikh Sood.

Alidai anawajua waliotekeleza shambulio hilo kwa sababu amekuwa akipokea vitisho kutoka kwa watu anaowafahamu na tayari alikuwa ametoa taarifa kwa vyombo vya dola.

Alisema kuwa siku tatu kabla ya tukio hilo alikoswakoswa kupigwa risasi na watu wasiofahamika wakati akitoka msikitini na akatoa taarifa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Arusha kuhusu tukio hilo. Sood anasema kuna baadhi ya vijana anawatuhumu juu ya matukio hayo.

Sheikh huyo ambaye ni Kiongozi wa dhehebu la Answar sun Kanda ya Kaskazini amekuwa akitofautiana na waumini wenzake kutokana na msimamo wake wa kutokukubaliana na baadhi ya waumini wenye msimamo mkali wa msikiti huo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alikemea matukio ya mabomu yanayolitikisa Jiji la Arusha katika siku za karibuni na kuviagiza vyombo dola kufanya uchunguzi wa kina kubaini wahusika wote ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha tukio hili limetekelezwa na watu walio karibu na Sheikh. Polisi wanaendelea na uchunguzi kwa sababu baadhi ya watu wanaotajwa kuhusika kwenye tukio hili pia ni miongoni mwa watuhumiwa kwenye matukio mengine ya milipuko ya bomu Arusha,” alisema Mulongo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatusi Sabasi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa majeruhi wanaendelea vyema huku polisi wakiendelea na uchunguzi wa kina kuwabaini wahusika.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alielezea kusikitishwa na matukio ya milipuko ya mabomu Arusha na kuliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina kuwakamata wahusika bila kujali vyeo, nyadhifa, dini, itikadi wala rangi zao.

“Arusha tunapita katika kipindi kigumu sana. Kwanza tulishuhudia mlipuko wa bomu kanisani, ikafuatiwa na lile la mkutano wa hadhara wa Chadema, kabla ya mwingine kulipuka kwenye baa na sasa nyumbani kwa Sheikh,” alisema Lema.

SOURCE: MWANANCHI

LOWASSA, SITTA NA WASSIRA HAWANA SIFA ZA KUWANIA URAIS; WARIOBA

“Na mimi nashangaa kwa nini, kwa kweli nashangaa kabisa kutajwatajwa huku, wazee kama mimi na Salim (Dk Salim Ahmed Salim). Nini kimetokea katika nchi hii hata sisi tufikiriwe?” Jaji Joseph Warioba

“Na mimi nashangaa kwa nini, kwa kweli nashangaa kabisa kutajwatajwa huku, wazee kama mimi na Salim (Dk Salim Ahmed Salim). Nini kimetokea katika nchi hii hata sisi tufikiriwe?” Jaji Joseph Warioba

  • Asema anatakiwa awe kijana mwenye maadili, mwajibikaji

  • Asema hatagombea urais, aachwe alee wajukuu

Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba ametoa dira ya urais katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kutaja sifa za rais anayefaa kuiongoza Tanzania.

Warioba alisema kwamba taifa la Tanzania linastahili kuongozwa na vijana wenye nguvu ya mwili na akili. “Mimi nafikiri tuangalie kati ya vijana tulionao, nani anatufaa kuiongoza nchi, tusirudi kuangalia wazee,” alisema Jaji Warioba.

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari hizi katika mahojiano maalumu yaliyofanyika wiki hii ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Uchaguzi huo mkuu ambao ni wa tano wa vyama vingi nchini, unatarajiwa kulipatia taifa rais mpya, baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake wa utawala wa awamu ya nne.

“Uongozi mzuri unatengenezwa na haiba, wajihi, dhamira, uwezo, maadili, uhodari, hekima na maarifa. Sifa hizi hazipatikani kutokana na uzoefu wa miaka mingi kwenye siasa hata baadhi ya vijana wanazo,” alisema Makamba.

Alitolea mifano mingi duniani ambapo vijana ambao hawakuwa na uzoefu kabisa katika nafasi za siasa wameshinda na kubadilisha nchi kama Tony Blair wakati anakuwa Waziri Mkuu wa Uingereza aliongoza nchi hiyo kubwa wakati alikuwa hajawahi kuwa hata Naibu Waziri.

“Barack Obama (Rais wa Marekani) alikuwa Seneta miaka mitatu tu, Julius Nyerere alikuwa Mwalimu akaingia siasa akaja kupewa uongozi wa nchi akiwa na miaka 39 tu.”

Katika maelezo yake Jaji Warioba alisema kwamba tangu uhuru, walioshika madaraka ya kuliongoza taifa walikuwa ni vijana.

