BARUA YA MUME WA FLORA MBASHA KWA MCHUNGAJI GWAJIMA

MUME WA FLORA MBASHA

Hii barua ya Mume wa Mwimbaji wa Nyimbo za injili nchini – Flora Mbasha kwenda kwa mchungaji maarufu nchini, Mchungaji Gwajima inakuhusu….

“Mchungaji …yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri’ wa ghafla wa mkewangu Mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mkewangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwakoMchungaji, naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!!

Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mkewangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!

Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha??

Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna nini hapo??

Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa!

Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia hoteli ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya forest hill!!

Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es salaam!!

Lakini uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mkewangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu arudi hotelini kingsway!!

Kwaa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!! Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!!

Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako… na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!! Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda Yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!

Mkewangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!! Lakini nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mkewangu Fedha Au huyo mchungaji mwanamazingaombwe Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize nionekane sifai katika jamii Ni nini kilichokuoata mkewangu??

Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana! Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!!

Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!! Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!!

Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!!

Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!!

Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!!
Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!

Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti!

Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!!
Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda..”

Kwako – Mchungaji Gwajima

SOURCE:- mwanahalisiforum.com

Advertisements

NINA WASIWASI KAMA MWAFAKA AU MARIDHIANO YATAPATIKANA AGOSTI WAKATI BUNGE MAALUMU LITAKAPOKUTANA; BOMANI

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu, Jaji Mark Bomani akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Michael Matemanga

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu, Jaji Mark Bomani akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Michael Matemanga

Dar es Salaam. Jaji mstaafu Mark Bomani amelishauri Bunge Maalumu la Katiba kuweka kando suala la muundo wa serikali kwa kuwa ndiyo chanzo cha mgawanyiko mkubwa baina ya wajumbe.

Pia amewashauri wajumbe wa Bunge hilo wanaounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kurejea bungeni ili mchakato huo uweze kuendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Jaji Bomani alisema suala la muundo wa Serikali licha ya kusababisha mgawanyiko limesababisha hoja nyingine muhimu kusahaulika. 

“Kwa bahati mbaya sana kwa maoni yangu, mjadala wa mapendekezo hayo umezua malumbano na ubishi mkali, kiasi cha kufanya baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo kujitoa,” alisema Jaji Bomani. 

Alisema amewahi kutoa maoni kwamba suala lote la muungano na idadi ya Serikali linatakiwa lijadiliwe kwanza ama na Serikali mbili zilizopo, yaani Zanzibar na ya Muungano au Wazanzibari waulizwe iwapo wanautaka muungano. 

“Hata hivyo nina wasiwasi kama mwafaka au maridhiano yatapatikana mwezi Agosti Bunge Maalumu litakapokutana, kwa kuwa zimejitokeza tofauti kubwa za kimtazamo au kiitikadi bila kusahau masilahi binafsi,” alisema Jaji Bomani. 

Alisema kwa uzoefu wake katiba nzuri kwa nchi yoyote ni ile ambayo imepatikana kwa wananchi wengi kuikubali na siyo vinginevyo.

“Katiba nzuri ni ya maridhiano. Katiba nzuri haiwezi kupatikana kwa wingi wa kura au hoja ya nguvu tu bali inatakiwa iwe inakubalika na walio wengi (consensus),” alisema.

Aliyataja mambo mengine muhimu ambayo yanapaswa kujadiliwa na wajumbe kuafikiana ni pamoja na suala la uwakilishi sawa wa jinsia yaani asilimia 50 kwa 50, kwenye ubunge na halmashauri za wilaya.

“Suala la mawaziri kutokuwa wabunge nalo pia nafikiri linaweza kujadiliwa na mwafaka ukapatikana, muundo wa tume huru ya uchaguzi na suala la mgombea binafsi nalo naamini linajadilika wanaoliogopa hawana msingi wa kufanya hivyo,” alisisitiza Jaji Bomani.

SOURCE:- Mwananchi

PRINCE AKISHIO NA MKEWE WATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Mwana wa Mfalme wa Japan Prince Akishino na mkewe Princess Kiko leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuona jinsi inavyotoa huduma zake kwa Watanzania.

