MWANA FA KUJA NA VIDEO YA MFALME WAKATI UJIO MPYA WA G-NAKO WASUBIRIWA…

MWANA FA ft.G NAKO - MFALME www.allstartz.blogspot.com

Msanii wa Hip Hop, Hamis Mwinjuma aka Mwana FA anatarajia kuachia video ya wimbo wake ‘Mfalme’ aliomshirikisha G-Nako baada ya kushoot video hiyo nchini Kenya.

G-Nako, alinukuliwa jana akisema kuwa Mwana FA alikuwa na idea ya video hali ambayo ilisaidia video hiyo kufanyika kwa muda mfupi. “Director ambaye tumefanya naye video ni yule ambaye alishoot video ya AY, Asante anaitwa Kevin Bosco. Director alikuwa na mawazo yake na Mwana FA alikuwa na mawazo yake, kilichofanyika kizuri ni yale mawazo yaliwekwa pamoja halafu yakauwishwa, kwahiyo nazani kila kitu kilienda sawa,” alisema G.

Wakati huo huo rapper huyo alizungumzia ujio wa single yake mpya baada Joh Makini na Nick Pili kuachia kazi zao.

“Kazi zangu zinakuja na unajua sisi namna tunafanya kazi huwa tunapeana muda kidogo ambao akitoa mtu upatikane muda wa watu wasikilize, kwasababu mara nyingi watu wanatuconfuse kutuweka kama kundi, lakini sisi ni kampuni na vilevile kila mtu anakuwa na project zake,” alisema. “Kwahiyo kazi zangu zinakuja na hapa katikati ulisikia kazi yangu na Godzilla inaitwa ‘Tumewaka ‘ nayo inafanya vizuri nafikiri naipa muda kidogo halafu nafikiri baada ya mwezi wa Ramadhani kwisha hapo mbele kidogo tu nitaachia ngoma. Mgoma zipo nyingi ila sijapata ngoma yenyewe ambayo itatoka lakini mpaka sasa hivi ngoma ambayo inaleta upinzani ni nyimbo ambayo nimefanya na King Kiki na Joh Makini na pia bado narekodi kwahiyo u never know.”

Advertisements