Wazee kugombea urais

Akijibu swali kama atakuwa tayari wananchi wakimtaka kuwania urais baada ya kazi kubwa ya kukamilisha Rasimu ya Katiba nchini, Jaji Warioba alisema:

“Hili nilikwishalijibu, tusahau mawazo kwamba sisi (wazee) tutarudi madarakani. Nadhani mara ya mwisho tulipozungumza niliwaambia inafika wakati kiongozi unang’atuka. Unawaachia vijana ambao wana nguvu ya kimwili na akili ndiyo watumikie taifa hili, waongoze nchi.

“Na mimi nashangaa kwa nini, kwa kweli nashangaa kabisa kutajwatajwa huku, wazee kama mimi na Salim (Dk Salim Ahmed Salim). Nini kimetokea katika nchi hii hata sisi tufikiriwe?” alihoji Jaji Warioba.

Alisema kuwa tangu uhuru hadi sasa Tanzania imetayarisha vijana wengi wanaofaa kuliongoza taifa na kuongeza:

“Hatuna ombwe la uongozi, tunao vijana wengi sana, tena kwa bahati nzuri nchi kwa kiwango kikubwa ilikuwa ikiongozwa na vijana.”

Huku akitaja mifano ya viongozi hao vijana walioongoza taifa, Warioba ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema:

Makundi ya urais

Warioba pia aliulizwa iwapo makundi yanayotajwa kusaka urais katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015 kuwa huenda yanahusika na kusuasua kwa Mchakato wa Katiba Mpya.

Alisema kwamba, yeye na wenzake waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba walikutana jijini Dar es Salaam kwa siku tatu na kutafakari mchakato huo unavyokwenda ukihusisha maeneo na makundi mbalimbali.

“Tulikwenda kutafakari, hatutaki kwenda kwenye matukio, wala kuzungumzia makundi, nasema wote wakae pamoja waone masilahi ya taifa, kwa sababu wasipokaa pamoja kuna hatari ya mchakato huu wa Katiba Mpya kukwama. Na kukwama siyo kwa masilahi ya taifa,”alisema.

Ikiwa Rasimu ya Katiba Mpya itapitishwa na mapendekezo yake ya kuwapo kwa mfumo wa serikali tatu, kutalazimika kuwapo kwa Rais wa Tanganyika, Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo nguvu na mfumo wa kisiasa kubadilika.

SOURCE: MWANANCHI

VIDEO: MR BLUE AKIWA NA VIJANA WA B.O.B MICHARAZO WAMEACHIA KICHUPA KIPYA KIITWACHO “SHUT UP” (KIMYA).

Vijana wa B.O.B Micharazo, wakiongozwa na front runners, Mr Blue na Nyandu Tozi, wameachia video ya ngoma yao mpya iitwayo ‘Shut Up’ (Kimya).

Kwenye ngoma hiyo iliyotayarishwa na Marco Chali, rappers hao wanafanya mtindo wa kubeto na hivyo kupeleka onyo kali kuwanyamazisha wapinzani wao. Katika verse ya Mr Blue ambaye amesima vizuri amefungua ngoma hiyo kwa panch “Helo Dar es Salaam mbona kimya jiji zima mbona limezizima/Hakuna cha Sharobaro wala ming’aro ya kuazima/ Mmebakiza uharo kumbe washenzi mlipima/Wabaya wetu mbona kimya, vipi wazima au nanyinyi mlipima,” anarap Kabayser.

Wengine waliochana kwenye ngoma hiyo ni Blood Gaza, Bobby MC, Cotton, Uswege na Beka Title aliyesimama kwenye chorus.

BARUA YA MUME WA FLORA MBASHA KWA MCHUNGAJI GWAJIMA

MUME WA FLORA MBASHA

Hii barua ya Mume wa Mwimbaji wa Nyimbo za injili nchini – Flora Mbasha kwenda kwa mchungaji maarufu nchini, Mchungaji Gwajima inakuhusu….

“Mchungaji …yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri’ wa ghafla wa mkewangu Mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mkewangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwakoMchungaji, naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!!

Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mkewangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!

Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha??

Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna nini hapo??

Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa!

Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia hoteli ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya forest hill!!

Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es salaam!!

Lakini uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mkewangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu arudi hotelini kingsway!!

Kwaa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!! Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!!

Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako… na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!! Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda Yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!

Mkewangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!! Lakini nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mkewangu Fedha Au huyo mchungaji mwanamazingaombwe Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize nionekane sifai katika jamii Ni nini kilichokuoata mkewangu??

Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana! Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!!

Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!! Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!!

Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!!

Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!!

Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!!
Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!

Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti!

Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!!
Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda..”

