Wakazi wa jiji la Mbeya wamejitokeza kwa wingi katika stendi kuu mpya iliopo eneo la nane nane RRM kwaajili ya kuomba maeneo ya kufanyia biashara zao katika eneo hilo.Wageni kutoka mikoani mnataarifiwa kua stendi kuu ya jiji la Mbeya kwa sasa ipo eneo la nanenane (karibu na Uyole) na si mjini soko matola tena kama iliyokuwa hapo awali,lakini si wa mikoani tu bali hata baadhi ya wilaya za jiji la Mbeya.Hivyo ukifik jijini Mbeya usishangae kuambia kuwa basi linaishia hapo eneo la Nane nane,kwani ndipo ilipo Stendi Kuu mpya kwa sasa na siku zote.

 

Muonekano wa eneo la Stendi kuu hiyo.
Abiria wakisubiria Usafiri kwenye stendi kuu hiyo.
Sehemu ya kuingilia Mabasi.
Mabasi madogo yanayofanya safari zake katika baadhi ya Wilaya za Jiji hilo la Mbeya.
Sehemu ya Wakazi wa Jiji la Mbeya waliojitokeza kwa ajili ya kuomba maeneo ya kufanyia biashara zao kwenye Stendi kuu Mpya ya jiji la Mbeya.Picha zote na Fadhil Atick
Advertisements