Akitoa salamu za pongezi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Agnes Mtawa amesema Hospitali imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la JICA katika maeneo mbalimbali ya huduma ikiwemo ujenzi wa maabara maalumu ya watoto, ujenzi wa Kituo cha Maelezo ya Afya Muhimbili pamoja na kuongeza uwezo wa Hospitali katika kuboresha huduma zake kupitia mpango wa uboreshaji huduma (quality improvement program).

Katika ziara yao, wametembelea Jengo la watoto kitengo cha watoto walioungua moto, wodi ambazo zimekidhi viwango vya ubora wa huduma, na jengo la wazazi ili kuona namna ambavyo akina mama wanapata huduma za afya ya mama na mtoto.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Agnes Mtawa akisalimiana na Prince Akishino wakati alipowasili Hospitalini hapo. Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Dkt. Mahadhi Juma Maalim.

Prince Akishino na Mkewe Princess Kiko wakifurahia jambo katika mojawapo ya wodi za watoto ambazo zimekidhi viwango vya program ya uboreshaji wa huduma.

Mkuu wa Idara ya Afya ya Akina Mama Dkt. Mathew Kallanga akitoa ufafanuzi kwa Prince Akishino kuhusu idara yake inavyowahudumia akina mama.

Princess Kiko akifurahia na akina mama baada ya kuona mtoto aliyekuja kliniki.

TACAIDS WAONGEA NA WANAHABARI KWENYE VIWANJA VYA SABASABA JIJINI DAR

Afisa Mawasiliano Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika banda la TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba jana Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela

Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika banda la TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba jana Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mawasiliano Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa

 

Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela akimuuliza swali Mwelimisha Rika kutoka PSI (Population Service International) Bi: Veronica Mbilinyi alipotembelea banda hilo katika Viwanja vya Sabasaba leo jijini Dar es Salaam.(Picha na: Genofeva Matemu)

MWANA FA KUJA NA VIDEO YA MFALME WAKATI UJIO MPYA WA G-NAKO WASUBIRIWA…

MWANA FA ft.G NAKO - MFALME www.allstartz.blogspot.com

Msanii wa Hip Hop, Hamis Mwinjuma aka Mwana FA anatarajia kuachia video ya wimbo wake ‘Mfalme’ aliomshirikisha G-Nako baada ya kushoot video hiyo nchini Kenya.

G-Nako, alinukuliwa jana akisema kuwa Mwana FA alikuwa na idea ya video hali ambayo ilisaidia video hiyo kufanyika kwa muda mfupi. “Director ambaye tumefanya naye video ni yule ambaye alishoot video ya AY, Asante anaitwa Kevin Bosco. Director alikuwa na mawazo yake na Mwana FA alikuwa na mawazo yake, kilichofanyika kizuri ni yale mawazo yaliwekwa pamoja halafu yakauwishwa, kwahiyo nazani kila kitu kilienda sawa,” alisema G.

Wakati huo huo rapper huyo alizungumzia ujio wa single yake mpya baada Joh Makini na Nick Pili kuachia kazi zao.

“Kazi zangu zinakuja na unajua sisi namna tunafanya kazi huwa tunapeana muda kidogo ambao akitoa mtu upatikane muda wa watu wasikilize, kwasababu mara nyingi watu wanatuconfuse kutuweka kama kundi, lakini sisi ni kampuni na vilevile kila mtu anakuwa na project zake,” alisema. “Kwahiyo kazi zangu zinakuja na hapa katikati ulisikia kazi yangu na Godzilla inaitwa ‘Tumewaka ‘ nayo inafanya vizuri nafikiri naipa muda kidogo halafu nafikiri baada ya mwezi wa Ramadhani kwisha hapo mbele kidogo tu nitaachia ngoma. Mgoma zipo nyingi ila sijapata ngoma yenyewe ambayo itatoka lakini mpaka sasa hivi ngoma ambayo inaleta upinzani ni nyimbo ambayo nimefanya na King Kiki na Joh Makini na pia bado narekodi kwahiyo u never know.”

