{TAZAMA MAGOLI KOMBE LA DUNIA 2014} UBELGIJI YAIZAMISHA MAREKANI MUDA WA ZIADA 2 – 1

Belgium-vs-United-States-World-Cup-2014-Round-Of-16-Soccer-Wallpaper-2048x1536

Timu ya taifa ya Ubelgiji ilifanikiwa kuzifumania nyavu mara mbili katika muda wa ziada na kusababisha hamaki kwa wapenzi wa timu ya taifa ya Marekani, ushindi huo wa 2-1 umeivusha Ubelgiji katika hatua ya 16 bora na kuingia robo fainali.

Ni vigumu kuelezea mchezo huu uliochezwa Jumanne Julai 14, 2014 nchini Brazil, labda neno sahihi zaidi kwa kuielezea timu ya Marekani ilikuwa ni “kutaabika”. Shujaa wa Marekani katika mchezo huu alikuwa ni kipa wao Tim Howard ingawa pamoja na ustadi wake alishindwa kuzuia mabao mawili ya Ubelgiji katika kipindi cha kwanza cha muda wa ziada.

Ubelgiji huenda wangeweza kushinda mapema kabla ya muda wa nyongeza lakini alikuwa ni Howard huyohuyo aliye zima ndoto zao, Kwa upande wa timu ya Marekani nao walipata nafasi kadha, almanusura wafunge katika dakika ya 90 na kwa mshangao wa wengi Chris Wondolowski akapaisha mpira akiwa yeye na nyavu.

Muda wa nyongeza tulishuhudia Ubelgiji wakitawala mpira kwa kiasi kikubwa, ilikuwa dakika ya 93 tu kupitia kwa mshambuliaji Kevin De Bruyne Ubelgiji wakajipatia bao la kwanza huku lile la ushindi likisubiri sekunde chache tu kabla ya kipindi cha kwanza cha muda wa nyongeza kwisha, hali ilio wadhoofisha wa Marekani.

Marekani ilizinduka kipindi cha pili cha muda wa nyongeza pale Michael Bradley alipofanikiwa kuupitisha mpira katikati ya msitu wa mabaki wa Ubelgiji ukamkuta chipukizi wa miaka 19 Julian Green ambaye bila makosa akaiandikia marekani bao. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa chipukizi huyo kuichezea timu yake ya taifa ya marekani katika kombe la Dunia nchini Brazil.

Hadi mwisho ubao wa matangazo zilisomeka 2 -1, hii ilikuwa safari ya mwisho ya timu ya taifa ya Marekani ambayo imeandika historia ya aina yake katika mashindano hayo. Juhudi, vipaji ambavyo vimeonyesha na timu hiyo ya Marekani tokea hawali walipofanikiwa kuvuka kundi lao la kifo zilimalizika baada ya dk. 120 dhidi ya moja kati ya timu bora kabisa duniani. Kwa hakika si dhani kama unaweza kuomba zaidi ya hapo.

text

ilikuwa dk. 114′ ambapo marekani karibia wapate goli la kuzawzisha kupiti mpira wa dhabu uliopigwa kivundi sana ….

text

hili ndiyo goli la kufutia machozi la timu ya Taifa ya Marekani lililofungwa katika dk. 107′ kupitia kwa chipukizi  Julian Green, ambaye ana mika 19.

text

Goli la ushindi la timu ya Ubelgiji lilifungwa Dk. ya  105′ Lukaku ambaye alipata pasi kutoka kwa De Bruyne.

text

Mshambuliaji wa Marekani Wondolowski alikosa goli la wazi katika dk. ya 90′

text

Kipa wa marekani alifanikiwa kuokoa mpira ambao ulionekana wazi kuwa ungeweza kuza goli katika dk. 76′ 

text

Dk. 69′ alikuwa mshambuliaji wa Ubelgiji aliye achia mkwaju mkali lakini ukatoka nchje ya lango la Marekani.

Advertisements