Kwako – Mchungaji Gwajima

SOURCE:- mwanahalisiforum.com

NINA WASIWASI KAMA MWAFAKA AU MARIDHIANO YATAPATIKANA AGOSTI WAKATI BUNGE MAALUMU LITAKAPOKUTANA; BOMANI

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu, Jaji Mark Bomani akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Michael Matemanga

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu, Jaji Mark Bomani akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Michael Matemanga

Dar es Salaam. Jaji mstaafu Mark Bomani amelishauri Bunge Maalumu la Katiba kuweka kando suala la muundo wa serikali kwa kuwa ndiyo chanzo cha mgawanyiko mkubwa baina ya wajumbe.

Pia amewashauri wajumbe wa Bunge hilo wanaounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kurejea bungeni ili mchakato huo uweze kuendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Jaji Bomani alisema suala la muundo wa Serikali licha ya kusababisha mgawanyiko limesababisha hoja nyingine muhimu kusahaulika. 

“Kwa bahati mbaya sana kwa maoni yangu, mjadala wa mapendekezo hayo umezua malumbano na ubishi mkali, kiasi cha kufanya baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo kujitoa,” alisema Jaji Bomani. 

Alisema amewahi kutoa maoni kwamba suala lote la muungano na idadi ya Serikali linatakiwa lijadiliwe kwanza ama na Serikali mbili zilizopo, yaani Zanzibar na ya Muungano au Wazanzibari waulizwe iwapo wanautaka muungano. 

“Hata hivyo nina wasiwasi kama mwafaka au maridhiano yatapatikana mwezi Agosti Bunge Maalumu litakapokutana, kwa kuwa zimejitokeza tofauti kubwa za kimtazamo au kiitikadi bila kusahau masilahi binafsi,” alisema Jaji Bomani. 

Alisema kwa uzoefu wake katiba nzuri kwa nchi yoyote ni ile ambayo imepatikana kwa wananchi wengi kuikubali na siyo vinginevyo.

“Katiba nzuri ni ya maridhiano. Katiba nzuri haiwezi kupatikana kwa wingi wa kura au hoja ya nguvu tu bali inatakiwa iwe inakubalika na walio wengi (consensus),” alisema.

Aliyataja mambo mengine muhimu ambayo yanapaswa kujadiliwa na wajumbe kuafikiana ni pamoja na suala la uwakilishi sawa wa jinsia yaani asilimia 50 kwa 50, kwenye ubunge na halmashauri za wilaya.

“Suala la mawaziri kutokuwa wabunge nalo pia nafikiri linaweza kujadiliwa na mwafaka ukapatikana, muundo wa tume huru ya uchaguzi na suala la mgombea binafsi nalo naamini linajadilika wanaoliogopa hawana msingi wa kufanya hivyo,” alisisitiza Jaji Bomani.

SOURCE:- Mwananchi

PRINCE AKISHIO NA MKEWE WATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Mwana wa Mfalme wa Japan Prince Akishino na mkewe Princess Kiko leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuona jinsi inavyotoa huduma zake kwa Watanzania.

Akitoa salamu za pongezi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Agnes Mtawa amesema Hospitali imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la JICA katika maeneo mbalimbali ya huduma ikiwemo ujenzi wa maabara maalumu ya watoto, ujenzi wa Kituo cha Maelezo ya Afya Muhimbili pamoja na kuongeza uwezo wa Hospitali katika kuboresha huduma zake kupitia mpango wa uboreshaji huduma (quality improvement program).

Katika ziara yao, wametembelea Jengo la watoto kitengo cha watoto walioungua moto, wodi ambazo zimekidhi viwango vya ubora wa huduma, na jengo la wazazi ili kuona namna ambavyo akina mama wanapata huduma za afya ya mama na mtoto.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Agnes Mtawa akisalimiana na Prince Akishino wakati alipowasili Hospitalini hapo. Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Dkt. Mahadhi Juma Maalim.

Prince Akishino na Mkewe Princess Kiko wakifurahia jambo katika mojawapo ya wodi za watoto ambazo zimekidhi viwango vya program ya uboreshaji wa huduma.

Mkuu wa Idara ya Afya ya Akina Mama Dkt. Mathew Kallanga akitoa ufafanuzi kwa Prince Akishino kuhusu idara yake inavyowahudumia akina mama.

Princess Kiko akifurahia na akina mama baada ya kuona mtoto aliyekuja kliniki.

TACAIDS WAONGEA NA WANAHABARI KWENYE VIWANJA VYA SABASABA JIJINI DAR

Afisa Mawasiliano Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika banda la TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba jana Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela

Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika banda la TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba jana Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mawasiliano Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa

 

Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela akimuuliza swali Mwelimisha Rika kutoka PSI (Population Service International) Bi: Veronica Mbilinyi alipotembelea banda hilo katika Viwanja vya Sabasaba leo jijini Dar es Salaam.(Picha na: Genofeva Matemu)