HATIMAYE KITUO CHA REDIO CHA BBC CHANASA SAUTI ADIMU YA BI. REGINA MWALEKWA

Wakiwa wenye Nyuso za Furaha.Watangazaji mahiri wa Radio na Televisheni,Bi.Regina Mwalekwa aliyekuwa mtangazaji wa Radio One na baadae akahamia Clouds FM/TV na sasa amejiunga na Shirika la Utangazaji la BBC akiwa na mtangazaji mwenzake kutoka kituo cha televisheni cha ITV/Radio One Bi.Fatma Almas Nyangasa,kama walivyonaswa na Camera yetu ndani ya viwanja vya maonyesho ya Saba saba yanayoendelea hivi sasa jijini Dar. Bi Regina Mwalekwa kwa sasa sauti yake itakuwa ikisikika rasmi kupitia kituo cha redio cha BBC. Tunamtakia kila lakheri katika kituo chake kipya cha kazi.

Bi.Regina Mwalekwa akifanya mahojiano na mmoja wa washiriki wa maonyesho ya biashara ya Kimataifa ya Saba saba yanayoendelea katika viwanja vya Mwal. Julius Nyerere jijini Dar.

SAFARI YA MWISHO YA MWANAHABARI NGULI NCHINI, MZEE NKWABI NG’WANAKILALA

Mwanahabari wa Reuters nchini Bw. Fumbuka Ng’wanakilala (aliyebeba msalaba), pamoja na wadogo zake, Lugendo (kushoto) na Manyanda (kulia), wakiwaongoza waombolezaji waliobeba jeneza lenye mwili wa Baba yao, Marehemu Mwl. Nkwabi Ng’wanakilala baada ya kuwasili nyumbani kwao Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Julai 01 mwaka huu, kwa ajili mazishi. Mwl. Ng’wanakilala, ambaye alikuwa Mhadhiri katika Idara ya Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), jijini Mwanza alifariki Juni 27, katika Hospitali ya Bugando baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo na tumbo. PICHA ZOTE/JOHN BADI

Mzee Nkwabi Ng’wanakilala enzi za uhai wake.

Ndugu, jamaa na waombolezaji wakilitelemsha jeneza lenye mwili wa Mwl. Ng’wanakilala kutoka kwenye gari baada ya kuwasili nyumbani Kibamba.

Sehemu ya waombolezaji wakiwa msibani Kibamba

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO BW. Raphael Hokororo (kati) akiwa na wadau wa habari waliokuwepo mazishini

TANZANIA YATAJWA MIONGONI MWA NCHI 35 ZENYE VIKOSI BORA ZAIDI VYA KIJESHI DUNIANI

Pichani ni kikosi cha wapiganaji wa kitanzania ambao wanaunda kikosi cha umoja wa mataifa nchini DRC wakiwa kazini.

Tanzania ni nchi peke ya Kiafrika ambayo imetajwa kati ya nchi 35 ulimwenguni yenye vikosi imara vya kijeshi {Special Fource}. Hutafiti huu umetokana na kazi nzuri ambayo imefanywa na vikosi hivyo nchini Kongo DRC.

Moja ya sifa zilizoangaliwa ni nidhamu, uwezo wa vifaa ikiwemo utayari wa vikosi hivyo kupambana katika mazingira magumu, kuokoa mateka na kukamata maharamia wakiwemo magaidi.

Taarifa hizi ambazo zimenukuliwa kutoka mtandao wa www.atchuup.com ambao ni maarufu kwa kuandika habari za teknologia ya kivita na kijasusi, zimeonya na kuyaonea huruma makundi ya waasi na kigaidi ambayo yatalazimika kupambana na vikosi hivi.

MONUSCO FIB commander Brig Gen. James Mwakibolwa akiwapokea wapiganaji wa kikosi cha kutuliza na kupokonya silaha makundi ya waasi Mashariki ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC walipo wasili katika mji wa Goma

 

Wapiganaji wa Tanzania wanao undakikosi cha kutuliza na kupokonya silaha makundi ya waasi Mashariki ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC walipo wasili katika mji wa Goma

 

Wapiganaji Tanzania wanao hunda kikosi cha kutuliza na kupokonya silaha makundi ya waasi Mashariki ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC walipo wasili katika mji wa Goma PICHA NA MONUSCO